Uhaba wa madarasa, wanafunzi madarasa mawili tofauti ndani ya jengo moja, walimu wawili wafundisha muda mmoja

Uhaba wa madarasa, wanafunzi madarasa mawili tofauti ndani ya jengo moja, walimu wawili wafundisha muda mmoja

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Walimu wawili wakifundisha katika jengo moja lenye wanafunzi wa madarasa tofauti, la pili na la tatu katika Shule ya Msingi Ifua, Kitongoji cha Ifua wilayani Kilolo, mkoani Iringa

Jengo lenyewe choka mbaya, limejengwa kwa matope, hamna Cha sakafu Wala Nini! Ni Kama karne ya 17 duuh!..​

IMG_20210804_115031.jpg
 
Jimbo gani hilo.Umasikini wetu ni mtaji kwa wanasiasa.Halafu mtu anasema nitagawa laptop kila while huku vyoo shida
 
Hivi lile sanamu la yule marehemu limeshaanza kujengwa
 
Nimeshangaa sana kwa akili hiyo waliyotumia
Hivi kweli ukiangalia hiyo clip wakati wote wawili wanaongea unaelewa chochote hapo?
Imagine ndio mwanafunzi halafu mtoto ataelewa nini hapo maana sikio moja huku lingine huko

Hii ni aibu kama ni tozo zetu za kiuzalendo basi hela zangu ziende huko ingawa najua wanazila wengine

Viongozi hawana hata habari
 
Huko nkoa ya Ntwara, kuna shule, darasa moja, wanakaa wanafunzi wa awali, darasa la kwanza na la pili kwa wakati mmoja chini ya mwalimu mmoja tu. Walimu walikuwa watatu darasa la awali mpaka la saba. Hivi sasa wameongeka walimu wawili sasa wametimia watano.
 
Hata community ya hapo inaoneka ipo chini Sana kujua umuhimu wa elimu bado inasubiria wanasiasa wawatatulie changamoto zao.Kwa afrika si ajabu kukuta mmoja wa mzawa wa kijiji hicho ni tajiri Mkubwa tu mjini,moyo wa kusaidia tulipotoka hatuna watz.
 
Huko nkoa ya Ntwara, kuna shule, darasa moja, wanakaa wanafunzi wa awali, darasa la kwanza na la pili kwa wakati mmoja chini ya mwalimu mmoja tu. Walimu walikuwa watatu darasa la awali mpaka la saba. Hivi sasa wameongeka walimu wawili sasa wametimia watano.
Hatari sana kodi zetu zinatumika kumkamatia Mbowe ambae sie tija kwa mlipa kodi wala tishio la nchi.Hapo si watoe hata milioni 5 tu kwa nguvu ya wananchi yanapatikana madarasa 5.Kama v8 moja tu la mkurugenzi linakunywa lita 2000 kwa mwezi SAwa na kodi yetu milioni 4 na laki 8 imechomwa kwenye dizeli si mkurugenzi apaki v8 apande daladala hio pesa atakayookoa kwa mwezi huo inatosha kabisa kupata madarasa 5 kwa ajili ya future ya watoto hao.
 
Uchumi wa kati,tulieni tunajenga nchi kwanza!miaka zaidi ya 50 ya kutawaliwa na chama dola bado hali hii ipo nchini!pesa ya kujenga shule wasubiri ila pesa ya kugharimia kesi ya Mr.Mbowe ipo nyingi tu,IGP nyumba za ibada unakwenda kufanya nini?
 
Kilolo kwenye utajiri wa miti, chai na maparachichi?
Wazazi wajiongeze.
Wazazi wa kinondoni ,temeke ilala nk walijiongeza kupata miundombinu mizuri ya kusomea watoto wao? au hao wakilolo sio walipa kodi au sio wananchi?
 
Kazi ya kodi zetu ni nn hasa,kuna wanafunzi walifukiwa kifusi wakichimba kifusi kwa ajili ya ujenzi wa choo cha shule,ummy akaishia kuwahamisha walimu wote pale hii ni aibu sana kwa wanasiasa.
 
Wazazi wa kinondoni ,temeke ilala nk walijiongeza kupata miundombinu mizuri ya kusomea watoto wao? au hao wakilolo sio walipa kodi au sio wananchi?

Faida ya kuingoja serikali nadhani umeiona sasa. anza, serikali ije kukuunga mkono. maeneo mengi wamefanya hivyo na wamefanikiwa. siamini kama ni kilolo, maana watu wa kilolo ni wapenda maendeleo sana.
 
Ndalichako Joyce, ndalichako Joyce, ndalichako Joyce 🧐
Ndalichako hata habari Hana kwasababu mtoto wake anasoma kwenye academy nje ya nchi.
Huku Kilolo kulikua na mkurugenzi mmoja mwanamke anayejiskia sana kumbe alikua hatimizi majukumu yake.
Now we know
 
Back
Top Bottom