Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umenena vema, kwa kiasi kikubwa na kubaliana nawe,lakini ktk namba sita siafiki vijana wa form 6 kupewa fursa ya kufundisha,kimsingi sizani kama ualimu unaanza na kuishia kufundisha mambo ya masomo ya darasani tu. Nijuavyo nikwamba ualimu ni zaidi ya chaki na ubao,ingawa pia haitajwi lakini nadhani ufumbuzi wa kuwatumia form 6 ' voda fasta' huko nyuma unamchango ktk matokeo haya mabovu, inasikitisha sana kusikia wanafunzi watahiniwa wanaandika matusi baada ya kushindwa kujibu waliyo ulizwa, kwa mwaka wa pili mfululizo nayasikia madai haya. Hivyo ni wito wangu kuwa pamoja na mambo mengine serikali ni lazima iboreshe mazingira ya kujifunza na kufundishia, na kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu ktk mambo yote ya msingi. Tafadhali taaluma ya ualimu isiingiliwe hovyo haya yote yakizingatiwa yata saidia kurudisha ufaulu mzuri pamoja na kuinua ubora wa elimu nchini.
mkuu nakubaliana na wewe kwa 100% mimi sijapita form 6 nimetoka o'level nikapelekwa ufundi nikasoma mechanicla engineering kweli ilikuwa ni ngumu sana ukizingatia nilichukuliwa kutoka kwenye shule ya academic na sio ya ufundi kama ilivyokuwa kawaida ya shule za FTC. lakini mimi nimetokea huko baada ya kumaliza niliingia shule moja ya private kufundisha mathematics kwa miaka 2.5 kwa kifupi mpaka sasa matunda yakufundisha kwangu o'level yanaonekana kwenye vyuo takribani vyote hapo tanzania. Baada yahapo nikaendelea na elimu ya chuo kikuu. mpaka sasa ni mhandisi inaniuma sana kuona wanafunzi wanafail kiasi kama hiki tukiwa na vijana wengi tu wanasema hawana kazi kwanini tusiwapeleke hao kufundisha hata mwaka mmoja ninauhakika wataleta product nzuri sana kwa taifa. tatizo la walimu wa sekondari nikubwa sana si kwa mishahara tu walimu wengi walioko huko wanafundisha masomo hata ambayo sio yao mimi kuna mwalimu na mfahamu kabisa alishaajiliwa alikuwa nafundisha mathematics lakini kwa sasa nasoma undergraduate chuo fulani aliniomba kumfundisha kwa kweli sikutegemea kusikia mwalimu hajui hata hesabu za milinganyo na BODMAS nilishangaa sana nayeye anasema eti alikuwa mwalimu anafundisha sekondari kabla ya kuja kusoma ni hatari sana. Si laumu sna wanafunzi ila tuanze na wazazi pia hata wale wanaowatrain walimu kunatatizo kubwa na hiki kitu si cha jana kimeingia kiliingia kwenye system kwa wale waliokuwa wanafake veti ndio wengi ni walimu huko primary hata o'level.Niliwahi kutoa angalizo hapo nyuma na nikasema kuwa tunaweza kupunguza matatizo ya walimu ktk shule zetu hasa za kata kwa kuweka alama za kuvuka kwenda kidato kimoja kutoka kingine na pia nikasema tunawataalamu wengi kutoka vyuo vikuu wanamaliza na kuanza kuzurura mitaani kutafuta kazi bila mafanikio sasa hawa serikali ingewaajiri na kuwalipa kulingana na elimu zao ili waende wakarescue situation ya elimu kwani pia kwa macho yangu mwalimu mmoja anafundisha shule fulani ya kata niliwahi kumpa swali la simultaneos eqn na akashindwa hata aanzie wapi kulifanya hapo nikapata picha kuwa hata baadhi ya walimu wetu hawana ubora na sifa.
Naishauri serikali itumie wasomi wake ambao watakuwa tayari kupokea ajira hizi ili tuweze okoa janga hili.
Mimi ni mhandisi na ninafanya shughuli zangu binafsi na huwa tunakutana mara kwa mara na wenzangu na inaonekana wanaunga mkono hoja ya kuanza sasa kushirikisha wasomi kutoka elimu za juu kusaidia kuinua elimu kuanzia shule za sekondari n.k
Hakuna linaloshindikana ndugu zangu watanzania na tuache kulalamika tu kwani huu ni wakati muafaka wa ku solve problem na sio kuiachia serikali pekee kwani sisi wazazi pia ndio chanzo cha kuporomoka kwa elimu hasa kutokana na malezi mabaya tunayowapa watoto wetu na wengi wetu kuwa busy na shughuli zetu na kusahau watoto wetu wanafanya nini.
