Hio ndio hali inayoendelea. Rais Mwinyi alikuja na nia njema kabisa akitaka kujitofautisha na watangulizi wake. Nia hio ilionekana mapema. Sasa watu wanajiuliza kulikoni ile spidi haionekani kuendana na alichomaanisha hadi sasa kunani?
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu mbali mbali vya tathmini, Rais Mwinyi anakutana na changamoto za kimya kimya kutokana na sababu mbali mbali.
Uhafidhina: Hakuna kipya chini ya uhafidhina Zanzibar. Waliopewa nafasi kwenye Serikali zilizopita wote ni CCM na waliomuweka au kuchangia Rais Mwinyi KUINGIA MADARAKANI NI HAO HAO. Ni kawaida Serikalini Zanzibar, Kusikia kwamba " muache, atatulia mwenyewe" Wanavyotaka wahafidhina unakuwa ndio msimamo wa chama hata kama unavunja sheria. Zanzibar imezoeleka Wahafidhina kuwa juu ya sheria na kuachwa. Hali hii imevikumba hata vyombo vya ulinzi kuwashughulikia wahalifu ambao hujiegemeza kwenye chama na kulindwa.
Nia njema ya Dkt Mwinyi inaishia kwenye matamko na utekelezaji ukishushwa chini kwenye kunasua sua tu. Huo ndio uhalisia.
Kujuana na Deko
Zanzibar kumezidi watu kuajiriwa na kupewa nafasi kwa kujuana. Hata Dkt Mwinyi Mwenyewe anajua hili na amewahi kulisemea. Kila unayemgusa ana mtu na analindwa kwa mwavuli wa undugu na uchama. Bahati mbaya CCM Zanzibar ilibeza uwezo na kutoajiri wenye sifa. Kuna nongwa na visasi kila mtu kumpendelea wake. Kichaka kikubwa ni chama. Ubadhirifu na wizi umeota mizizi kwenye awamu zote na kila aukijaribu kuchukua hatua unakwama.
Ziko wapi Ripoti za Uchunguzi za ubadhirifu za wizi na ajira hewa kwenye SMZ AMBAZO TILIAMBIWA KUMEUNDWA TUME?
Nani wamewajibibishwa kwa dhati kwa upotevu wa mamilioni ya miradi mifano ya ZUSP na Uwekaji Taa barabarani na Ununuzi wa Meli ya MV Mapinduzi II?
Hatua gani zimechukuliwa kuwajibishwa kwa wanaolalamikiwa kote mawizarani, Maashirikani, Halmashauri na manispaa?
Hatua gani zimechukuliwa kwa wanaotajwa kwenye Ile Show ya ONGEA NA RAIS MWINYI? tunazo taarifa malamiko ni mengi mno lkn hatuoni hatua?
KUPWAYA KWA WASAIDIZI WAKE
Hiki nacho kinaonekana kwa UWAZI. Spidi imeyayuka hata kwa mawaziri walioanza kujizolea umaarufu. Wamepotea na mambo ni yale yale. Mzigo wa kuwabeba makada walioharibu na kuwawajibisha ni mzito kwa Dkt Mwinyi maana unawahusu CCM.
Katika hali hio, hakuna mpya maana tatizo linajulikana. Huu ni mzigo wa Chama. Chama kimebeba makondokando na kiko tayari kuyalinda.
Uchambuzi unaonesha Kuondoka kwa JPM na Maalim Seif vile vile kumerudisha nyuma jitihada. Nini kitegemewe?
Jee Rais Mwinyi ataweza ? hilo ndio Suali lililopo. Utamaduni wa kulindana, kupeana vyeo na nongwa ni mgumu mno.
Zanzibar kuna shida iliyolelewa kwa muda mrefu na hadi sasa hakuna tiba kutokana na ushindani wa kisiasa na upinzani wenye nguvu kiasi kwamba huo ndio uchochoro wa kupiga kwa sababu unakuwa na uhakika wa kulindwa.
Tunakaribisha mjadala kwa aliye na la kusema.
Kishada.