Uhakika: Jinsi Vita ya Urusi na Ukraine Itakavyokwamisha Upandishaji wa Mishahara ya Wafanyakazi

Uhakika: Jinsi Vita ya Urusi na Ukraine Itakavyokwamisha Upandishaji wa Mishahara ya Wafanyakazi

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Dodoma, Jumapili 17/4/2022
Vita ni shida. Vita ni taabu. Vita ni balaa. Nani angeweza kutabiri kwamba vita kati ya Urusi na Ukraine ingeathiri uchumi na kuvuruga mipango ya maendeleo ya serikali kiasi hiki? Sasa ni dhahiri kuwa vita hii imepelekea mdororo wa uchumi wa taifa.

Uchumi wa taifa unapovurugika, mambo mengi sana huenda kombo. Kati ya mipango mingi itakayovurugika ni uwezo wa serikali kuwaongeza mishahra wafanyakazi. Tukumbuke ahadi ya kuwaongezea mishahara wafanyakazi ilitolewa na Mh Rais Samia Suhulu mnamo tarehe 1/5/2021 wakati akihutubia halaiki ya wafanyakazi. Alisema kuwa atawaongezea pekeji (mishahara) wafanyakazi ifikapo tarehe 1/5/2022. Lakini kwa sababu ya Urusi kuivamia Ukraine na kusababisha vita, ahadi hii haitaweza kutekelezwa. Kiongozi mmoja kutoka serikalini alinukuliwa akisema kuwa serikali ilikuwa na nia thabiti kuwaongeza mishahara wafanyakazi lakini imeshindikana kwa sababu ya uwepo wa vita ya Urusi na Ukraine. “Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kila mfanyakazi anapata mshahara bora lakini mchakato wa kuangalia kama mshahara uongezeke au la utaanza mara baada ya vita ya Urusi na Ukraine kukoma kwa kuwa vita hii imeharibu sana uchumi wetu”. Alisema.

Wataalamu wa masuala ya uchumi wanasema kuwa vita ya Urusi na Ukraine imesababisha kupanda kwa bei ya mafuta na hivyo kusababisha bei ya kila kitu kupanda. Tukumbuke mishahara ya wafanyakazi inatokana na kodi wanazokamuliwa wananchi. Serikali haiwezi kuwaongezea kodi wapigakura kwa kuwa tayari wana hali ngumu ya maisha. Aidha, ikiwa serikali itapandisha mishahara ya wafanyakazi, hali hiii itasababisha mfumuko wa bei na watakaoumia zaidi sio wafanyakazi (kwa kuwa tayari watakuwa na mishahara mikubwa) bali ni wananchi wa kawaida. Vilevile, uchumi wa taifa utadorora zaidi.

“Kwa hiyo, unaweza kuona kwamba kuongeza mishahara sio neema kwa watumishi bali ni balaa kwao na kwa nchi nzima. Serikali haiwezi kukubali kufanya jambo lenye athari kubwa kiasi hiki pasipo kuzingatia madhara yake kwa uchumi wa taifa na uchumi wa mwananchi mmmoja mmoja”. Alisema.

MAONI YANGU
Mimi naona uamuzi wa serikali ni sahihi kwa kuwa nyongeza ya mishahara itawaathiri wapigakura wasiokuwa na hatia kwa maslahi ya kikundi kidogo cha watu wanaojiita wafanyakazi. Hili jambo sio la kukurupuka kama vile panya anavyokurupuka kutoka kwenye kibuyu. Kuna mambo kama matatu hivi yanayopaswa kuangaliwa kwa kina kabla ya kufikiria kuongeza mishahara ya wafanyakazi.

Mosi, tukumbuke CCM inafanya uchaguzi wa ndani mwaka huu na wajumbe watakaoshiriki kupiga kura nao wana hali ngumu za kiuchumi. Endapo serikali itawakakua zaidi watu hawa wanaweza kupata hasira na kuwachagua wafuasi wa sukuma gang, hivyo kumkwamisha Rais wetu katika mipango yake ya maendeleo.

Pili, nyongeza ya mishahara ikichochea mfumuko wa bei na kupelekea wapigakura kuichukia serikali kuna hatari ya wapigarakura kuwapigia kura sukuma gang mwaka 2025 na kumtupa nje Rais wa watu aliyepo madarakani sasa. Fikiria kikundi kidogo cha sukuma gang kilivyoitafuna nchi kwa kipindi kifupi tu cha miaka 6 halafu warejee tena madarakani? Haiwezekani.

