Uhakika: Jinsi Vita ya Urusi na Ukraine Itakavyokwamisha Upandishaji wa Mishahara ya Wafanyakazi

Uhakika: Jinsi Vita ya Urusi na Ukraine Itakavyokwamisha Upandishaji wa Mishahara ya Wafanyakazi

Tutajiharibia taifa letu, Rushwa, wizi na ufisadi wa mali za umma utaongezeka mno ukizingatia serikali ya sasa haina uwezo wa kukemea maovu haya basi tujiandae kuliangamiza taifa
 
Hizi sababu za kutowaongeza mishahara wafanyakazi zinaweza zisiishie ,
kwani hatujui baada ya vita ya urusi nini kitatokea tena.

Hivyo ni vyema serikali ikawa ongeza tu

Hiyo ni haki yao

Liwalo na liwe

Anyway wafanya kazi hamna cha kufanya nyie ni kama mbwa tu bosi wenu anachowaelekeza mnatekeleza

Poleni sana

Magufuli hakuwaongeza miaka mitano hamkufanya lolote

Hata chief Hangaya hatawaongeza na hamtakuwa na cha kumfanya.
,[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Really?The dogs? Scavengers?
 
MAONI YANGU
Mimi naona uamuzi wa serikali ni sahihi kwa kuwa nyongeza ya mishahara itawaathiri wapigakura wasiokuwa na hatia kwa maslahi ya kikundi kidogo cha watu wanaojiita wafanyakazi. Hili jambo sio la kukurupuka kama vile panya anavyokurupuka kutoka kwenye kibuyu. Kuna mambo kama matatu hivi yanayopaswa kuangaliwa kwa kina kabla ya kufikiria kuongeza mishahara ya wafanyakazi.

Mosi, tukumbuke CCM inafanya uchaguzi wa ndani mwaka huu na wajumbe watakaoshiriki kupiga kura nao wana hali ngumu za kiuchumi. Endapo serikali itawakakua zaidi watu hawa wanaweza kupata hasira na kuwachagua wafuasi wa sukuma gang, hivyo kumkwamisha Rais wetu katika mipango yake ya maendeleo.

Pili, nyongeza ya mishahara ikichochea mfumuko wa bei na kupelekea wapigakura kuichukia serikali kuna hatari ya wapigarakura kuwapigia kura sukuma gang mwaka 2025 na kumtupa nje Rais wa watu aliyepo madarakani sasa. Fikiria kikundi kidogo cha sukuma gang kilivyoitafuna nchi kwa kipindi kifupi tu cha miaka 6 halafu warejee tena madarakani? Haiwezekani.

Tatu, mdororo wa uchumi utakaosababishwa na kupanda kwa mishahara ya wafanyakazi ni zaidi ya uhujumu uchumi. Kwanini serikali ikubali kikundi kidogo cha watu, tena wasiokuwa na madhara kwenye sanduku la kura, wahuhujumu uchumi wa nchi nzima? Ni mwendawazimu pekee anayeweza kuruhusu hili kutokea.

Nawasilisha.​
So watumishi waumie on the expense of wapigakura
 
Asil
Mleta hoja ana wivu TU na wafanyakazi! Endelea kuteseka TU kwani mishahara ya wafanyakazi imekwishapangiwa bajeti na bajeti ilishasainiwa hairudishwi kuandaliwa upya!

Kuwananga wafanyakazi na kuwaita kindi dogo lisilo na madhara kwenye sandukua kura ni kuwadharau na kuwadhalilisha Kwa uchache wao! Laiti ungeijua nguvu ya wafanyakazi kwenye sandukua la kura na kura zenyewe usingeandika vile!

Nani kakuambia wafanyakazi wanahongwa nyongeza ya mshahara ili waichague ccm? Nyongeza ni haki Yao kisheria sema mwendakuzimu alivunja na kuvuruga
Asilimia ngapi
 
Hata Vita visingeweko bado Serikali haijawa na utashi wa kupandisha mishahara wafanyakazi!
Vita vya Russia na Ukraine vimeleta ahuweni kwa Serikali yetu! Vimeisadia Serikali kukwepa kutatua changamoto za wananchi kwa kisingizio cha Vita.
Mkuu vita imesababisha mfumuko wa bei ya mafuta na bei za kila kitu. Serikali ni sikivu, wallah kungekuwa hakuna vita wafanyakazi wote waneongezwa mishahara, niamini mimi.
 
