Uhaba wa DOLA (U.S.D) Tanzania na ukimya wa Serikali

Kwa ufupi Dollar nyingi zitakuja endapo tutakopa pesa zaidi au tusubirie msimu wa watalii
Kukopa sio njia nzuri, madeni yakizidi pia ni hatari kwa taifa.
Ninaamini njia nzuri na ya dharura kwa Tanzania ni kuongeza uzalishaji wa bidhaaa za kilimo na kupunguza uagizaji wa bidhaa zinazoweza kuzalishwa hapa nchini kama mafuta ya kula, mbolea, bidhaa za ngozi, bidhaa za katani, pamba, chikichi na tumbaku nk.
Njia hii itasaidia fedha za kigeni zinazoingia zisitoke kwa wingi bali kwa vitu vya lazima pekee.

Vitu hivi vikiwekewa mkazo vinaweza kuzalishwa hapa nchini kwa kiwango cha kutosheleza na kuzidi, shida ni UBINAFSI wa viongozi wetu.
 
Kihesabu; ina tafsiri ya kuwa, tunatumia sana vitu vya nje kuliko wao kutaka vya kwetu.
Ningekuwa na maamuzi; biashara zote za kuagiza vitu nje na kuingiza nchini ningezipiga chini, na kuwapa kipaumbele wale wote wanaofanya biashara ya kupeleka vitu nje.​
 
Pia nishati ya mafuta inakula fedha ya kigeni wakati wao hawazalishi fedha za kigeni (sheli); zipunguzwe
 
Kuna siku nilienda kufanya TT benki fulani hapa Kariakoo sokoni ikawa pesa ya charge imepungua, nikawauliza dola ngapi inahitajika wakanambia dola 40 na uzuri nilikuwa na TSH nikawaambia niuzieni hizo dola 40 wakasema dola hawana, imagine dola 40 benki hawana?
 
Tuliambiwa tunaachana na uchumi wa mabeberu. Tutumie pesa ya China na Urusi.
 
Mazao ya biashara tumeyazingua sana
 
Hili ndio suruhisho, mengineyo ni kuzunguka mbuyu na hii iambatane na technology upgrading ya nchi.
 
Shida ni watu.... serikali haifanyi biashara
 
Team Russia ndiyo muda wenu wa kuleta currency yenu ya Russia au China Ili mpindue meza vzr
 
Chawa wapo humu kusema kumkimgia saa100 kifua kuwa ni swala la kidunia
 
Wakati bandari tu mama anataka kuziuza maana zimeshaamshinda itakuwa hiyi migodi
 
Utaitwa dictata Na kupewa Kila aina baya kuwa unaua biashara za watu
 
Utaitwa dictata Na kupewa Kila aina baya kuwa unaua biashara za watu
Kama mikakati itapangiliwa vizuri, wengi wataacha biashara ya uchuuzi na kuwekeza kwenye uzalishaji na kusafirisha nje
 
Jana nimekwenda NMB wananiambia kununua dola mwisho USD 500
 
Shida ni watu.... serikali haifanyi biashara
Nathani kuna jambo hulielewi mkuu,
Serikali inatumia zaidi ya 70% ya fedha za kigeni nchini.
Gharama za ujenzi wa reli zaidi ya trillion 10
Gharama za ujenzi daraja la Busisi zaidi ya 700 billion

Gharama za ujenzi wa bwawa la Umeme
La Nyerere zaidi ya trillioni 7

Ujenzi wa barabara na madaraja unaofanywa na kampuni za nje
Uagizaji wa mafuta ( petrol, diesel nk)
Ulipaji wa deni la taifa

Hayo yote yanafanywa na serikali kwa fedha za kigeni sio Tsh.
 
Hivi haya mahundi nakadharika vinavyoenda nchi za afrika mashariki mfano Kenya, wafanyabiashara wetu wanauza kwa dola kweli?
 
Hivi haya mahundi nakadharika vinavyoenda nchi za afrika mashariki mfano Kenya, wafanyabiashara wetu wanauza kwa dola kweli?
Wananunua kwa pesa ya Kenya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…