Uhaba wa fedha wakwamisha vikao vya Bunge la Afrika Mashariki

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) limetangaza kuahirisha vikao vyake kwa muda usiojulikana kutokana na changamoto za kifedha

Hali hiyo ya kifedha imesababishwa na baadhi ya nchi wanachama kushindwa kulipa michango yao ya deni hali iliyoathiri vikao vikao vya bunge vilivyokuwa vimepangwa kufanyika kuanza Januari hadi Juni 2025.

1739108273584.png
Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Februari 7, 2025, jijini Arusha na Afisa Habari wa EALA, Nicodemus Ajak Bior, uamuzi huu umefikiwa baada ya kikao cha Kamisheni ya EALA na Viongozi wa Kamati kilichoketi Februari 6, 2025.

Kutokana na hali hiyo, Spika wa EALA, Joseph Ntakarutimana, amesema ameshafanya majadiliano na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la EAC, Beatrice Asukul Moe, na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Veronica Mueni Nduva, ili kuhimiza Nchi Wanachama ambazo bado hazijalipa michango yao kulipa deni lao haraka ili kuwezesha bunge kuendelea na shughuli zake.

Matazamio ya Spika Ntakarutimana ni kuwa hali hiyo itakuwa imepatiwa ufumbuzi ndani ya Wiki tatu zijazo.

Taarifa hiyo ilisisitiza kwamba EALA itaendelea kujitolea katika kutimiza jukumu lake la kukuza umoja wa kikanda kupitia Sheria, Usimamizi, na Uwawakilishi.

EAC inaundwa na Mataifa nane ambayo ni Tanzani, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Somalia.
 
Kingo si ijitolee madini wauze!
 
Walioingia kibabe jana Dar kwenye mkutano wametoa michango au nako wanaendeleza ubabe?
 
📌📌EBU TUJUZANE UKITOA POSHO NA MARUPURUPU NA DIPLOMATIC PASSPORT HAO WABUNGE NA HILO BUNGE LINA KIPI CHA KUISAIDIA HII JUMUIYA ILIYO ICU.

HILO BUNGE LINGEKUWA NA TIJA KIKAO CHA JANA KUJADILI M23 NA DRC KILIKUWA HAKINA UMUHIMU.

📌📌📌MUNGU ASAIDIE WAENDELEE KUKOSA HELA MAANA HAKUNA KITU WANAFANYA KWENYE HUO MKUSANYIKO WAO!!!

KATI YA HAWA VIPOFU NANI WA KUMUONGOZA MWENZAKE😂😂😂.

Back
Top Bottom