Wanabodi,
Mabandiko mengine sio mabandiko ya kitoto!, ukijiona huelewi, we jipitie tuu!.
Angalizo la Alama ya Kuuliza "?".
Mimi mwenzenu jameni, nimewahi kuitwa mahali na kufikishwa mbele ya kamati fulani kwa kutuhumiwa nimesema statement fulani!, kumbe masikini mimi, sikutoa statement, niliuliza tuu!. Aliyenituhumu, hakuiona alama ya kuuliza, hivyo naomba kutoa angalizo la alama ya kuuliza?, bandiko hili sio la statement ni bandiko la swali.
Bandiko hili ni moja ya mabandiko yangu ya dhana dhanifu kuwa kuna uwezekano na huyu naye pia anadanganywa na amedanganyika!.
Leo nimeisikia tena dhana ya uhaini, ikitajwa mahali!, the voices behind inaniambia anadanganywa na amedanganyika!.
Hii issue ya uhaini nimewahi sio tuu kuizungumzia humu, bali nimeiandikia makala
View attachment 3098981 Ijue Katiba ya JMT kwa Jicho la Mtunga Katiba: Watanzania Tusishabikie Uhaini. Hukuna Uhaini wa Kauli na Maneno, Uhaini ni Mipango na Matendo
Humo nilisema
Uhaini Tanzania..., My God!. Kuna Uwezekano Anadanganywa na Kadanganyika?. Mimi ni Tomaso, I Don't Believe This at All!. Sitatizwi na Uongo Wao, Natatizwa na The Motives Behind Such Lies!.
Nimesema hili sio bandiko la watoto kwasababu natafuta the motives behind such lies ili kumjulisha mtu wetu inawezekana kuwa anadanganywa na watu wake, hivyo kama mtu ukidanganywa na watu wako unaowaaminia bila wewe kujua unadanganywa, ukidanganyika sio kosa lako wewe
unaodanganywa,; kwasababu hao wanaokudanganya ni watu wako unao waaminia, hivyo kudanganyika ni halali yako!, ila kosa ni la hao wanao kudanganya, na siku ukiujua ukweli kuwa ulikuwa unadanganywa, ndipo utaelewa kuwa ni kweli hapa duniani kuna watu na viatu, wengine ukiwaona machoni ni kama watu, lakini mioyoni ni mashetani wakubwa wamwaga damu za watu!.
Hii sio mara ya kwanza kwa hao watu kufanya vitendo na madudu ya ajabu ajabu kisha kudanganya mamlaka juu ku justify udhaoimu wao.
Enzi za Nyerere, alikataa na akawatundika msalabani baadhi yao na kuwafagia toka juu mpaka chini, ndio maana enzi za JPM, tulishauri
TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!
Nyerere aligoma kudanganywa, Mwinyi akadanganywa, Mkapa akadanganywa kwenye ubinafsishaji. Jakaya akadanganywa sana tuu kwenye rasilimali zetu.
Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika?
JPM mwanzo aligoma kudanganywa na kudanganyika kwenye rasilimali zetu, akakaza, akabana na kukaba, tukauliza humu ataweza?
Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts? kiukweli JPM alikuwa ni chuma, alikaza, vyuma vikabana, akabana akabana mwisho akaachia!
Mimi ni mtu wa mastori stori, kuna watu wanapenda mastori mastori na wana muda wa kusoma makitu marefu, na kuna wako wako busy hawana time na mastori, wao wanataka vitu short and clear. Wale wa mastori tuendelee, wale wa short and clear, just jump to the conclusion
Baadhi ya matukio ya ajabu ajabu kisha kuvalishwa uongo
Huu uhaini unaoelezwa sasa, ni uhaini wa aina gani?!.
Inawezekana yule Mzee wa watu (Mungu amuweke mahala pema peponi), kwa vile ni mstaafu wa jeshi, anawezekana anahesabika ndiye the strategist, hivyo kuhesabika ni mtu hatari he had to go!. Watekelezaji wakajua tukiharibu sura kwa acid hatatambulika tena!. Mwili umeokotwa Ununio Jumamosi asubuhi, ni polisi wameuchukua na kuu dump mortuary ya hospital ya Mwananyamala. Jumamosi mchana polisi haikutoa taarifa yoyote kuokota mwili wowote, bali Kamanda Musiime alitangaza Jeshi la Polisi kumtafuta huyo Mzee!. Jumamosi usiku ndio ndugu wanautambua mwili!.
Kufuatia kelele nyingi, CinC akatoa amri ya kufanyika uchunguzi wa kina!. Sasa ili kujikosha na kujisafisha, ikabidi itengenezwe script ya movie ya uhaini, ili ku justify kwa CinC why ameshughulikiwa!, wale mnao subiria taarifa ya uchunguzi wa tukio hilo, endeleeni kusubiria, kama ni wasiojulikana, taarifa itatolewa lakini kama ni 'wasiojulikana', tutasubiri sana kama taarifa ya tukio la pyu pyu za Tundu Lissu!.
Binadamu wote ni sawa, thamani ya uhai wa mtu na roho ya mtu, inalingana, huwezi kumtoa mtu uhai kivile, baada ya kelele za kitaifa na kimataifa, unaamua kutunga script ya uhaini!, na kweli jana CinC kakasirika kweli kweli!, yeye hajui kuwa ni script!.
Huu ni ushuhuda wangu jinsi PT wanavyo bambikia watu kesi mbaya, hawachelewi kubambikia watu uhaini!.
Conclusion
The bottom line ni polisi wetu wana bambika watu kesi mbaya hadi za mauaji!, hivyo hawezi kushindwa kubambika uhaini!.
Hivyo mtu ukihisiwa tuu wewe ni hatari kwa usalama wa the status quo, unabambikiwa kesi, unapotezwa, na sasa hadi uhaini unazungumzwa!.
Kwa vile mimi ni Tomaso, siamini kabisa dhana ya uhaini mpaka tuthibitishiwe!.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali