Uhaba wa sukari: Taasisi ipi ilipaswa kuona mapema (early warning systems) lakini haikuona?

Uhaba wa sukari: Taasisi ipi ilipaswa kuona mapema (early warning systems) lakini haikuona?

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Kama nchi, kuna mahali mfumo ulishindwa kufanya kazi sawasawa. Either Bodi ya Sukari, au Taasisi ya Takwimu au Vitengo ndani ya wizara.

Nani hakufanya nini ambacho alitakiwa kufanya? Na katika sekta nyingine mbali na sukari, mifumo yetu ina njia za kutoa tahadhari kwa viongozi?

Iwe ndani ya mahakama, jeshi, ardhi, ustawi wa jamii, lishe, afya, mifumo imekaaje katika kutoa tahadhari na ni kwa namna gani inawasiliana? Sasa hivi kuna janga kubwa la kansa, pale ocean road inasemekana wagonjwa wa kansa wengi wanatoka kanda ya ziwa, shida nini? Migodi ya kienyeji inayotumia kemikali na inapakana na mashamba ya watu? Uvuvi haramu wa kutumia kemikali? Tunafanyaje kudhibiti?

Sina wasiwasi na uwezo wa Bashe, yuko vizuri kwa asilimia 100, ila hili linaweza kuwa angalizo kwake akazie suala la tathmini na taarifa kwa wakati.
 
Usipate tabu na haya mambo. Asilimia kubwa ya matatizo ya nchi hii yanatengenezwa kisiasa ili kumnufaisha/kuwanufaisha mtu/watu fulani. Mwisho wa siku utasikia CCM imemaliza tatizo la sukari wakati chanzo au waliotengeneza tatizo ni wao.
 
Mifumo yetu ya nchi haipo vizuri nadiriki kusema ivyo kwenye mambo mengi ya nchi,mpaka litokee jambo ndio utaona udhaifu wetu
 
Back
Top Bottom