Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,929
Wadau naomba kuuliza kwa anayejua, uhai ulianzaje?
Uhai umeanzia kwenye maji, (sio maji haya tunayokunywa na kufulia nk) billions of years ago.
Hayo maji (biotic soup) kipindi hicho yalipopigwa na nuru ya jua ya moja kwa moja (the direct sun rays/light) ndipo vitendo vya kikemia vilitendeka kwenye hayo maji (Biotic soup)--- kwa maneno mengine hayo maji (biotic soup/maji uhai) yalikuwa ni mchanyiko wa elements na compounds mbalimbali (ni hizi hizi zilizopo leo duniani)
zilizojikusanya katika mipangilio maalumu mbalimbali na hiyo nuru ya jua ilipozipiga ikawa ndio kichocheo (catalyst) cha hiyo soup kutenda kitendo cha kikemikali na hivyo kutengeneza viumbe hai wa aina mbalimbali kulingana na mchanganyiko wa hiyo biotic soup ulivyokuwepo na ndio maana viumbe hai tupo tofauti na hiyo ni kulingana na aina tofauti za biotic soups.
Nuru ya jua ya moja kwa moja ni ile nuru isiyozuiwa na Ozone layer yaani ni nuru iliyojaa UV rays (Ultra violet rays) na ndio hizi rays zilisaidia reaction katika biotic soup ili viumbe hai wakazaliwa hapa ardhini, Mungu anasema kwenye Qur'an tukufu; Allah amewaotesheni ardhini kama mimea (sikumbuki aya), Pia Amesema; Kila kiumbe hai kimetokana na maji (sikumbuki aya).
Mtu anaweza kuuliza; sasa imekuaje hatuoni tena viumbe wakitokea kama ilivyokuwa hapo awali??-- jibu ni hili; Hivi sasa mwanga wa jua hauji moja kwa moja duniani kama hapo awali, ozone layer inauchuja isitoshe hayo maji ya uhai (biotic soup) hayapo tena kama yalivyokuwa hapo awali na yote yametiririshwa na kuwa bahari hizi tunazoziona leo, hiyo chumvi ya bahari ndio zile elements na compounds zilizotumika kuundia Biotic soups, isitoshe Mungu alitaka mpango huo ufe ili uje mpango mpya wa kuzaliana kwani mpango wa biotic soup ulikuwa ni mpango wa kuzalisha mbegu za viumbe hai (progenitor scheme), na katika hao viumbe hai wa mwanzo (progenitors) kuumbwa kwa njia hiyo walikuwa wote wa kike ndipo hao wakazaa uzao wa kike na kiume.
Katika uumbaji huo wa awali inasemwa mtu ndiye alikuwa kiumbe hai wa mwisho kuumbwa.