Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

Wana JF katika kikao cha bunge kilichopita wabunge walitoa hoja zao za msingi ktk kuletea taifa hili maendeleo. Kiti cha Spika kikatumia ubabe wake. Matokeo ya kidato cha nne yametangazwa, wanafunzi 1600 na ushee tu, ndio waliopata daraja la kwanza, haiwezekani. Kawambwa step down, huwezi chochote, acheni siasa, mitaala haieleweki, vitabu vya kiada na ziada havieleweki, kila shule kivyake, bado ma-godown yamejaa vitabu ya wazabuni hamjalipa, mnatupeleka wapi? Tutafukuzana kama paka na panya, ohoo! grii!!
 
Necta wametangaza matokeo..jamani watu wamefeli sana, hiki kizazi sijui kinaelekea wapi..hali ni tete!

Hongera kwa waliofaulu, waliofeli ni wao kujipanga sana.

Kwa mujibu wa habari hii chini, tunaweza kusema:

Kati ya wanafunzi 397,136 waliofanya mtihani; 240,750 walipata SIFURI!
- Division I - 1,641 => 0.41%
- Division II - 6,453 => 1.62%
- Division III - 15,426 => 3.88%
- Division IV - 103,327 => 26.02%
- Division 0 = [397,136 - (1,641+6,453+15,426+103,327)] -> 270,289 => 68.06%
Duuh tuna kazi kubwa!!.
 
wafunge vyuo wajenge macasino, kumbi za starehe. na inabid chadema ikiingia madarakani 2015 iwarudishe hawa watoto darasani hata kwa bakora inaelekea serikali ya ccm imeshindwa wajibu wake.
 
Wana JF salaam kwenu! nina post post hii kwa masikitiko yangu makubwa sana, ingawa wengi mmeshaliongelea hili! Nimekuwa nikitazama mara tatutau haya matokeo:
dv 1 1,641
dv 2 6,453
dv 3 15,426
dv 4 103,327
dv 0 240,903

Halafu eti bado waziri wa elimu, naibu wake na katibu mkuu wa wizara hii wanategemea mwisho wa mwezi huu wabebe kodi za watanzania kama mishahara, hawaoni aibu? wanasubiri nini kama kuna upuuzi kama huu umetokea? Bado Nape nae bado anao ujasiri wa kusifia serikali dhaifu namna hii iliyoko madarakani hana hata aibu kukaa kuongea mipasho yake ya kuisema chadema wakati watoto 240,903 hawajui hatma ya maisha yao kielimu! NA NDIO MAANA NAAMUA KUIITA WIZARA HII YA SERIKALI YA CHAMA CHA CCM KUWA NI WIZARA YA KUTENGENEZA WAJINGA
 
Wajinga walishatengenezwa zamani sana. Hamjagutuka? Ukitaka fanya research ndogo sana. Chagua member kama 50 wa JF randomly. wape heading yeyote eg: MAISHA YANGU; waambie waandike kwa kiswahili au kiingereza kitu kama page 2 za A4 uone vituko.
 
kp11122012.jpg
 
and they dare blame it on social networks and media as if they are so clean of this education massacre they committed to the kids.some of us we started owning phones from form one,social networking at the same time but how did we use that to our advantage and make it part of our education is where we differ.you blame a teenager for dating?are u serious?
the moment mkiamua kuwa na mtaala wa taifa wa elimu ulio na tija kwa taifa na kuboresha maslahi na mazingira ya kazi ya walimu pamoja na mazingira ya kusomea halafu wakaendelea kufail,then they can come and blame it on the social networks and media.
besides hizo shule za kata mngezifanya Technical Schools tungewaona wa maana zaidi maana techinical schools zetu zote waliamua kuzifanya secondary school matokeo yake wanatuzalishia zero tu kila mwaka zinaongezeka.
 
duh kiukweli matokeo mabaya yanatokana na mambo mengi ila mengi ktk matatizo ya kishule example shule za kata uhaba wa vifaa vya kufundishi. Kama madawati,vitabu,maabara,maktaba,walimu nk.. Japo social networks zinachangia kimtindo.
 
Wanajamii forum napenda kutoa pole sana kwa wale kwa namna moja au nyingine tumeathirika na matokeo ya kidato cha nne. Si tu kiuchumi bali hata kisaikolojia maana elimu ya sasa si bure kama tunavyoambiwa maana tunalipia kuanzia maji, umeme, madawati, walinzi nk.

Nilitaka kuishitaki serikali kwa kuwapotezea vijana wetu muda wakufanya maendeleo na kuwakusanya kwenye shule zisizo na walimu, madawati, vyoo, vitabu na maabara na mwisho wake kuwarudisha mitaani wakiwa na zero.

