Uhaba wa DOLA (U.S.D) Tanzania na ukimya wa Serikali

Uhaba wa DOLA (U.S.D) Tanzania na ukimya wa Serikali

Tarehe 08 Juni 2023 nilienda katika benki moja kubwa TU hapa nchini,ambayo kwa miaka yote ya kazi zangu hua naitumia kwa ajili ya malipo ya ununuzi wa nje ya nchi.
Nikiwa na fomu zangu za TT kwa ajili ya kufanya malipo kwa fedha ya USD niliambiwa,"unafahamu kua hakuna usd?".
Hakuna USA Kwa zaidi ya wiki mbili Sasa"je unaweza kulipa kwa Yuan? Maana hizo tunazo nyingi".
Niliwaeleza umuhimu wa shida yangu,wakaanza kupigana simu ofisini,mazungumzo yalikua ni kua hakuna USD.
Maneno waliyokua wakiongea hawakujua kama najua kinachoendelea duniani.

Sitaki kusema mengi lakini USD imeadimika.
Nasikia hata wabunge walihoji Hali hiyo.
Je Putin ndio chanzo Cha kuadimika Dola au,wachumi naomba mje mtoe ufafanuzi plz.
 
Hivi kuna U.S.A
U.S.B
na
U.S.D?
sasa wew bank ulifata nin U.S.D au U.S.C
maana nikiangalia hapo kinachokosekana bank ni U.S.C pekee
 
Kumekuwa na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni hapa Tanzania hasa USD ambayo ndio hutumika sana kwa malipo kwa biashara za kimataifa.

Pamoja na kupanda kwa dola na kushuka kwa shilingi kutoka 2375 mpaka 2405 bado imekuwa shida sana kupatikana.

Kwanza ilianza mabenki kuweka ukomo wa kununua dola mpaka 5000 USD pekee. Na sasa wameweka ukomo wa 1000 USD pekee.

Maduka ya kubadilisha fedha za kigeni hakuna dola, Benki hazina dola, wafanyabiashara hawana dola Serikali iko kimya na hakuna hatua za dharura zinazochukulia kunusuru hali hii mbaya kiuchumi.

Sasahivi ukihitaji dola 30,000 inabidi uzunguke kwenye mabenki karibu mwezi mzima ili kuzipata
Hali hii imekuwa changamoto sana kwa wafanyabiashara (Waagizaji)

Nauliza hii nchi tuna Serikali?!
Tuanze kuzoea kuuza na kununua kwa fedha yetu!
 
Naweza nikaita hii ni propaganda, si china wala uturuki inayoweza zuia matumizi ya Dola hata North Korea, yaani unajaribu kusema kuwa ukienda na Dola kwenye hizo nchi ukichenji benki zitakataa?

Kilichopo Tanzania kuna upungufu WA foreign reserve fuatilia data za BOT utaona.

Hifadhi ya fedha za kigeni Tanzania Kwa sasa inatosheleza miezi minne Tu kipindi cha wakati 2022 ilikuwa miezi mitano mpaka sita(ripoti ya mwezi April 2023)
Hapa sasa umeongea kisomi na sio story za hawa wengine.
 
Ngoja nikusaidie mkuu,

Bibi yako unayemwongelea nina imani anavaa nguo, hizo nguo zinatoka China nk
Unahitaji dola kuzinunua na kuzileta hapa ili bibi
anunue na azivae.

Bibi yako akiumwa anatumia dawa lakini hatuna viwanda vingi vya dawa, zinaagizwa nje
Ili bibi azipate ni lazima ziagizwe nje kwa dola.

Umesema bibi yako anahitaji mahindi
Ili upate mahindi unahitaji mbolea
Serikali yako inaagiza mbolea nyingi nje ya nchi kwa kutumia dola.

Bibi yako anasafiri sio?
Magari, pikipiki nk yanatumia mafuta lakini hatuchimbi mafuta, serikali inatumia fedha nyingi sana (dola) kuagiza mafuta ili bibi yako apande gari kwenda sokoni kununua mahitaji uliyoorodhesha.
Yapo mengi sana lakini nadhani nimetumia lugha rahisi na utakuwa umenielewa.
Asipokuelewa na hapa mchape kibao.
 
Kukopa sio njia nzuri, madeni yakizidi pia ni hatari kwa taifa.
Ninaamini njia nzuri na ya dharura kwa Tanzania ni kuongeza uzalishaji wa bidhaaa za kilimo na kupunguza uagizaji wa bidhaa zinazoweza kuzalishwa hapa nchini kama mafuta ya kula, mbolea, bidhaa za ngozi, bidhaa za katani, pamba, chikichi na tumbaku nk.
Njia hii itasaidia fedha za kigeni zinazoingia zisitoke kwa wingi bali kwa vitu vya lazima pekee.

Vitu hivi vikiwekewa mkazo vinaweza kuzalishwa hapa nchini kwa kiwango cha kutosheleza na kuzidi, shida ni UBINAFSI wa viongozi wetu.
Hii paragraph ya mwisho umemalizia vizuri.
 
Chawa wapo humu kusema kumkimgia saa100 kifua kuwa ni swala la kidunia
.
Screenshot_20230314-142310_100653.jpg
 
Yuan kama unataka kuagiza kitu China tu lakini nchi nyingi hawaitambui.
 
Mi nazan tuiombe marekani baada ya tsh tutumie dollar shiling tuikane kwa muda
 
Back
Top Bottom