Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

Mungai alibaka elimu yetu kwa kutuhamisha kwenye misingi yetu ya awali nakuleta ufamili, undugu, na urafiki kwenye swala la elimu
 

mkuu kwenye red nimetoa wazo kama hilo kutokana hatuna jinsi kwa sasa shule ni nyingi sana hatuwezi kuzalisha walimu wakuweza kutosheleza mahitaji tufanye miaka 4 huku vyuo vyenye kozi ya ualimu wakiendelea kuhitimu
 
kwa shule zetu za kata tunaweza kuweka mazingira ya walimu kuyapenda mazingira kwa kuwanunulia sola. Mfano sola hapa china inayoweza kuendesha TV, fan, na tube light 8 hadi 12 haizidi 1.5million sasa kwa nini tusianze kutengeneza mazingira hata kwa kuwakopesha walimu ili waishi maisha safi hata huko kijijini?
 
Niliwahi kutoa angalizo hapo nyuma na nikasema kuwa tunaweza kupunguza matatizo ya walimu ktk shule zetu hasa za kata kwa kuweka alama za kuvuka kwenda kidato kimoja kutoka kingine na pia nikasema tunawataalamu wengi kutoka vyuo vikuu wanamaliza na kuanza kuzurura mitaani kutafuta kazi bila mafanikio sasa hawa serikali ingewaajiri na kuwalipa kulingana na elimu zao ili waende wakarescue situation ya elimu kwani pia kwa macho yangu mwalimu mmoja anafundisha shule fulani ya kata niliwahi kumpa swali la simultaneos eqn na akashindwa hata aanzie wapi kulifanya hapo nikapata picha kuwa hata baadhi ya walimu wetu hawana ubora na sifa.
Naishauri serikali itumie wasomi wake ambao watakuwa tayari kupokea ajira hizi ili tuweze okoa janga hili.
Mimi ni mhandisi na ninafanya shughuli zangu binafsi na huwa tunakutana mara kwa mara na wenzangu na inaonekana wanaunga mkono hoja ya kuanza sasa kushirikisha wasomi kutoka elimu za juu kusaidia kuinua elimu kuanzia shule za sekondari n.k
Hakuna linaloshindikana ndugu zangu watanzania na tuache kulalamika tu kwani huu ni wakati muafaka wa ku solve problem na sio kuiachia serikali pekee kwani sisi wazazi pia ndio chanzo cha kuporomoka kwa elimu hasa kutokana na malezi mabaya tunayowapa watoto wetu na wengi wetu kuwa busy na shughuli zetu na kusahau watoto wetu wanafanya nini.
Tena baadhi ya watu humu wamekuwa wakipoteza muda na kutoleana maneno ya kashfa juu ya dini zao hadi usiku wa manane na kusahau utaifa wao nashindwa kuelewa ni wapi nchi hii inakwenda watu hatuko productive kabisa ila selfishness na chuki zimejaa ktk vifua vyetu...nawasihi ndugu zangu tuamke na tujenge Tanzania iliyobora na tuwaige japo kwa mbali ndugu zetu wachina ambao kwa pamoja waliamka na kuanza kujenga taifa lao ambalo leo hii ni mfano duniani.
Nakerwa na watu ambao wakiamka tu wanaanza kuleta hoja za upuuzi na matusi na dharau na wanashindwa kuelewa ni watu wa rika ngapi wanasoma thread zao na wanajifunza nini..
Tumeachwa mbali sana na Uganda na Kenya kielimu basi hatuna budi kuamka na kuingia front kuisaidia nchi yetu kwani hata ukikaa pembeni utaendelea kuwa mtanzania.
Pia ndugu zetu mnao ishi nchi za nje mjaribu kuacha uzandiki na kutuchafulia amani ya nchi yetu kwani nyie mmekosa pa kwenda ndio maana hamuoni umuhimu wa kurudi kujenga nchi mmekaa tu mkishangaa mabarabara ya juu ya wazungu huku mkishuhudia nchi yenu ikiporomoka kielimu na kimaadili na mnashindwa hata kutuletea uzoefu wenu kutwa kucha mnashinda kwenye thread za udini na siasa.
Namalizia kwa kusema kuwa sisi sote ni wamoja basi tushirikiane ktk kuinua taaluma nchini mwetu ikiwamo pia kumrudia muumba wetu kwani bila yeye hatutaweza kufika popote.
 