Lakini nilipokuwa na soma sheria ya elimu nikakutana na kitu hiki "ELIMU SIYO MAHITAJI YA LAZIMA KWA MTANZANIA KIKATIBA" nikaduwaa kabisa na nikaona ndio maana wizara (Dr. Kawambwa, Ndalichako na Mulungo ndio maana wanafurahia matokeo maana hatuna pakuwabana kisheria.

1. Tubadilishe sera ya elimu maana inaonekana kikatiba inakizana na na hali halisi ya upatikanaji wa elimu kwa watanzania.

2. Malalamiko ya wizara: Nijambo la kuchukiza na kuendelea kuuhadaa umma wa watanzania kwa yale yaliyotolewa na Dr. Kawambwa siku anatangaza matokeo na hata kililichokuwa anongea katibu wake Dr. Ndalichako.

Nasema hivyo kwa sababu gani? kutupia lawama kuwa wazazi/walezi tuyalaani kila njia maana hayana ukweli wowote kama serikali ndio inatoa vibali vya bar, guest, kumbi za burudani, internet cafe. Kwa nini isiweze kuwazuia wamiliki kuruhusu vijana wetu wasiingie kwenye sehemu hizo kupitia viongozi wake kama mabalozi, wenyeviti na hata watendaji? Chukulia mzazi/mlezi mwanafunzi anaondoka asubuhi kwenda shule inakuwa ni ngumu sana kuthibiti mwananfunzi ambaye ana akili timamu bila kujali umri wake. Si hivyo tu hata sisi wananchi nivingumu kujua huyu ni mwanafunzi au ni muuza bar/guest maana siku hizi wanavaa uniform sawa na nawanafunzi. Ninaona ni muda mwafaka kuweka wanafunzi wetu wawe na uniform moja tu na ikibadilika labda kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine na si ndani ya mkoa zinachanganya sana hizi uniform.

3. Mitaala ya elimu ninaona ibadilishe turudi tulikokuwa mwanzo. Tuliosoma shule za msingi 1980s' na 1995s' mtakubaliana na mimi elimu ya msingi ilikuwa bora sana tukiwa na walimu wengi tu wa UPE lakini leo hii walimu waupe ni wachache sana na form 4 ni wengi na kufail ndio kumeongezeka ile mbaya.Chukulieni mfano wa kitabu cha hisabati cha darasa la 6 (rangi Jano) na 7 (rangi kijani) kilichotumika kuanzia 1989 sijui kilifutwa lini. lakini kama ukichukua kitabu cha hisabati cha darasa la sita cha miaka hiyo chenye rangi ya jano ukaangalia na mathematics book 1 kinachotumia form one leo utaona vinatofautiana topic mmoja tu decimal repeating/Recurring. Swali kwa nini hiki kitabu kilifutwa? Ushauri wangu naona kirudishwe maana ilikuwa ni sehemu nzuri yakumfanya mwanafunzi awe anasumbuka na lugha tu (kiswahili kwenda Kiingereza).

Lakini tusishahu kuwa mitaala ya zamani ilikuwa na inataka mwanafunzi wa darasa la I & II ajue "KUSOMA, KUANDIKA NA KUHESABU" ulikuwa ni msingi mzuri sana unaotosha kwa umri wamtoto lakini leo hii mtoto wa miaka 6 hadi 7 anamasomo 7 na vitabu vingi kama nini hapo unategemea mtoto anajua kile kilichoandikwa humo ndani? Nafikiria msingi mkuu wa sekondari unaanzia Primary mtoto aliyetoka na msingi mzuri primary ni marachache sana kwenda kuyumba secondary na akiyumba kunakuwepo na sababu lakini kama hana foundation nzuri kutoka primary ni wachache sana wanaoweza kwenda kufanya vizuri secondary.Na hii inahitaji bidii sana kwa mwanafunzi wa aina hii kuliko aliye na msingi mzuri wa primary.

Tution naomba zipingwe marufuku zinakalilisha watoto tu sisi hatujasoma tution tunaelimu nzuri kuliko hata wale wanaoshinda kwenye tution kuanzia darasa la awali hadi sekondari kweli ni aibu kubwa sana watoto hawapumziki tunawakalilisha kila kitu hawana hata muda wa kupumzika si likizo wanatakiwa tution sijajua maana ya mapumziko nini.

utitiri wa vitabu kama vile vya kina Nyangwine vifutwe haraka iwezekana navyo si tu vinawapotosha vijana balia vinawafanya kukalili na kupoteza misingi ya elimu nzuri maana wao ndio wanakula rushwa na serikali na kuweza kuviingiza kwenye soko eleweni vijana wetu wengi wasiku hizi ni wavivu kusoma kwa hiyo wanapoona vitabu kama hivi wanafurahia kumbe ndio wanajiua.

