Uhafidhina, Deko na kujuana kwa wana CCM, kunamkwaza Rais Mwinyi Zanzibar

Uhafidhina, Deko na kujuana kwa wana CCM, kunamkwaza Rais Mwinyi Zanzibar

Hili linchi alikuwa analiweza mwenda zake tu.
Watanzania tuna utamaduni mbovu sana kwenye swala la uwajibikaji.
Ubabaishaji na longolongo ni nyingi mno!
Watu wakitoka hapo wanawalaumu viongozi kuwa hawawaletei maendeleo wakati wakwamishaji ni hao hao wananchi.
 
Hio ndio hali inayoendelea. Rais Mwinyi alikuja na nia njema kabisa akitaka kujitofautisha na watangulizi wake. Nia hio ilionekana mapema. Sasa watu wanajiuliza kulikoni ile spidi haionekani kuendana na alichomaanisha hadi sasa kunani?

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu mbali mbali vya tathmini, Rais Mwinyi anakutana na changamoto za kimya kimya kutokana na sababu mbali mbali.

Uhafidhina: Hakuna kipya chini ya uhafidhina Zanzibar. Waliopewa nafasi kwenye Serikali zilizopita wote ni CCM na waliomuweka au kuchangia Rais Mwinyi KUINGIA MADARAKANI NI HAO HAO. Ni kawaida Serikalini Zanzibar, Kusikia kwamba " muache, atatulia mwenyewe" Wanavyotaka wahafidhina unakuwa ndio msimamo wa chama hata kama unavunja sheria. Zanzibar imezoeleka Wahafidhina kuwa juu ya sheria na kuachwa. Hali hii imevikumba hata vyombo vya ulinzi kuwashughulikia wahalifu ambao hujiegemeza kwenye chama na kulindwa.

Nia njema ya Dkt Mwinyi inaishia kwenye matamko na utekelezaji ukishushwa chini kwenye kunasua sua tu. Huo ndio uhalisia.

Kujuana na Deko
Zanzibar kumezidi watu kuajiriwa na kupewa nafasi kwa kujuana. Hata Dkt Mwinyi Mwenyewe anajua hili na amewahi kulisemea. Kila unayemgusa ana mtu na analindwa kwa mwavuli wa undugu na uchama. Bahati mbaya CCM Zanzibar ilibeza uwezo na kutoajiri wenye sifa. Kuna nongwa na visasi kila mtu kumpendelea wake. Kichaka kikubwa ni chama. Ubadhirifu na wizi umeota mizizi kwenye awamu zote na kila aukijaribu kuchukua hatua unakwama.

Ziko wapi Ripoti za Uchunguzi za ubadhirifu za wizi na ajira hewa kwenye SMZ AMBAZO TILIAMBIWA KUMEUNDWA TUME?

Nani wamewajibibishwa kwa dhati kwa upotevu wa mamilioni ya miradi mifano ya ZUSP na Uwekaji Taa barabarani na Ununuzi wa Meli ya MV Mapinduzi II?

Hatua gani zimechukuliwa kuwajibishwa kwa wanaolalamikiwa kote mawizarani, Maashirikani, Halmashauri na manispaa?
Hatua gani zimechukuliwa kwa wanaotajwa kwenye Ile Show ya ONGEA NA RAIS MWINYI? tunazo taarifa malamiko ni mengi mno lkn hatuoni hatua?

KUPWAYA KWA WASAIDIZI WAKE
Hiki nacho kinaonekana kwa UWAZI. Spidi imeyayuka hata kwa mawaziri walioanza kujizolea umaarufu. Wamepotea na mambo ni yale yale. Mzigo wa kuwabeba makada walioharibu na kuwawajibisha ni mzito kwa Dkt Mwinyi maana unawahusu CCM.

Katika hali hio, hakuna mpya maana tatizo linajulikana. Huu ni mzigo wa Chama. Chama kimebeba makondokando na kiko tayari kuyalinda.

Uchambuzi unaonesha Kuondoka kwa JPM na Maalim Seif vile vile kumerudisha nyuma jitihada. Nini kitegemewe?

Jee Rais Mwinyi ataweza ? hilo ndio Suali lililopo. Utamaduni wa kulindana, kupeana vyeo na nongwa ni mgumu mno.

Zanzibar kuna shida iliyolelewa kwa muda mrefu na hadi sasa hakuna tiba kutokana na ushindani wa kisiasa na upinzani wenye nguvu kiasi kwamba huo ndio uchochoro wa kupiga kwa sababu unakuwa na uhakika wa kulindwa.

Tunakaribisha mjadala kwa aliye na la kusema.

Kishada.
Kamchagua mdogo wake kua katibu mkuu
 
MTU mwenye akili timamu hawezi kuacha kuongeza mishahara Kwa miaka mitano mfululizo.
 
Dhalimu alikuwa anaweza nini, yeye mwenyewe alikuwa ni muendesha miradi ya hasara. Alichofanikiwa ni kudhibiti vyombo vya habari na kutangazwa kwa propaganda alizozitaka yeye.
kwa hiyo saiz mnapata habar pesa ya nchi aipigwi sio
 
Kuna shida jamani.

Rais Mwinyi alijitahidi kuziba miaNYA. ALIZUIA UAJIRI MPYA NA KUHAKIKI. Ripoti kimya na hawajawajibishwa watu. Fedha zilipigwa mno kwenye mishahara hewa hasa vinavyoitwa VIKOSi. Mlolongo ni mrefu.

Wateule wa zamani wa Dkt Shein hawajaguswa na hawagusiki.

Kuna uchafu kwenye taasisi nyingi. Viongozi wana skendo nyingi hawagusiki yalikuwa mapendekezo ya Chama.

Chama kinamfunga miguu na Mikono.

Wateule gani hawagusiki wakati kasimamisha wakuu wa vikosi na wakurugenzi kadhaa?

Na jana kaendeleza tena kufumua hawa wakurugenzi.
IMG-20210710-WA0011.jpg



IMG-20210710-WA0010.jpg
 
Una akili kweli wewe? Nchi ya watu milioni 60 unawaona wote vilaza kasoro "cult leader" wako
Hili linchi alikuwa analiweza mwenda zake tu.
Watanzania tuna utamaduni mbovu sana kwenye swala la uwajibikaji.
 
kwa hiyo saiz mnapata habar pesa ya nchi aipigwi sio

Ilipigwa wakati wake, na sasa inapigwa vile vile. Tofauti ya sasa na wakati wake ni unafuu wa habari kupatikana.
 
Ilipigwa wakati wake, na sasa inapigwa vile vile. Tofauti ya sasa na wakati wake ni unafuu wa habari kupatikana.
mm binafsi naona bora wapige msipate habari kuliko wakapiga habar m'mepata lakuwanya amna katiba inawalinda
 
mm binafsi naona bora wapige msipate habari kuliko wakapiga habar m'mepata lakuwanya amna katiba inawalinda

Tusipojua hata hasira ya kutusukuma kufanya kitu itatoka wapi?
 
Wateule gani hawagusiki wakati kasimamisha wakuu wa vikosi na wakurugenzi kadhaa? Na jana kaendeleza tena kufumua hawa wakurugenzi. View attachment 1849256 View attachment 1849260
Unaposema chama kinamfunga miguu sikubaliani nawe kwani kuna maamuzi ya uendeshaji Serikali hayahitaji vikao vya chama, tatizo ninaloliona Urais wa Dr Mwinyi umezongwa na washauri wengi kila mmoja anamvuta rais katika muongozo wake matokeo yake anapoteza dira na kutojua jambo la kufanya, mfano suala la uteuzi wa watendaji hili halihitaji vikao vya chama, suala la kuwajibisha viongozi wazembe hili halihitaji vikao vya chama haya ni mambo yalio ndani ya mamlaka ya Rais
Mkuu chama ni mwenendo, imani, utashi na utamaduni.

CCM Zanzibar ina huo mwenendo na utamaduni Wa kuleana.

Kila mmoja anamuogopa Mwenzake na kuhofu makundi. Chama kinashindwa kumpa full sapoti ya kushughulikia walaji na wazembe ma a na wote ni CCM. Wapo hapo Kwa mgongo Wa chama na kujuana Ki familia.

Ukimgusa mtu umegusa maslahi ya chama na Mapinduzi.

Huo ndio
 
Wateule gani hawagusiki wakati kasimamisha wakuu wa vikosi na wakurugenzi kadhaa?

Na jana kaendeleza tena kufumua hawa wakurugenzi.
View attachment 1849256


View attachment 1849260
Mkuu
Wateule gani hawagusiki wakati kasimamisha wakuu wa vikosi na wakurugenzi kadhaa?

Na jana kaendeleza tena kufumua hawa wakurugenzi.
View attachment 1849256


View attachment 1849260
Mkuu unaamini hao ndio wahusika? Hio ni circle ambayo Rais iko mikononi mwake ndio akajitutumua. Lkn jiulize Kwa miaka 5 Waziri aliyepita, Hazina n.k.

Hatua Ganii zimehukuliwa kuwawajibisha waliobariki haya ? Kwa sababu ya kuogopa kukipasua chama analazimika kunywea?

Hii ni miradi ya wakubwa.
 
Mkuu

Mkuu unaamini hao ndio wahusika? Hio ni circle ambayo Rais iko mikononi mwake ndio akajitutumua. Lkn jiulize Kwa miaka 5 Waziri aliyepita, Hazina n.k.

Hatua Ganii zimehukuliwa kuwawajibisha waliobariki haya ? Kwa sababu ya kuogopa kukipasua chama analazimika kunywea?

Hii ni miradi ya wakubwa.

Naelewa sana. Bora huyu anajitutumua.
Aliyepita aliambiwa kwamba kuna magendo yanafanyika uwanja wa ndege, akasema anafaham hilo lakini watu wanaohusika na huo mchezo hawezi kuwagusa.

Unakumbuka pia Mwinyi amefumua JKU, KMKM na maeneo mengine? Naelewa ugumu na changamoto zilizopo mbele yake lakini pia juhudi zake zisibezwe, tusubirie matokeo.

Nnachokubaliana na wewe mfumo wa dekezo na undugu umetamalaki sana visiwani.
 
Back
Top Bottom