Uhalali wa kocha wa Yanga kubeba rangi nyekundu na nyeupe hadharani

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
Wakati wa shamrashamra za kubeba ubingwa, kocha wa Yanga, Nasredine Nabi alionekana akipiga picha huku akishikilia bendera ya nchi yake yenye rangi nyekundu na nyeupe.

Rangi hizo zilikwishapigwa marufuku kuonekana katika hadhira ya Yanga, na msimamo huo umeshatolewa mara kadhaa na uongozi wa Yanga, na kwa mifano michache ni pale uongozi ulipokataa kwa nyakati tofauti nembo za wadhamini wa ligi na klabu ya Yanga, kama vile Vodacom, GSM na NBC ambazo zote zilikuwa na rangi nyekundu na nyeupe inayodhaniwa kuwa inavutia kibiashara katika makampuni mengi.

Uongozi wa Yanga ulikwishaweka wazi msimamo kwamba rangi hizo haziendani na 'utamaduni' wa timu yao. Je, kocha Nabi hakujua hilo au alijua akapuuzia? Je, uongozi wa klabu ya Yanga utamchukulia hatua za kinidhamu iwapo itabainika alifanya makusudi kuvunja utamaduni wa klabu?

Uzi

 
Ni bendera ya nchi yake
 
"Wanaoumia Ni Wengi Kuzidi Coastal Union"


In Mpenja Voice [emoji23]
 
Mbumbumbu katika peak yako mwezini.
 
Kumbuka kuwa hiyo ni bendera ya nchi yake huyo kocha na siyo nembo au rangi tu kwenye nguo au mapambo
 
Hata mjinga akinyamaza uhesabiwa hekima.

Tafuta video za TP Mazembe siku wanachukuwa Ubingwa wa Africa Mbwana Samatta alikuwa amejifunga bendera gani!
 
Hata mjinga akinyamaza uhesabiwa hekima.
Tafuta video za TP Mazembe siku wanachukuwa Ubingwa wa Africa Mbwana Samatta alikuwa amejifunga bendera gani!
Ni kweli, ungenyamaza ningekuhesabu bado upo miongoni mwa wenye hekima
 
Sijazungumzia bendera ya nchi, nimezungumzia utamaduni wa rangi za Yanga. Kwa hiyo anayetaka kuzungumza basi agusie hilo la rangi nyekundu na nyeupe kwenye mkusanyiko wa Yanga
Utateseka sana, bado ubingwa wa FA, jihadhari usije kupata stroke.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜†πŸ˜πŸ˜πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜†πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜„πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…