Uhakika Bro
JF-Expert Member
- Mar 29, 2022
- 3,644
- 4,315
‘KURUTI!, UHAKIKA WA VITENDO!’ kwa sauti kali ya kuamrisha mara ya kwanza naisikia ilikuwa ni jeshini. Ilipenya na kueleweka haraka kwa sababu mbili; Mosi, kile nilichokijua tangu mwanzo kuhusu uhakika, nilipenda kulitumia kiingereza ‘sure’. Lakini sababu ya pili ipo wazi ni kuogopa adhabu ambayo ingenipata,…. Hapana, sio ingenipata,… ni ingetupata sote (na mimi nikiwamo) endapo wote ama mmoja wetu asingezingatia amri ipasavyo. Jeshini sio ajabu kumsikia afande akisema, “Babaa…. liMOJA limeharibu kazi, WOTE tunarudia, au WOTE lala chini, biringika!”
Ndugu zangu kama ilivyokuwa kwa kwata, maendeleo pia ni sifa ya ki-kundi. Maendeleo ya jamii yanaathiriwa na kila mwanajamii husika. Mitaa iliyoendelea ambayo mtu wake wa chini naye anayo maendeleo kiasi fulani, ni raha kuishi hapo kwa watu wote. Lakini katika mitaa ambayo mtu wa chini anakuwa; kwanza hana pesa, pia hana hata nafasi (kazi halali) ya kuzitafutia hizo pesa zenyewe. Kuishi katika mitaa hiyo hakuna usalama (kumbuka ‘panya-road’) wala raha, mtu hawezi kujiachia hata kama kibinafsi-binafsi kimaisha yupo vizuri. Kwata haitapendeza ikiwa askari wawiliwatatu tu ndio watakaouishi uhakika wa vitendo halafu wengine wakaharibu kazi. Kiukweli wengi wakitopea katika kuharibu kwata, itafika mahala hao ndio watakaoonekana kuwa sahihi. Halafu wale wanaopatia; ndio wanakosea sasa!
Ni hatari kufikia hali ya nchi kuhama na kuondoka kwenye uhalisia wa kuishi kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria. Watu kadhaa wakiamua kuishi kwa rushwa na magendo haitakuwa mbaya sana kama wengine watabaki katika ‘kwata’ na kufuata utaratibu. Lakini, Mungu na apishe mbali, ikatokea watu walio kinyume na utaratibu wakawa wengi zaidi hadi ikafikia hali ya u-kawaida wa utaratibu wa kutofuata utaratibu; Itakuwa ndiyo imekwisha hiyo maana kupona hapo ni kazi kwelikweli.
Fikiria kwa mfano leo kampuni fulani ya nchi ya pili kiuchumi duniani iamue kuleta bidhaa ya kiwango cha juu Afrika jinsi itakavyopata tabu. Kwanza, tutaichukulia haina ubora kwa tunavyohisi tunaufahamu ‘utaratibu’ wa ubora na bei za bidhaa ‘fekifeki’ za kutoka huko. Endapo ataweka bei inayoendana na ubora halisi wa bidhaa, atakosa wateja na kuambulia kauli kama; “Yaani kwa bei hiyo ninunue kitu cha nchi hiyo, si bora niongeze kiasi fulani ninunue [tena cha mtumba!] cha mzungu/mjapani/mjerumani n.k”. Sijui itapita miaka mingapi wajukuu zetu wawaamini tena? Cha kushangaza! makampuni ya nje, yanayotumia rasilimali, watu na ardhi ya nchi hiyo ya Asia huzalisha na kuuza bidhaa kwa faida kubwa bila shida. Mfano ni pikipiki (zilizokuwa za kiJapan) na simu (za kiMarekani) zinazozalishiwa nchini humo kwa hivi sasa. Taifa zima linapata tabu kuwa la bei rahisi maana wengi walioshinda ni ubora hafifu, taifa zima limekuwa kihafifu-hafifu mazima. Ni huzuni.
Katika nchi za kiafrika kuna suala la uongozi na maslahi ya taifa. Ikiwa tutacheza vibaya tutaangukia katika mtego wa kuwa na kawaida ya rushwa na ubadhirifu mtindo utakaodumaza maendeleo. Lakini ‘kwata’ ya uongozi ikitawaliwa na wazalendo wasafi wenye moyo wa kuongoza kwa ubora wa hali ya juu basi tutafanikiwa wote.
Uhalisia wa mambo ni kwamba: iwe ni katika kuharibu au kutengeneza, mtu mmoja huathiri mafanikio ya jamii nzima;
1. Wakiharibu wote – TUMEHARIBU WOTE,
2. Wakiharibu wachache – TUMEHARIBU WOTE PIA
3. Wakipendezesha wachache – TUMEHARIBU WOTE BADO
Yaani ni hadi pale 4. Watakapopendezesha wote ndio tutakuwa WOTE TUMEPENDEZA!!.
Leo hii mimi ‘m-bongo’ nikifanya biashara na mzungu, kuna uwezekano mkubwa wa kutotimiza mkataba ukilinganisha na wenzetu. Nitapatana na mzungu kumpelekea muhogo, kisha ninapatana na mkulima kulima mihogo. Mwaka wa kwanza tunafanikiwa. Msimu unaofuata usishangae kukuta mkulima alibadilisha gia hewani akalima pilipili ‘zinazolipa’ wakati huo! Nikihitaji mzigo basi nitapigwa kiswahili tu. Tatizo ni je? mzungu nitampigaje kiswahili? (na hakuna msemo wa ‘kupiga kingereza’). Ingekuwa majirani zetu kesi ingefunguliwa (kwa mkulima), angelipwa fidia ya kuvunja mkataba naye angeenda kumlipa huyo mzungu fidia. Mimi mtanzania nikiiga na kufanya hilo lililo la kistaarabu, jamii inanigeukia kunilaumu kuwa nimekosa utu. Kwa wenzetu mnyororo mzima unafahamu endapo mkataba utavunjwa, itafanyika kiutaratibu rasmi utakaoacha pande zote zimeridhika. Ona, sasa mali inatolewa Tanzania kupelekwa nchi jirani ili kuuzwa nje kwa sababu mikataba na tenda bora majirani zetu ndio wanaozishinda. Yaani mali itumie rasilimali, watu na ardhi ya Tanzania lakini isipate ya mikataba (ya kuheshimika). Ikivushwa boda hapo ng’ambo tu ikawalipe pesa za kutosha kutokana na mikataba makini? Si huzuni hii? Jamani uhakika wa vitendo ni muhimu sana ndugu zangu.
Uhakika wa vitendo ndugu zangu, utatupatia uhakika wa kujua kuwa mimi ninapaswa kufanya hiki na ninakifanya, na kile kingine ambacho ni jukumu la yule atakifanya pia. Uhakika wa vitendo ni pale ambapo madereva wanapishana kuilainii katika njia nyembamba kwa sababu tu kila mmoja anatambua kuwa dereva mwenzake atapita kulia kwake! Ni taa/honi ya salaamu BIIII!! Binafsi huwa ninaongezea kimoyomoyo; “Uhakika bro” ninapopita kushoto.
Uhakika wa vitendo utamruhusu mjasiriamali kumwambia mteja kwa uhakika kabisa; “baada ya siku tatu utaupokea mzigo wako” na kweli akaupokea! Hapo amepiga hesabu kuwa ataenda kusaga viungo kiwandani penye uhakika wa huduma! Kijana wa mashineni atanena kwa uhakika; “baada ya masaa matatu, mzigo utakuwa tayari” maana anao uhakika wa nishati/umeme kuwepo na mashine kufanya kazi. Mnyororo mzima unamuhusu hadi yule anayechapisha lebo na anayeuza vifungashio. Mwisho kabisa mtu wa usafirishaji atapita katika barabara ya uhakika na kutumia siku moja tu kufikisha mzigo kwa mteja salama. Sasa katika mnyororo huu mzima wa ‘kwata’ yetu hii asitokee mtu wa kuharibu kazi, ili kweli tutumie siku tatu kumfikia mteja. Uhakika wa vitendo ni muhimu sana.
Uhakika wa vitendo ndugu zangu hautakuja kwa kubadili wala kutunga sheria mpya maana sheria tayari zipo. Bali uhakika wa vitendo utakuja kwa utaratibu wa kufanya kiuhakika kitendo kimojakimoja cha mtu mmoja mmoja nchi nzima. Mtoto anakuwa katika nafasi yake kama mtoto. Mama anasimama kama mama. Baba anahakikisha anakuwa baba kwelikweli. Pia raisi, mwananchi, mwalimu, polisi, trafiki, mzalishaji wa bidhaa, msimamizi wa viwango, mkaguzi wa ubora, mhandisi na mtumiaji wa bidhaa wote waufuate utaratibu wa uhakika wa vitendo.
Siku nikigombea uraisi hii ndiyo itakayokuwa kaulimbiu. Hata bila huo uraisi kaulimbiu binafsi ni muhimu kwa ajili ya UHAKIKA WA VITENDO. Ndiyo, ninatambua mimi siamurishi kila kitu, lakini naamini kuwa kadri watu wengi zaidi wanapofanya juhudi matokeo huonekana. Maana hata Mungu pia hubariki juhudi zetu za dhati. Asanteni sana.

Upvote
0