Tutajiharibia taifa letu, Rushwa, wizi na ufisadi wa mali za umma utaongezeka mno ukizingatia serikali ya sasa haina uwezo wa kukemea maovu haya basi tujiandae kuliangamiza taifa
Mkuu usiwe na wasiwasi; mahakama zipo. kama mtu akikutikana amefanya ufisadi kwa makusudi, atapelekwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka na hata kufungwa jela au kunyongwa.
 
Hata Vita visingeweko bado Serikali haijawa na utashi wa kupandisha mishahara wafanyakazi!
Vita vya Russia na Ukraine vimeleta ahuweni kwa Serikali yetu! Vimeisadia Serikali kukwepa kutatua changamoto za wananchi kwa kisingizio cha Vita.
Msisahau bado takribani siku 5 tu serikali itoe msimamo wake huu hapa mnano siku ya Mei Mosi 1/5/2022
 
Dodoma, Jumapili 17/4/2022
Vita ni shida. Vita ni taabu. Vita ni balaa. Nani angeweza kutabiri kwamba vita kati ya Urusi na Ukraine ingeathiri uchumi na kuvuruga mipango ya maendeleo ya serikali kiasi hiki? Sasa ni dhahiri kuwa vita hii imepelekea mdororo wa uchumi wa taifa.

Uchumi wa taifa unapovurugika, mambo mengi sana huenda kombo. Kati ya mipango mingi itakayovurugika ni uwezo wa serikali kuwaongeza mishahra wafanyakazi. Tukumbuke ahadi ya kuwaongezea mishahara wafanyakazi ilitolewa na Mh Rais Samia Suhulu mnamo tarehe 1/5/2021 wakati akihutubia halaiki ya wafanyakazi. Alisema kuwa atawaongezea pekeji (mishahara) wafanyakazi ifikapo tarehe 1/5/2022. Lakini kwa sababu ya Urusi kuivamia Ukraine na kusababisha vita, ahadi hii haitaweza kutekelezwa. Kiongozi mmoja kutoka serikalini alinukuliwa akisema kuwa serikali ilikuwa na nia thabiti kuwaongeza mishahara wafanyakazi lakini imeshindikana kwa sababu ya uwepo wa vita ya Urusi na Ukraine. “Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kila mfanyakazi anapata mshahara bora lakini mchakato wa kuangalia kama mshahara uongezeke au la utaanza mara baada ya vita ya Urusi na Ukraine kukoma kwa kuwa vita hii imeharibu sana uchumi wetu”. Alisema.

Wataalamu wa masuala ya uchumi wanasema kuwa vita ya Urusi na Ukraine imesababisha kupanda kwa bei ya mafuta na hivyo kusababisha bei ya kila kitu kupanda. Tukumbuke mishahara ya wafanyakazi inatokana na kodi wanazokamuliwa wananchi. Serikali haiwezi kuwaongezea kodi wapigakura kwa kuwa tayari wana hali ngumu ya maisha. Aidha, ikiwa serikali itapandisha mishahara ya wafanyakazi, hali hiii itasababisha mfumuko wa bei na watakaoumia zaidi sio wafanyakazi (kwa kuwa tayari watakuwa na mishahara mikubwa) bali ni wananchi wa kawaida. Vilevile, uchumi wa taifa utadorora zaidi.

“Kwa hiyo, unaweza kuona kwamba kuongeza mishahara sio neema kwa watumishi bali ni balaa kwao na kwa nchi nzima. Serikali haiwezi kukubali kufanya jambo lenye athari kubwa kiasi hiki pasipo kuzingatia madhara yake kwa uchumi wa taifa na uchumi wa mwananchi mmmoja mmoja”. Alisema.

MAONI YANGU
Mimi naona uamuzi wa serikali ni sahihi kwa kuwa nyongeza ya mishahara itawaathiri wapigakura wasiokuwa na hatia kwa maslahi ya kikundi kidogo cha watu wanaojiita wafanyakazi. Hili jambo sio la kukurupuka kama vile panya anavyokurupuka kutoka kwenye kibuyu. Kuna mambo kama matatu hivi yanayopaswa kuangaliwa kwa kina kabla ya kufikiria kuongeza mishahara ya wafanyakazi.

Mosi, tukumbuke CCM inafanya uchaguzi wa ndani mwaka huu na wajumbe watakaoshiriki kupiga kura nao wana hali ngumu za kiuchumi. Endapo serikali itawakakua zaidi watu hawa wanaweza kupata hasira na kuwachagua wafuasi wa sukuma gang, hivyo kumkwamisha Rais wetu katika mipango yake ya maendeleo.