Tatu, mdororo wa uchumi utakaosababishwa na kupanda kwa mishahara ya wafanyakazi ni zaidi ya uhujumu uchumi. Kwanini serikali ikubali kikundi kidogo cha watu, tena wasiokuwa na madhara kwenye sanduku la kura, wahuhujumu uchumi wa nchi nzima? Ni mwendawazimu pekee anayeweza kuruhusu hili kutokea.

Nawasilisha.​
 
Sgang walishatepeta na Wala hatuwawazii Tena,tunawza jinsi ya kushuhudia mabadilliko dhidi ya njia mbaya zilizotumiwa na s gan🤔 na matumizi ya njia mpya zenye usawa na haki Kwa makundi yote,iwe Chamani au chaguzi za kitaifa🤔
 
Hizi sababu za kutowaongeza mishahara wafanyakazi zinaweza zisiishie ,
kwani hatujui baada ya vita ya urusi nini kitatokea tena.

Hivyo ni vyema serikali ikawa ongeza tu

Hiyo ni haki yao

Liwalo na liwe

Anyway wafanya kazi hamna cha kufanya nyie ni kama mbwa tu bosi wenu anachowaelekeza mnatekeleza

Poleni sana

Magufuli hakuwaongeza miaka mitano hamkufanya lolote

Hata chief Hangaya hatawaongeza na hamtakuwa na cha kumfanya.
,[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Yupi Kati ya hao mkuu?
IMG-20220417-WA0018.jpg
IMG-20220417-WA0019.jpg
 
Wakati unazungumza hayo mnaendelea kuiba hela zetu na hamuoni kama ni kosa au kuna athari.

Hizo hela mnazoiba zinatosha kuongeza mishahara ya watumishi bila kuleta athari zozote.
 
Mleta hoja ana wivu TU na wafanyakazi! Endelea kuteseka TU kwani mishahara ya wafanyakazi imekwishapangiwa bajeti na bajeti ilishasainiwa hairudishwi kuandaliwa upya!

Kuwananga wafanyakazi na kuwaita kindi dogo lisilo na madhara kwenye sandukua kura ni kuwadharau na kuwadhalilisha Kwa uchache wao! Laiti ungeijua nguvu ya wafanyakazi kwenye sandukua la kura na kura zenyewe usingeandika vile!

Nani kakuambia wafanyakazi wanahongwa nyongeza ya mshahara ili waichague ccm? Nyongeza ni haki Yao kisheria sema mwendakuzimu alivunja na kuvuruga sheria Sana!
 
hapo moyo unakuuma akiwaongezea sijui itakuwaje.ahhhh mnaanza kulia kulia subirini
 
Kwamba watumishi wa umma hawana madhara kwenye sanduku la kura? Mleta mada unaumwa wahi hospitali haraka sana! Ukisikia 2020 hadi marehemu walipiga kura unadhani walifufuka wakaingia vituoni kupiga kura? Au hao wanyonge wako ndo walizipiga?

Mama akitaka kujipitia kiulaini 2025 adili na watumishi wa umma tu, atakuwa kamaliza. Maana mwendazake na ukatili wake wote ila bado walimpitisha, japo kwa kutishiwa. Hao wanyonge wanaomlilia magu hata asipowasikiliza. Uzuri wa nchi hii raia hawana madhara, wanabwekea pembeni tu halafu hawachukui hatua yoyote.

Mtumishi mmoja ana madhara kwenye sanduku kuliko wanyonge 100+
 
Watumishi wa umma ni idadi ndogo sana ya watanzania na hawana madhara yoyote kwenye sanduku la kura mkuu.
 
Dodoma, Jumapili 17/4/2022
Vita ni shida. Vita ni taabu. Vita ni balaa. Nani angeweza kutabiri kwamba vita kati ya Urusi na Ukraine ingeathiri uchumi na kuvuruga mipango ya maendeleo ya serikali kiasi hiki? Sasa ni dhahiri kuwa vita hii imepelekea mdororo wa uchumi wa taifa.

Uchumi wa taifa unapovurugika, mambo mengi sana huenda kombo. Kati ya mipango mingi itakayovurugika ni uwezo wa serikali kuwaongeza mishahra wafanyakazi. Tukumbuke ahadi ya kuwaongezea mishahara wafanyakazi ilitolewa na Mh Rais Samia Suhulu mnamo tarehe 1/5/2021 wakati akihutubia halaiki ya wafanyakazi. Alisema kuwa atawaongezea pekeji (mishahara) wafanyakazi ifikapo tarehe 1/5/2022. Lakini kwa sababu ya Urusi kuivamia Ukraine na kusababisha vita, ahadi hii haitaweza kutekelezwa. Kiongozi mmoja kutoka serikalini alinukuliwa akisema kuwa serikali ilikuwa na nia thabiti kuwaongeza mishahara wafanyakazi lakini imeshindikana kwa sababu ya uwepo wa vita ya Urusi na Ukraine. “Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kila mfanyakazi anapata mshahara bora lakini jambo hili litafanyiwa kazi mara baada ya vita kukoma kwa kuwa uchumi wan chi umevurugika kwa kiasi kikubwa”. Alisema.

Wataalamu wa masula ya uchumi wanasema kuwa vita ya Urusi na Ukraine imesababisha kupanda kwa bei ya mafuta na hivyo kusababisha bei ya kila kitu kupanda. Tukumbuke mishahara ya wafanyakazi inatokana na kodi wanazokamuliwa wananchi. Serikali haiwezi kuwaongezea kodi wapigakura kwa kuwa tayari wana hali ngumu ya maisha. Aidha, ikiwa serikali itapandisha mishshara ya wafanyakazi, hali hiii itasababisha mfumuko wa bei na watakaoumia zaidi sio wafanyakazi (kwa kuwa tayari watakuwa na mishahara mikubwa) bali ni wananchi wa kawaida. Vilevile, uchumi wa taifa utadorora zaidi.

“Kwa hiyo, unaweza kuona kwamba kuongeza mishahara sio neema kwa watumishi bali ni balaa kwao na kwa nchi nzima. Serikali haiwezi kukubali kufanya jambo lenye athari kubwa kiasi hiki pasipo kuzingatia madhara yake kwa uchumi wa taifa na uchumi wa mwananchi mmmoja mmoja”. Alisemma.

MAONI YANGU
Mimi naona uamuzi wa serikali ni sahihi kwa kuwa nyongeza ya mishahara itawaathiri wapigakura wasiokuwa na hatia kwa maslahi ya kikundi kidogo cha watu. Mosi, tukumbuke CCM inafanya uchaguzi wa ndani mwaka huu na wajumbe watakaoshiriki kupiga kura nao wana hali ngumu za kiuchumi. Endapo serikali itawakakua zaidi watu hawa wanaweza kupata hasira na kuwachagua wafuasi wa sukuma gang, hivyo kumkwamisha Rais wetu katika mipango yake ya maendeleo.

Pili, nyongeza ya mishahara ikichochea mfumuko wa bei na kupelekea wapigakura kuichukia serikali kuna hatari ya wapigarakura kuwapigia kura sukuma gang mwaka 2025 na kumtupa nje Rais wa watu aliyepo madarakani sasa. Fikiria kikundi kidogo cha sukuma gang kilivyoitafuna nchi kwa kipindi kifupi tu cha miaka 6 halafu warejee tena madarakani? Haiwezekani.

Tatu, mdororo wa uchumi utakaosababishwa na kupanda kwa mishahara ya wafanyakazi ni zaidi ya uhujumu uchumi. Kwanini serikali ikubali kikundi kidogo cha watu, tena wasiokuwa na madhara kwenye sanduku la kura, wahuhujumu uchumi wa nchi nzima? Ni mwendawazimu pekee anayeweza kuruhusu hili kutokea.

Nawasilisha.​
Tutamkumbuka sana Magufuli. Alizuia viroba. Ona sasa vinaanza kurudi na mtumiaji huyu ameanza kuweweseka
 
Tutamkumbuka sana Magufuli. Alizuia viroba. Ona sasa vinaanza kurudi na mtumiaji huyu ameanza kuweweseka
Mkuu mimi nimetoa uchambuzi yakinifu; kama wewe unaona uchambuzi wangu una uhusiano na viroba, sawa tu mkuu.
 
Fanya kazi uwezavyo atakaeumia Ni mwanainchi wa kawaida,pole watanzania
 
Hata Vita visingeweko bado Serikali haijawa na utashi wa kupandisha mishahara wafanyakazi!
Vita vya Russia na Ukraine vimeleta ahuweni kwa Serikali yetu! Vimeisadia Serikali kukwepa kutatua changamoto za wananchi kwa kisingizio cha Vita.
 
Back
Top Bottom