lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,475
Tuanze kuzoea kuuza na kununua kwa fedha yetu!Kumekuwa na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni hapa Tanzania hasa USD ambayo ndio hutumika sana kwa malipo kwa biashara za kimataifa.
Pamoja na kupanda kwa dola na kushuka kwa shilingi kutoka 2375 mpaka 2405 bado imekuwa shida sana kupatikana.
Kwanza ilianza mabenki kuweka ukomo wa kununua dola mpaka 5000 USD pekee. Na sasa wameweka ukomo wa 1000 USD pekee.
Maduka ya kubadilisha fedha za kigeni hakuna dola, Benki hazina dola, wafanyabiashara hawana dola Serikali iko kimya na hakuna hatua za dharura zinazochukulia kunusuru hali hii mbaya kiuchumi.
Sasahivi ukihitaji dola 30,000 inabidi uzunguke kwenye mabenki karibu mwezi mzima ili kuzipata
Hali hii imekuwa changamoto sana kwa wafanyabiashara (Waagizaji)
Nauliza hii nchi tuna Serikali?!
Hapa sasa umeongea kisomi na sio story za hawa wengine.Naweza nikaita hii ni propaganda, si china wala uturuki inayoweza zuia matumizi ya Dola hata North Korea, yaani unajaribu kusema kuwa ukienda na Dola kwenye hizo nchi ukichenji benki zitakataa?
Kilichopo Tanzania kuna upungufu WA foreign reserve fuatilia data za BOT utaona.
Hifadhi ya fedha za kigeni Tanzania Kwa sasa inatosheleza miezi minne Tu kipindi cha wakati 2022 ilikuwa miezi mitano mpaka sita(ripoti ya mwezi April 2023)
Ukiitwa mpuuzi usilalame.Daaah eti hali ni mbaya sana.kwani bibi yng kule masoko inamsIdiaje iyo dola? Mahindi,mtama,dagaa ananunua kwa dola.mpk useme ivyo.
Asipokuelewa na hapa mchape kibao.Ngoja nikusaidie mkuu,
Bibi yako unayemwongelea nina imani anavaa nguo, hizo nguo zinatoka China nk
Unahitaji dola kuzinunua na kuzileta hapa ili bibi
anunue na azivae.
Bibi yako akiumwa anatumia dawa lakini hatuna viwanda vingi vya dawa, zinaagizwa nje
Ili bibi azipate ni lazima ziagizwe nje kwa dola.
Umesema bibi yako anahitaji mahindi
Ili upate mahindi unahitaji mbolea
Serikali yako inaagiza mbolea nyingi nje ya nchi kwa kutumia dola.
Bibi yako anasafiri sio?
Magari, pikipiki nk yanatumia mafuta lakini hatuchimbi mafuta, serikali inatumia fedha nyingi sana (dola) kuagiza mafuta ili bibi yako apande gari kwenda sokoni kununua mahitaji uliyoorodhesha.
Yapo mengi sana lakini nadhani nimetumia lugha rahisi na utakuwa umenielewa.
Hii paragraph ya mwisho umemalizia vizuri.Kukopa sio njia nzuri, madeni yakizidi pia ni hatari kwa taifa.
Ninaamini njia nzuri na ya dharura kwa Tanzania ni kuongeza uzalishaji wa bidhaaa za kilimo na kupunguza uagizaji wa bidhaa zinazoweza kuzalishwa hapa nchini kama mafuta ya kula, mbolea, bidhaa za ngozi, bidhaa za katani, pamba, chikichi na tumbaku nk.
Njia hii itasaidia fedha za kigeni zinazoingia zisitoke kwa wingi bali kwa vitu vya lazima pekee.
Vitu hivi vikiwekewa mkazo vinaweza kuzalishwa hapa nchini kwa kiwango cha kutosheleza na kuzidi, shida ni UBINAFSI wa viongozi wetu.
.Chawa wapo humu kusema kumkimgia saa100 kifua kuwa ni swala la kidunia