4. Swala la maadili naomba turudi nyuma pasipo kufuata mila na desturi zetu za awali na kuatamia mila za umagharibi hakika hatufiki wenzetu wameachana na fimbo kutokana na uelewa wa watoto wao kuwa mpana zaidi. Leo hii sisi tunakataza viboko haswa kwa shule za misingi na ndani ya familia zetu tukitegemea watoto watakuwa na maadili mema? kama sikosei mwezi November kuna gazeti mmoja lilichapisha wanafunzi walikuwa wanwatongoza walimu wa kike wa shule moja ya msingi pwani walipokataa waliamua kuwapiga walimu wakishirikiana na wazazi. Je, kweli unaona huyo mwalimu atakuwa na moyo wa kufundisha mtoto wa aina kama hiyo?

5. Ubabe wa serikali kuhusu madai ya wanafunzi ya shughulikiwe haraka sana iwezekanavyo ili walimu wawape moyo wakufundisha na sikuwakejeli na kuwadharau.

6. Kuhusu swala la uhaba wa walimu ninashuari kwa kuwa hatunanamna ya kuzalisha walimu ili kukidhi mahitaji ya sasa basi naomba serikali ilazimeshe wanafunzi wote wanaomaliza form 6 kabla hawajaenda vyuoni lazina wafundishe kwenye shule za sekondari kwa mwaka mmoja ndio waingie vyuoni kama ilivyokuwa huko nyuma kwenye jeshi. na wanafunzi watakapozidi wakuingia form six ifanyike vile wale wanaomaliza vyuoni lazima wakafundishe mwaka mmoja kabla ya kwenda fani husika. Ninaimani tunaweza kusukuma jahazi kwa sehemu fulani.

ni mtazamo wangu tu kwa sasa .
 
tusisubiri serikali iliyokosa mwelekeo itakuja na majibu kwetu nje ya kuishinikiza watoto wetu ndio wana adhirika na si hivyo tu hawa zee enzi zao ndio zinapita ujingwa wawatoto wetu leo ndio utakuwa janga kwa taifa la kesho
 
ccm hawana soni maana watoto wao hawasomi hata kwenye shule hizi maana wanapokuja na swala na vitabu, walimu, maabara si kweli shule kama Mwanza sec. Morogoro sec, Pungu, Makongo zina maabara nzuri tu kwa hiyo tatizo sio kama Dr. Kawambwa alivyosema
 
Hali ya Maisha ya Walimu nchini hasa vijijini inatisha. Imefikia mpaka walimu wengine kua Shoe shiners, Machangudoa, na Makuli. Jamii yenyewe inawadharau Walimu kutokana na kuonekana ni vinara wa kukopa katika Maduka.

Hata watoto walioko Mashuleni, ukiwauliza, Ukiwa mkubwa ungependa uwe nani? Majibu utakayo ya pata ni kama ifuatavyo:- Benki, Mbunge, Waziri, Daktari, TRA, Bandarini, Ikulu, Fisadi, etc.

Hautasikia hata mwanafunzi Mmoja akisema Mwalimu. Nakama utawauliza kwani hamtaji Ualimu, Wote wata anguka kicheko.

Sasa tuache unafiki. Sisi tule kuku, wenzetu wauze Ubuyu tena kwa kuwakopesha wanafunzi halafu mtarajie Maajabu.

Kimsingi walimu wamepoteza Moral ya kufundisha. Wameshafanya shule kama vijiwe tu.
 
Nadhani tatizo ni zaidi ya morale ya walimu

-idadi ya walimu ni ndogo ukilinganisha na shule ziliopo

-ubora/competence ya walimu mashaka

-ukosefu wa vitendea kazi

- english competence ya walimu na wanafunzi ni ndogo.

- uhaba wa revision aids, mfano past papers(indeed ni busara baraza liweke past papers kwenye website yao available free of charge)
 
Umenena vema, kwa kiasi kikubwa na kubaliana nawe,lakini ktk namba sita siafiki vijana wa form 6 kupewa fursa ya kufundisha,kimsingi sizani kama ualimu unaanza na kuishia kufundisha mambo ya masomo ya darasani tu. Nijuavyo nikwamba ualimu ni zaidi ya chaki na ubao,ingawa pia haitajwi lakini nadhani ufumbuzi wa kuwatumia form 6 ' voda fasta' huko nyuma unamchango ktk matokeo haya mabovu, inasikitisha sana kusikia wanafunzi watahiniwa wanaandika matusi baada ya kushindwa kujibu waliyo ulizwa, kwa mwaka wa pili mfululizo nayasikia madai haya. Hivyo ni wito wangu kuwa pamoja na mambo mengine serikali ni lazima iboreshe mazingira ya kujifunza na kufundishia, na kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu ktk mambo yote ya msingi. Tafadhali taaluma ya ualimu isiingiliwe hovyo haya yote yakizingatiwa yata saidia kurudisha ufaulu mzuri pamoja na kuinua ubora wa elimu nchini.
 
Back
Top Bottom