Tena baadhi ya watu humu wamekuwa wakipoteza muda na kutoleana maneno ya kashfa juu ya dini zao hadi usiku wa manane na kusahau utaifa wao nashindwa kuelewa ni wapi nchi hii inakwenda watu hatuko productive kabisa ila selfishness na chuki zimejaa ktk vifua vyetu...nawasihi ndugu zangu tuamke na tujenge Tanzania iliyobora na tuwaige japo kwa mbali ndugu zetu wachina ambao kwa pamoja waliamka na kuanza kujenga taifa lao ambalo leo hii ni mfano duniani.
Nakerwa na watu ambao wakiamka tu wanaanza kuleta hoja za upuuzi na matusi na dharau na wanashindwa kuelewa ni watu wa rika ngapi wanasoma thread zao na wanajifunza nini..
Tumeachwa mbali sana na Uganda na Kenya kielimu basi hatuna budi kuamka na kuingia front kuisaidia nchi yetu kwani hata ukikaa pembeni utaendelea kuwa mtanzania.
Pia ndugu zetu mnao ishi nchi za nje mjaribu kuacha uzandiki na kutuchafulia amani ya nchi yetu kwani nyie mmekosa pa kwenda ndio maana hamuoni umuhimu wa kurudi kujenga nchi mmekaa tu mkishangaa mabarabara ya juu ya wazungu huku mkishuhudia nchi yenu ikiporomoka kielimu na kimaadili na mnashindwa hata kutuletea uzoefu wenu kutwa kucha mnashinda kwenye thread za udini na siasa.
Namalizia kwa kusema kuwa sisi sote ni wamoja basi tushirikiane ktk kuinua taaluma nchini mwetu ikiwamo pia kumrudia muumba wetu kwani bila yeye hatutaweza kufika popote.
Cha msingi kwanza turudi tulipotoka japo tunasema kurudi nyuma ni mwiko.
Miaka ya tisini kiwango cha chini cha ufaulu ilikua 60% ambapo ilikua ni 90/150 lakini sasahivi hadimarks 70/250 yaani 28% mwanafunzi anaingia sekondari.
Hii inashusha hadhi ya elimu yetu,
Ttunakua na walioenda shule wengi kuliko wasomi.
Sio lazima wote waende sekondari hata kama wameshindwa.
Wajifunze vitu vingine maana kupeleka shule za sekondari wanafunzi wasioweza ni kutumia vibaya rasilimali.
Tusiogope eti majengo tuliyojenga hayatatumika, kama hakuna wanaostahili kuyatumia tuyafanye kuwa madarasa ya elimu za ufundi stadi na stadi zingine za maendeleo.
Tuzalishe wasomi kweli sio tunajitia aibu tu kwa matokeo mabovu matokeo yake tutafika mbali na kuamua ili madarasa yasikae bure,hata mwenye credit 2 ataingia kidato cha 5 mradi tu wawe wengi.
Matokeo ya kidato cha nne yanaanzia chini.
Funguka ndugu yangu! Usiogope Hapa ni Jamiiforums. Jiachie. Tell us the untold stories!
Wengi wameeleza kushtushwa na matokeo ya kidato cha nne. Kwakweli kiwango cha kufeli kimekuwa kikubwa sana. Hata hivyo kwa mtu anayefuatilia hali halis ya mambo nchini mwetu hatashangaa saana. Binafsi sishangai ninacho shangaa ni kwanini hali hii imekuwa haitokei. Kuna viashiria vingi tu kuwa mfumo wetu wa elimu nchini uko mahututi. Kuna matatizo mengi sana yameuzingira mfumo huu ambayo yasipotaftiwa majibu yatasambaratisha elimu kuliko tunavo dhani. Yapo matatizo mengi toka pande nyingi sana. Kuna mchango wa serikali,walimu na wataalamu wa elimu. Mengi yamesha semwa kuonyesha udhaifu wa maeneo hayo. Hata hivo kuna ukweli ambao wachache sana wanauona. Kwamba matokeo mabovu yanachangiwa sana na wanafunzi wenyewe na wazazi wao. Ntaendeleza mada hii........
Wengi wameeleza kushtushwa na matokeo ya kidato cha nne. Kwakweli kiwango cha kufeli kimekuwa kikubwa sana. Hata hivyo kwa mtu anayefuatilia hali halis ya mambo nchini mwetu hatashangaa saana. Binafsi sishangai ninacho shangaa ni kwanini hali hii imekuwa haitokei. Kuna viashiria vingi tu kuwa mfumo wetu wa elimu nchini uko mahututi. Kuna matatizo mengi sana yameuzingira mfumo huu ambayo yasipotaftiwa majibu yatasambaratisha elimu kuliko tunavo dhani. Yapo matatizo mengi toka pande nyingi sana. Kuna mchango wa serikali,walimu na wataalamu wa elimu. Mengi yamesha semwa kuonyesha udhaifu wa maeneo hayo. Hata hivo kuna ukweli ambao wachache sana wanauona. Kwamba matokeo mabovu yanachangiwa sana na wanafunzi wenyewe na wazazi wao. Ntaendeleza mada hii........