Cha msingi kwanza turudi tulipotoka japo tunasema kurudi nyuma ni mwiko.
Miaka ya tisini kiwango cha chini cha ufaulu ilikua 60% ambapo ilikua ni 90/150 lakini sasahivi hadimarks 70/250 yaani 28% mwanafunzi anaingia sekondari.
Hii inashusha hadhi ya elimu yetu,
Ttunakua na walioenda shule wengi kuliko wasomi.
Sio lazima wote waende sekondari hata kama wameshindwa.
Wajifunze vitu vingine maana kupeleka shule za sekondari wanafunzi wasioweza ni kutumia vibaya rasilimali.

Tusiogope eti majengo tuliyojenga hayatatumika, kama hakuna wanaostahili kuyatumia tuyafanye kuwa madarasa ya elimu za ufundi stadi na stadi zingine za maendeleo.

Tuzalishe wasomi kweli sio tunajitia aibu tu kwa matokeo mabovu matokeo yake tutafika mbali na kuamua ili madarasa yasikae bure,hata mwenye credit 2 ataingia kidato cha 5 mradi tu wawe wengi.

Matokeo ya kidato cha nne yanaanzia chini.
 
Hii ishu ya waalimu iko serious sana na kama serikali haitaretreat basi ijiandae kuona waalimu wanaharibu zaidi ya hapa
 
Huko sahihi sana mkuu na kama serikali haitaretreat mapema basi ijiandae kuona waalimu wanaharibu zaidi ya hapa
 
mkuu nakubaliana na wewe kwa 100% mimi sijapita form 6 nimetoka o'level nikapelekwa ufundi nikasoma mechanicla engineering kweli ilikuwa ni ngumu sana ukizingatia nilichukuliwa kutoka kwenye shule ya academic na sio ya ufundi kama ilivyokuwa kawaida ya shule za FTC. lakini mimi nimetokea huko baada ya kumaliza niliingia shule moja ya private kufundisha mathematics kwa miaka 2.5 kwa kifupi mpaka sasa matunda yakufundisha kwangu o'level yanaonekana kwenye vyuo takribani vyote hapo tanzania. Baada yahapo nikaendelea na elimu ya chuo kikuu. mpaka sasa ni mhandisi inaniuma sana kuona wanafunzi wanafail kiasi kama hiki tukiwa na vijana wengi tu wanasema hawana kazi kwanini tusiwapeleke hao kufundisha hata mwaka mmoja ninauhakika wataleta product nzuri sana kwa taifa. tatizo la walimu wa sekondari nikubwa sana si kwa mishahara tu walimu wengi walioko huko wanafundisha masomo hata ambayo sio yao mimi kuna mwalimu na mfahamu kabisa alishaajiliwa alikuwa nafundisha mathematics lakini kwa sasa nasoma undergraduate chuo fulani aliniomba kumfundisha kwa kweli sikutegemea kusikia mwalimu hajui hata hesabu za milinganyo na BODMAS nilishangaa sana nayeye anasema eti alikuwa mwalimu anafundisha sekondari kabla ya kuja kusoma ni hatari sana. Si laumu sna wanafunzi ila tuanze na wazazi pia hata wale wanaowatrain walimu kunatatizo kubwa na hiki kitu si cha jana kimeingia kiliingia kwenye system kwa wale waliokuwa wanafake veti ndio wengi ni walimu huko primary hata o'level.
 

uko sahihi si lazima wote waende sekondari nibora wakaenda wachache lakini wanaomudu masomo na sikupeleka tu hata wasiojua chukulia mwaka huu nilipokuwa nafuatailia matokea nikasikiwa naibu waziri akisema wanafunzi wa wastani wa 30% yaani 15/50 ya kila somo wamechanguliwa kwenda sekondari kweli nilihuzunika sana. miaka yetu hata wastani wa 60% ilikuwa ni ngumu sana kwenda sekondari na wengi walikuwa wanachukuliwa wa sichana lakini kwa mvulani ilikuwa haiwezekani.
 
Shule za Sec kuwa chini ya TAMISEMI ndio chanzo cha watoto kufeli. Nashauri turudi wizara ya Elimu kama zamani. Na wakulaumiwa ni Tamisemi na sio Wizara ya Elimu.
 
