Uhakiki wa Wanachama Chama Kipya Cha Siasa 1993

Utalalamika sana ila ndo ishatokea babu zako kufutwa kwenye historia. Waasisi walijua udini mlio nao ndo maana historia inaanza na kuishia kwa Nyerere na Karume tu.
 
Utalalamika sana ila ndo ishatokea babu zako kufutwa kwenye historia. Waasisi walijua udini mlio nao ndo maana historia inaanza na kuishia kwa Nyerere na Karume tu.
Mama...
Hapana mimi si mlalamishi wala si mdini.

Ningekuwa hivyo tayari hapa tushagombana.

Mimi hueleza fikra zangu kwa nia ya kuelimishana.

Historia ilifutwa lakini tumeirejesha na haitopotea kamwe.

Hapa JF nimesomesha wengi.
Kwenye group nina wanafunzi wengi sana.

Nimetiwa kwenye miradi mingi ya kuandika historia na vitabu vyangu vimechapwa na vinasomwa.

Nimeshirikishwa katika uandishi wa kitabu cha historia ya Zanzibar (2010).

Nimeshirikishwa pia katika kuandika maisha ya Mwalimu Nyerere (2020).


Mohamed Omari Mkwawa akiwa ameshika kitabu alichosaidia utafiti wake kwa kutoa taarifa ambazo kabla zilikuwa siri kubwa kuhusu kambi ya Kipumbwi iliyotoa Wamakonde walioshiriki katika mapinduzi ya Zanzibar 2010.


Jopo la Prof. Shivji waandishi wa Nyerere Biography wakinihoji kuhusu maisha ya Julius Nyerere 2013
Yaliyokuwa hayafahamiki leo yako hadharani na ni sehemu ya historia ya Tanzania.


Mtangazaji wa TBC1 akinihoji kuhusu kitabu cha maisha ya Mwalimu Julius Nyerere​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…