Pili, nyongeza ya mishahara ikichochea mfumuko wa bei na kupelekea wapigakura kuichukia serikali kuna hatari ya wapigarakura kuwapigia kura sukuma gang mwaka 2025 na kumtupa nje Rais wa watu aliyepo madarakani sasa. Fikiria kikundi kidogo cha sukuma gang kilivyoitafuna nchi kwa kipindi kifupi tu cha miaka 6 halafu warejee tena madarakani? Haiwezekani.

Tatu, mdororo wa uchumi utakaosababishwa na kupanda kwa mishahara ya wafanyakazi ni zaidi ya uhujumu uchumi. Kwanini serikali ikubali kikundi kidogo cha watu, tena wasiokuwa na madhara kwenye sanduku la kura, wahuhujumu uchumi wa nchi nzima? Ni mwendawazimu pekee anayeweza kuruhusu hili kutokea.

Nawasilisha.​
Mpuuzi wewe eti taarifa umeipata serikalini, umeokoteza taarifa toka puani kwako unaweka humu,
Eti kikundi kidogo cha watu, yaani bila wafanyakazi hata kujua ulichoandika usingejua,

Fikiria ungeenda shule na kufundishwa na mwalimu ambae anatakiwa alipwe mshahara na hakulipwa kama akili zako zinavyofikiri ungepata elimu?
 
Mkuu mimi nimetoa uchambuzi yakinifu; kama wewe unaona uchambuzi wangu una uhusiano na viroba, sawa tu mkuu.
Syo viroba tu na Bangi pia,

Sasa wewe kakutuma nani kufanya uchambuzi juu ya suala la mishahara ya wafanyakazi.

Tumia akli acha bangi
 
Mkuu vita imesababisha mfumuko wa bei ya mafuta na bei za kila kitu. Serikali ni sikivu, wallah kungekuwa hakuna vita wafanyakazi wote waneongezwa mishahara, niamini mimi.
Sasa nani kasema hawaongezewi na iko ktk bajeti ambayo waziri wa fedha wakati wa kuwasilisha plan alisema wameweka kipaombele ktk hilo?
Tena kasema wameweka fungu nono we ni nani wa kusemea serikali?
 
Mpuuzi wewe eti taarifa umeipata serikalini, umeokoteza taarifa toka puani kwako unaweka humu,
Eti kikundi kidogo cha watu, yaani bila wafanyakazi hata kujua ulichoandika usingejua,

Fikiria ungeenda shule na kufundishwa na mwalimu ambae anatakiwa alipwe mshahara na hakulipwa kama akili zako zinavyofikiri ungepata elimu?
Fikiria kwanza kabla ya kuandika mkuu. Huyo mwalimu bila sisi walalahoi kukamuliwa kodi serikali ingepata wapi pesa za kumlipa mshahara? Sasa unapaswa ujue kwamba hali ya uchumi ni mbaya kutokana na vita hivyo serikali haiwezi kuongeza mishahara. Umeelewa?
 
Syo viroba tu na Bangi pia,

Sasa wewe kakutuma nani kufanya uchambuzi juu ya suala la mishahara ya wafanyakazi.

Tumia akli acha bangi
Nimewanukuu vigogo wakubwa waliomo serikalini. Sasa wewe endelea kubana pua ikifika mei mosi ndipo utajua hujui.
 
Sasa nani kasema hawaongezewi na iko ktk bajeti ambayo waziri wa fedha wakati wa kuwasilisha plan alisema wameweka kipaombele ktk hilo?
Tena kasema wameweka fungu nono we ni nani wa kusemea serikali?
Bajeti iliyoongezwa ni kwa ajili ya ujenzi wa reli ya mwnedokasi sio kufanyia mchezo mchafu wa kuwaongezea wafanyakazi mishahara wakati tayari wana maisha mauzri ukilinganisha na wananchi wengine wa kawaida. Kaa ukijua hilo.
 
Ukitaka mshahara mnene, hamia Uingereza.

Ukitaka mshahara mnene, hamia Uingereza.

View attachment 2201478
Hapa Rais Nyerere aliongea ukweli tupu bila chenga wala kutia chumvi. Wafanyakazi wake zao wamejaza miguo kwenye mikabati halafu wanataka wongezewe mshahara? Huo ni ubinafsi mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom