Uhafidhina, Deko na kujuana kwa wana CCM, kunamkwaza Rais Mwinyi Zanzibar

Kuondoka kwa JPM na Maalim Seif -------hii ndio sababu nyingine KUBWA
 
Nchi ngumu ile, hapo bado hujazungumzia udini...
 
Mimi Mtanganyika ya Visiwani hayanihusu.
 
Ktk Rais ambaye hana confidence na kiti chake ni Mwinyi. Maana hata watumushi chini yake wanajua Abcd za namna alivyo upata. Hana ubavu hata kidogo wa kuwayumbisha
Exactly, tena ukizingatia wanamchukulia kama ni mbara aliyepandikizwa ndio kabisa.
 
Sikubaliani na wazo lako
Kwa Afrika Rais anaweza kukuteua umtangaze ku2a Rais ukimaliza unanyea debe gerezani maana hata ukipeleka kesi zako atamteua wa kuzibatilisha.

Tatizo la nchi za kiafrika ni Wizi kwa VIONGOZI wanaingia wakiwa na nia KUPIGA zamu zao, ni mwendonwa KUMEKI.

Jingine ni kukosa UTHUBUTU na UJASIRI bora uwe Mwizi wewe Rais peke yako na kuwathibiti wengine. Wengi wanaona maisha yao , familia na jamaa zao yatakuwa HATARINI hivyo kuamua kujisalimisha na kutumikia KIKUNDI fulani kujitoa mhanga ni jambo ADIMU.

Usaliti wa KIAFRIKA . Waafrika tunatumika na mataifa kutugawa , na miongoni mwetu wapo Agent wako tayari watoe ramani ilimradi tu watahakikishiwa usalama wa maisha yao huko nje au ndani, ukijitoa Mhanga UTANG'OLEWA fasta , utatawala au kuongoza kwa vurugu wanaharakati Uchwara miingoni mwetu wataibuka, hakuna asiye na makosa watayatumia kukumaliza kabisa

Wengi inabidi wanyweee
 
Specific Kwa Zanzibar. Hali ni tofauti na maelezo mengine. Kule chama kinatumika kama kichaka.

Mifumo yote imedhibitiwa kichama na si uweledi. System yote imejazwa makada ambao hata kama Rais ana nia njema wanamuhujumu kimtindo.

Kwanza siri zinavuja na kujadiliwa vijiweni Kwa CCM. Mila mtu ni mwanamapinduzi.

Wizi na kulindana Tu.
 
Mwinyi, alikuwa anatembelea gia ya Magufuri,na sio Mwinyi tu hata mawaziri wengi wamepotea, Sasahivi mambo yameanza kurudi kawaida,hata maofisini nyodo zimerudi kila saa wako kwenye vikao,Wakina Mwinyi wote ulikuwa moto wa mabua tu.
Magufuli huyu jambazi ama
 
Veting system Haifai. Ukitaka kuleta mabadiliko Zanzibar inabidi uanzie mbali.

Kila kitu kimefujwa Kwa zaidi ya miongo minne sasa, Kama miaka 35 hivi na kuja Kwa vyama vingi.

Zanzibar imeathiriwa na siasa mno.

Wataalamu wengi walifukuzwa makazini, hakukuwa na succession plan. Wat u wakapachikwa kisiasa na kujazwa makazini hapo ndipo tatizo lilipoanzia.

Kuanzia hapo kilichoendelea ni majanga hadi Leo. Akili za wakubwa ni kuingia ikulu Kwa njia yoyote ile.
Sass kulipana fadhila ndio inakuwa mpango mzima.

Its a long story. Itoshe kusema Dr Mwinyi anakwazwa na mila za CCM za kudekezana, uhafidhina na kupendeleana Zanzibar
 
Kwa tathmini ya haraka inaonesha kuwa Rais Hussein Mwinyi hakuwa amejiandaa kuwa Rais wa Zanzibar,hakuwa na ajenda juu ya nini anakusudia kukifanya katika kuiongoza Zanzibar zaidi ya kutegemea mbeleko ya Rais magufuli, kutoijua kwake Zanzibar na watu wake kwa kiasi kikubwa kunamfanya kuonekana kiongozi mgeni asiejua mfumo na miiko ya uongozi wa Zanzibar ni kweli kwa sasa amepwaya sana na amepoteza ile haiba alioanza nayo siku za awali za uongozi wake,miongoni mwa mambo yanayotajwa kumfelisha ni kusikiliza ushauri wa kikundi cha watu kinachojinasibisha na siasa za Jimbo lake la kwahani,watu hao hawana uwezo wa uongozi wala uzoefu katika kusimamia masuala ya uendeshaji wa nchi, kwa hiyo ukiondoa sababu zilizoelezwa na mleta mada zipo sababu hizi ambazo zinamkwaza dr Mwinyi na matokeo yake anaweza kumaliza muhula wake huku kukiwa hakuna hatua kubwa ya maendeleo iliyopigwa huko Zanzibar.
 
Unaposema chama kinamfunga miguu sikubaliani nawe kwani kuna maamuzi ya uendeshaji Serikali hayahitaji vikao vya chama, tatizo ninaloliona Urais wa Dr Mwinyi umezongwa na washauri wengi kila mmoja anamvuta rais katika muongozo wake matokeo yake anapoteza dira na kutojua jambo la kufanya, mfano suala la uteuzi wa watendaji hili halihitaji vikao vya chama, suala la kuwajibisha viongozi wazembe hili halihitaji vikao vya chama haya ni mambo yalio ndani ya mamlaka ya Rais
 
Unawajua CCM au unawasikia wewe? Wako tayari kuendele akumhujumu rais wao kuliko kuitoa Sirikali kwa upinzani 😀

Huyu utawala wake utajaa changamoto mpaka akiamua "kutulia"
 
Kwa hiyo anajitutumua tu.mwisho wa miaka 5 hii utamuona kashazeeka mamvi tele .muulize obama uraisi sio lele mama kuna vitu vingi vipi nyuma ya pazia.
Amewatumbua wale wahasibu 80 waliofukuzwa kazi kwa kuchezea mifumo ya makusanyo.sasa hapo angetaka aendelee angejaza wahasibu kutoka bara huku na wale wazembe awahamishie mikoani ya mbali huku bara kama vile ngara.kiteto.mwanga nk watanyooka tu .lkn kwa kiongea sana wa zenji wanamsikiliza halafu hawatekelezi.mchana wenda kula urojo ndio imetoka hiyo hawarudi tena kazini.
 
Mkuu chama ni mwenendo, imani, utashi na utamaduni.

CCM Zanzibar ina huo mwenendo na utamaduni Wa kuleana.

Kila mmoja anamuogopa Mwenzake na kuhofu makundi. Chama kinashindwa kumpa full sapoti ya kushughulikia walaji na wazembe ma a na wote ni CCM. Wapo hapo Kwa mgongo Wa chama na kujuana Ki familia.

Ukimgusa mtu umegusa maslahi ya chama na Mapinduzi.

Huo ndio mkwazo wenyewe na hio ndio CCM ilivyo Zanzibar.
 
Hawezi tekeleza ipasavyo kile anachoamini kwasababu uenyekiti wa Chama hajapewa!!atawachukuliaje hatua???
 
Tatizo la Zanzibar ni CCM, Zanzibar hakuwezi kutokea mabadiliko as long as CCM ndio inaongoza. Mwinyi hawezi fanya chochote kwa kupitia CCM.
 
Magufuli huyu jambazi ama
Jambazi alikuwa Baba yako,muuza unga, ndio maana alikuwa na chuki na Magufuri, kwenye uko wenu wote mpaka mwisho wa dunia unafika, akuna mtu atakeyefikia cheo cha Magufuri,Jaribu kueshimu watu hata kama umpendi,wewe mbwa.
 
Ya Zanzibar hayatuhusu, kwenye matatizo yenu mnataka tujadili lakini kwenye kula keki yenu hamtaki kutushirikisha
 
Hili linchi alikuwa analiweza mwenda zake tu.
Watanzania tuna utamaduni mbovu sana kwenye swala la uwajibikaji.
Alichoweza mwendazake nn mbona mnampa sifa sanaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…