Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Exactly, tena ukizingatia wanamchukulia kama ni mbara aliyepandikizwa ndio kabisa.Ktk Rais ambaye hana confidence na kiti chake ni Mwinyi. Maana hata watumushi chini yake wanajua Abcd za namna alivyo upata. Hana ubavu hata kidogo wa kuwayumbisha
Sikubaliani na wazo lakoHivi ulitegemea rais aliyeingia madarakani kwa wizi wa kura na umwagaji damu awe na nguvu zipi za kuhoji, na hata kuchukua hatua? Uzuri ni kuwa rais, pamoja na anaowahoji wanajua kabisa kaingia madarakani kwa mbeleko. Akiwachukulia hatua, uchaguzi unaofuata hawezi kushinda huo urais bila mbeleko.
Specific Kwa Zanzibar. Hali ni tofauti na maelezo mengine. Kule chama kinatumika kama kichaka.Sikubaliani na wazo lako
Kwa Afrika Rais anaweza kukuteua umtangaze ku2a Rais ukimaliza unanyea debe gerezani maana hata ukipeleka kesi zako atamteua wa kuzibatilisha.
Tatizo la nchi za kiafrika ni Wizi kwa VIONGOZI wanaingia wakiwa na nia KUPIGA zamu zao, ni mwendonwa KUMEKI.
Jingine ni kukosa UTHUBUTU na UJASIRI bora uwe Mwizi wewe Rais peke yako na kuwathibiti wengine. Wengi wanaona maisha yao , familia na jamaa zao yatakuwa HATARINI hivyo kuamua kujisalimisha na kutumikia KIKUNDI fulani kujitoa mhanga ni jambo ADIMU.
Usaliti wa KIAFRIKA . Waafrika tunatumika na mataifa kutugawa , na miongoni mwetu wapo Agent wako tayari watoe ramani ilimradi tu watahakikishiwa usalama wa maisha yao huko nje au ndani, ukijitoa Mhanga UTANG'OLEWA fasta , utatawala au kuongoza kwa vurugu wanaharakati Uchwara miingoni mwetu wataibuka, hakuna asiye na makosa watayatumia kukumaliza kabisa
Wengi inabidi wanyweee
Magufuli huyu jambazi amaMwinyi, alikuwa anatembelea gia ya Magufuri,na sio Mwinyi tu hata mawaziri wengi wamepotea, Sasahivi mambo yameanza kurudi kawaida,hata maofisini nyodo zimerudi kila saa wako kwenye vikao,Wakina Mwinyi wote ulikuwa moto wa mabua tu.
Unaposema chama kinamfunga miguu sikubaliani nawe kwani kuna maamuzi ya uendeshaji Serikali hayahitaji vikao vya chama, tatizo ninaloliona Urais wa Dr Mwinyi umezongwa na washauri wengi kila mmoja anamvuta rais katika muongozo wake matokeo yake anapoteza dira na kutojua jambo la kufanya, mfano suala la uteuzi wa watendaji hili halihitaji vikao vya chama, suala la kuwajibisha viongozi wazembe hili halihitaji vikao vya chama haya ni mambo yalio ndani ya mamlaka ya RaisKuna shida jamani.
Rais Mwinyi alijitahidi kuziba miaNYA. ALIZUIA UAJIRI MPYA NA KUHAKIKI. Ripoti kimya na hawajawajibishwa watu. Fedha zilipigwa mno kwenye mishahara hewa hasa vinavyoitwa VIKOSi. Mlolongo ni mrefu.
Wateule wa zamani wa Dkt Shein hawajaguswa na hawagusiki.
Kuna uchafu kwenye taasisi nyingi. Viongozi wana skendo nyingi hawagusiki yalikuwa mapendekezo ya Chama.
Chama kinamfunga miguu na Mikono.
Unawajua CCM au unawasikia wewe? Wako tayari kuendele akumhujumu rais wao kuliko kuitoa Sirikali kwa upinzani 😀Hivi ulitegemea rais aliyeingia madarakani kwa wizi wa kura na umwagaji damu awe na nguvu zipi za kuhoji, na hata kuchukua hatua? Uzuri ni kuwa rais, pamoja na anaowahoji wanajua kabisa kaingia madarakani kwa mbeleko. Akiwachukulia hatua, uchaguzi unaofuata hawezi kushinda huo urais bila mbeleko.
Mkuu chama ni mwenendo, imani, utashi na utamaduni.Unaposema chama kinamfunga miguu sikubaliani nawe kwani kuna maamuzi ya uendeshaji Serikali hayahitaji vikao vya chama, tatizo ninaloliona Urais wa Dr Mwinyi umezongwa na washauri wengi kila mmoja anamvuta rais katika muongozo wake matokeo yake anapoteza dira na kutojua jambo la kufanya, mfano suala la uteuzi wa watendaji hili halihitaji vikao vya chama, suala la kuwajibisha viongozi wazembe hili halihitaji vikao vya chama haya ni mambo yalio ndani ya mamlaka ya Rais
Jambazi alikuwa Baba yako,muuza unga, ndio maana alikuwa na chuki na Magufuri, kwenye uko wenu wote mpaka mwisho wa dunia unafika, akuna mtu atakeyefikia cheo cha Magufuri,Jaribu kueshimu watu hata kama umpendi,wewe mbwa.Magufuli huyu jambazi ama
Ya Zanzibar hayatuhusu, kwenye matatizo yenu mnataka tujadili lakini kwenye kula keki yenu hamtaki kutushirikishaHio ndio hali inayoendelea. Rais Mwinyi alikuja na nia njema kabisa akitaka kujitofautisha na watangulizi wake. Nia hio ilionekana mapema. Sasa watu wanajiuliza kulikoni ile spidi haionekani kuendana na alichomaanisha hadi sasa kunani?
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu mbali mbali vya tathmini, Rais Mwinyi anakutana na changamoto za kimya kimya kutokana na sababu mbali mbali.
Uhafidhina: Hakuna kipya chini ya uhafidhina Zanzibar. Waliopewa nafasi kwenye Serikali zilizopita wote ni CCM na waliomuweka au kuchangia Rais Mwinyi KUINGIA MADARAKANI NI HAO HAO. Ni kawaida Serikalini Zanzibar, Kusikia kwamba " muache, atatulia mwenyewe" Wanavyotaka wahafidhina unakuwa ndio msimamo wa chama hata kama unavunja sheria. Zanzibar imezoeleka Wahafidhina kuwa juu ya sheria na kuachwa. Hali hii imevikumba hata vyombo vya ulinzi kuwashughulikia wahalifu ambao hujiegemeza kwenye chama na kulindwa.
Nia njema ya Dkt Mwinyi inaishia kwenye matamko na utekelezaji ukishushwa chini kwenye kunasua sua tu. Huo ndio uhalisia.
Kujuana na Deko
Zanzibar kumezidi watu kuajiriwa na kupewa nafasi kwa kujuana. Hata Dkt Mwinyi Mwenyewe anajua hili na amewahi kulisemea. Kila unayemgusa ana mtu na analindwa kwa mwavuli wa undugu na uchama. Bahati mbaya CCM Zanzibar ilibeza uwezo na kutoajiri wenye sifa. Kuna nongwa na visasi kila mtu kumpendelea wake. Kichaka kikubwa ni chama. Ubadhirifu na wizi umeota mizizi kwenye awamu zote na kila aukijaribu kuchukua hatua unakwama.
Ziko wapi Ripoti za Uchunguzi za ubadhirifu za wizi na ajira hewa kwenye SMZ AMBAZO TILIAMBIWA KUMEUNDWA TUME?
Nani wamewajibibishwa kwa dhati kwa upotevu wa mamilioni ya miradi mifano ya ZUSP na Uwekaji Taa barabarani na Ununuzi wa Meli ya MV Mapinduzi II?
Hatua gani zimechukuliwa kuwajibishwa kwa wanaolalamikiwa kote mawizarani, Maashirikani, Halmashauri na manispaa?
Hatua gani zimechukuliwa kwa wanaotajwa kwenye Ile Show ya ONGEA NA RAIS MWINYI? tunazo taarifa malamiko ni mengi mno lkn hatuoni hatua?
KUPWAYA KWA WASAIDIZI WAKE
Hiki nacho kinaonekana kwa UWAZI. Spidi imeyayuka hata kwa mawaziri walioanza kujizolea umaarufu. Wamepotea na mambo ni yale yale. Mzigo wa kuwabeba makada walioharibu na kuwawajibisha ni mzito kwa Dkt Mwinyi maana unawahusu CCM.
Katika hali hio, hakuna mpya maana tatizo linajulikana. Huu ni mzigo wa Chama. Chama kimebeba makondokando na kiko tayari kuyalinda.
Uchambuzi unaonesha Kuondoka kwa JPM na Maalim Seif vile vile kumerudisha nyuma jitihada. Nini kitegemewe?
Jee Rais Mwinyi ataweza ? hilo ndio Suali lililopo. Utamaduni wa kulindana, kupeana vyeo na nongwa ni mgumu mno.
Zanzibar kuna shida iliyolelewa kwa muda mrefu na hadi sasa hakuna tiba kutokana na ushindani wa kisiasa na upinzani wenye nguvu kiasi kwamba huo ndio uchochoro wa kupiga kwa sababu unakuwa na uhakika wa kulindwa.
Tunakaribisha mjadala kwa aliye na la kusema.
Kishada.
Alichoweza mwendazake nn mbona mnampa sifa sanaaaaaHili linchi alikuwa analiweza mwenda zake tu.
Watanzania tuna utamaduni mbovu sana kwenye swala la uwajibikaji.
Huyu jamaaa mjinga sana sielewi alikuwa anaiwezaje wakati nchi ilimshinda kabisaAlikua anaiwezaje wakati kuna madudu kibao yamefanyika akiwepo yeye