Uhalali wa cheti kutoka Marriage Conciliation Board ni upi?

Mama pretty

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2020
Posts
2,082
Reaction score
4,103
Wakuu habari,

Inatambulika kuwa inapotokea shida ya kutoelewana kwa wanandoa wawili na kutaka kusuluhisha migogoro yao, hushauriwa kuendea mabaraza ya usuluhishi ya ndoa;

BAKWATA (kwa ndoa iliyofungwa kwa sheria za kiislamu) na Taasisi za kikristo au kanisani ( kwa ndoa iliyofungwa kwa sheria za kikristo)

Sasa je, ni upi uhalali wa cheti kutoka hayo mabaraza ya usuluhushi kwa ajili ya kupeleka mahakamani inapotokea kushindwa kusulihisha mgogoro kwa wanandoa kwa ndoa yenye viashiria ya kuvunjika?

Je, barua kutoka hayo mabaraza inaweza kutambulika kama ushahidi/ cheti kwa mahakama?

Je, ni nani anatakiwa kusaini hivyo vyeti?

Je, ni taratibu zipi za kufuatwa kisheria kwa uhalali wa cheti kutoka mabaraza ya usuluhushi ya ndoa?
 
Serikali ni muamuzi wa mwisho ila taasisi za dini ni mawakala wa serikali na wana tambulika kihalali. Lakini kama wana ndoa hawakuridhika na taasisi za dini wanakwenda kupata suluhishi mahakamani.

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Mabaraza ya usuluhishi yamewekwa kama formalities za ukamilishaji wa suluhu ya ndoa. Baraza lipo chini ya laymans wa sheria za ndoa ambao wao wamewekwa ili wa jaribu kusikiliza na kutafuta suluhu pasipo kuhusisha legal technicalities kwa kutumia ile hekma ya kawaida tuu.

Iwapo wataona kuna viashiria vya ndoa kuweza tengamaa basi watawapeni muda wa kujitafakari ili mpate suluhu,kama wataona hamuwezi kupata suluhu basi huandika ushauri na cheti kama kielelezo cha kwamba wao wameshindwa au wameweza

Umuhimu wa cheti kama hicho ni kwamba kinahalalisha na kupunguza au kutunza muda wa mahakama kufanya mashauri ya ndoa kwa wakati,ni kigezo kwamba kabla hujafika mahakamani kwa kesi ya taraka uwe umepitia barazani.
 
kama unajua kizungu soma hiyo attachment and link vitakusaidia. Kama hujui kizungu pole maana Magufli aliwadanganya kuwaharibu akili na Kiswahili
 
Attachments

Asante kwa ufafanuzi.
 
Asante kwa mchango wako.
Je upi utaratibu wa huo ushauri kufika mahakamani? Sheria ya ndoa ya Tanzania inasemaje kwenye uhalali wa cheti hicho?
 
kama unajua kizungu soma hiyo attachment and link vitakusaidia. Kama hujui kizungu pole maana Magufli aliwadanganya kuwaharibu akili na Kiswahili
Nimesoma hiyo attachment nmeielewa.. swali langu linarudi pale pale, upi uhalali wa cheti kutoka mabaraza ya usuluhushi? Sheria inasemaje?
Nikijibiwa hapa itakua imenisaidia sana..
 
si nimekuwekea link hiyo? au sijakuelewa. Ukisoma hiyo case law na link , the answer to your question is home and dry, I guess!
Hapana hujanielewa.. kwenye link at least imezungumzia MCB na functions zake na imeelezea pia dissolution of marriage by the court ambapo imeorodhesha namna talaka na effects za ku dissolve ndoa inavyokuwa ikiwemo mgawanyo wa mali pamoja na custody and maintenance of children.

Na attached case law imezungumzia parties kupeleka malalamiko yao kuhusu ndoa kwenye ward land tribunal ambapo huko hushulikia masuala ya ardhi na nyumba lakini si usuluhushi wa masuala ya kindoa ambapo imepigwa PO kwa ground hiyo. Yani parties zimeenda kwenye wrong baraza hivyo kushindwa kusuluhisha mgogoro wa kindoa na kuamriwa waanze upya process...

Tafadhali soma tena swali langu ulielewe ndipo unijibu.
 
Back
Top Bottom