Blazing Inferno
Member
- May 10, 2021
- 25
- 24
Habari wakuu.
Tunapozungumzia kufundisha Literature tunazungumzia walimu wabobevu wa lugha ya kiingereza kwasababu hakuna fasihi bila lugha.
Kwa muda mrefu nimekua nikitatizwa na upungufu wa walimu wa somo la English literature mashuleni. Hivyo nimesukumwa kufuatilia suala hili kwa undani na kwa utafiti wangu mdogo nilioufanya kwenye websites na prospectus za vyuo mbalimbali nimegundua kua course za literature zinatolewa na vyuo vichache sana.
Vyuo vingi vinajumuisha Literature ndani ya course za English mfano unakuta Bachelor of Arts With Education (Geography & English) English literature inajumuishwa kidogo sana ndani ya English kitu ambacho kinapelekea kushindwa kutengeneza walimu ama wataalamu madhubuti wa fasihi ya lugha ya kiingereza.
Ikumbukwe kwamba fasihi ni pana sana na inahitaji isomwe kwa upana wake na si kama ifanywavyo kwamba mwalimu wa fasihi atasoma poetry kidogo, drama kidogo na prose kidogo bila kuzama ndani zaidi. Suala hili linatengeneza walimu ambao si competent kwenye literature na wengi wao hujikuta katika hali ya kujilazimisha kufundisha somo hili mashuleni bila kuwa na utaalamu wa kutosha.
Ukija vyuoni pia utakuta walimu wa literature ni wachache sana kwasababu vyuo havitoi kipaumbele kwenye course hii.
Literature ni muhimu sana na ina opportunities nyingi ambazo bado vijana wengi hawazijui na kwa kusema hivyo ningependa kushauri vyuo vikuu vyenye social sciences au language centers kuandaa utaratibu wa kuanzisha degree programmes za literature.
Wasalam.
(NB: Mada hii ni ndefu na pana sana inahitaji majadiliano ya kina na kwa bahati mbaya nimeandika hapa JF kwa haraka ili angalau kufikisha ujumbe. Itapendeza zaidi kama kuna wataalamu wengine hapa waiongelee kwa mawanda mapana)