mhuogomkavu
Senior Member
- Jun 23, 2017
- 116
- 102
Ameandika Professor FRANK JONATHAN PIUS.
Hivi majuzi ulianza mchakato wa uchakuzi mkuu ndani ya CHADEMA kuwachagua viongozi wao wakuu wa kukiongoza chama hicho kwa miaka mingine mitano mbele, mchakato huu umeshuhudiwa ukigubikwa na vitimbi vya kila aina ndani ya chama hicho.
Hivi majuzi nimemsikiliza Prof. Safari aliyekuwa mwenyekiti msaidizi wa chama hicho kwa kipindi cha nyuma akizungumzia masuala kadhaa yaliyohusu mchakato huo wa uchaguzi ndani ya chama hicho.
Kwa ujumla Prof. Safari alizungumzia mambo mengi kama vile kutokuwa na Demokrasia ya kweli ndani ya chama hicho japo mwenyekiti wa chama hicho na wafuasi wake wanahubiri na kujinasibu kuwa chama chao kina demokrasia hali inayopingana na uhalisia uliopo ndani ya chama hicho.
Aidha aliongeza kuwa yapo mengi yanayosemwa na wadau na wachambuzi mbalimbali wa masuala ya siasa na Demokrasia kukikosoa Chama hicho japo uongozi wa juu “unayafumbia macho” mambo hayo huku yakiwa na ukweli ndani yake.
Mambo mengine ni pamoja na maamuzi yanayohusu chama hicho hufanywa na kikudi cha watu wachache “High levels” (sio kamati kuu) na baadaye kuutangazia umma kuwa ni maamuzi ya kamati kuu ili hali miongoni mwa kamati kuu hawajui what going on.
Ukichukua muda wako kumsikiliza na kumtafakari Prof. Safari utagundua kuwa yapo mengi yaliyo na ukakasi ndani ya chama hicho japo wanachana na viongozi wanaonekana kama “all is well” ndani ya chama hicho.
Swali la kujiuliza ni kuwa kwanini wabunge na viongozi wa chama hicho hawasubutu kunyanyua vinywa vyao kuyasema yanayowakwaza.
Anyway sitaki kuwakumbusha kuhusu CHACHA WANGWE wala visa vya ZITTO KABWE kipindi walipotia nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti Taifa katika chama hicho, achilia mbali yaliyomsibu Mzee Sumaye hivi majuzi mpaka kumpelekea kuachana na chama hicho.
Viongozi wengi ndani ya Chama hicho wamemeza ndoano hali inayowasababisha kusema NDIO pale boss wao anaposema ndio na akisema HAPANA basi wooote kwa pamoja wanaitikia HAPANA kwa shangwe na vigelegele wakisaidiwa na vijana wao waliojazana katika mitandao ya kijamii.
Utakuwa unajiuliza hiyo ndoano wameimezaje, ndoano hiyo wengi wao wameimeza kwa “kupewa” nyadhifa fulani fulani ndani ya chama hicho na wengine kupitishwa kwenye majimbo mbalimbali ili wagombee Ubunge (Tonge tamu jamani), ukinyanyua kinywa tu yanakukuta ya Mzee Sumaye na kanda ya Pwani yake.
Ukitaka kuthibitisha hili rejea kauli ya Mbowe hivi majuzi aliposema kuwa anamtaka Lissu awe makamu mwenyekiti wa chama hicho na baadae Lissu kutumiwa fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti na kuijaza kisha kuirejesha, hii maana yake nini?
Hii inamanisha hizo process za ujazaji na urejeshaji wa fomu ni ushahidi tu kuwa hatua zimefuatwa ila kiuhalisia tayari boss kashasema na kashaamua Lissu atakuwa Makamu Mwenyekiti wake utake usitake, very interesting.
Mzee Sumaye alionywa sana kuhusu kugombea nafasi ya kiti cha enzi cha Mzee mwenye chama ila alishupaza shingo na kuamua kujitosa kuwania nafasi hiyo asijue kuwa anajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe (waandaaji wa kitimoto rosti wanaelewa namaanisha nini hapa).
Yaliyomtokea ndio kama mlivyosikia haina haja ya kuyaeleza sana japo bottom of line ni kuwa mzee aliangukia pua katika nafasi ya uenyekiti kanda ya Pwani kwa kupata kura nyingi za HAPANA dhidi ya kura za NDIO, hii ndio inaitwa usijaribu kucheza na kiti cha mfalme.
Wahenga walisema ya ngoswe muachie ngoswe, nami mwandishi wenu namwachia ngoswe aendelee kuongoza Saccoss yake kwa utashi wake.
Ila niwashauri kuwa pale wanapoimba kuhusu Demokrasia wahakikishe wanaanzia kwenye chama chao wawe na uhalali wa kusimama majukwaani na kutokwa na misuli ya shingo kuhubiri kuhusu demokrasia.
Nisiwachoshe kwa leo acha niwatakie majukumu mema tukutane tena kwenye makala nyingine tukijaaliwa uzima.