Wengi wameeleza kushtushwa na matokeo ya kidato cha nne. Kwakweli kiwango cha kufeli kimekuwa kikubwa sana. Hata hivyo kwa mtu anayefuatilia hali halis ya mambo nchini mwetu hatashangaa saana. Binafsi sishangai ninacho shangaa ni kwanini hali hii imekuwa haitokei. Kuna viashiria vingi tu kuwa mfumo wetu wa elimu nchini uko mahututi. Kuna matatizo mengi sana yameuzingira mfumo huu ambayo yasipotaftiwa majibu yatasambaratisha elimu kuliko tunavo dhani. Yapo matatizo mengi toka pande nyingi sana. Kuna mchango wa serikali,walimu na wataalamu wa elimu. Mengi yamesha semwa kuonyesha udhaifu wa maeneo hayo. Hata hivo kuna ukweli ambao wachache sana wanauona. Kwamba matokeo mabovu yanachangiwa sana na wanafunzi wenyewe na wazazi wao. Ntaendeleza mada hii........
 

Na mimi nawashangaa sana wanaosema waziri Kawambwa ajiuzuru, kwa kosa gani alilofanya?
Kutekeleza ilani ya CCM? Iliyoanzisha shule za kata?
Siwaelewi kabisa watu hao, waliona kabisa kupitia vyombo vya habari ambapo shule ya watoto mia nne na ushee ina walimu wawili. Watu wenye akili walipopiga kelele wenye serikali yao wakasema hizo ni changamoto za maendeleo. Tumeona sasa kuwa hizo walizoita changamoto kumbe ni janga la kitaifa.
Taifa linatengeneza watu wajinga, ambao hawawezi kushindana sawasawa katika ulimwengu huu wa Technolojia.
Nilitarajia watu waseme Rais Kikwete imetosha sasa kufanya majaribio ya kutawala, mpishe mtanzania mwingine, umeshindwa kazi. Pumzika baba, umechoka!
 
hata versity si lazima wote waende,haya ya wote wapate yanaiua nchi.. hivi kwann nyumba ya mwalimu kijijn haipewi solar?
 
#umeckia hii...Matokeo
kidato cha nne ‘feki’
Mkurugenzi GREEN
ACRES AFICHUA SIRI
NZITO
Alitaja mfano wa
mwanafunzi,Humphrey
Sanga mwenye namba
01197/148, ambaye
hakufanya mitihani hiyo
lakini matokeo
yanaonesha amefaulu
kwa kupata alama nzuri.
“Huyu mwanafunzi
tulimsimamisha na
hakufanya mitihani,lakini
matokeo yake
yanaonekana amepata
hivi;Civics D,Historia
D,Jiografia C,Kiswahili
D,English C,Physics D,
Chemistry C,Biology
C,Basic Mathematics
D,ambapo
amepata daraja la tatu
pointi 24,” alisema
Bujugo.
Alimtaja mwanafunzi
mwingine,Martin
Rushaigwa,namba
01197/0173 ambaye
alifanya masomo ya
‘Arts’.
Alisema matokeo ya
mwanafunzi huyo
yanaonesha kuwa
ameongezewa alama za
masomo ya biashara ya
Bookeeping na
Commerce ambayo
hakuyafanya
kabisa.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu uliyoandika ni kweli tupu. Hata mimi nina mawazo kama yako. Huhitaji vifaa maalum kujua elimu ya Tanzania imegeuka janga. Pitia mtiririko ya posts zinazoandikwa na wana JF (usithubutu kupima quality kwani utazirai) uone watu wa chuo kikuu wasivyojua kuandika na kujieleza kwa kiswahili. Watu walisomea mtihani na hawakuelimika.
 
Wadau hawa watoto wote wamefeli mbona ni kama form five hali itakuwa mbaya zaidi, madarasa yatakuwa wazi, na kwa wale vilaza ndio itakuwa tabu mara tatu..nyie mnasemaje?
 
Labda itasaidia madarasa kutokuwa na wanafunzi wengi kupita kiasi. Kwa hali hii walimu hawatakuwa na kazi ngumu kufundisha.
 
2012 Form 4 results

DIV 1: 1,641 (0.4%)
DIV 2: 6,453 (1.6%)
DIV 3: 15,426 (3.9%)
DIV 4: 103,327 (26.0%)
DIV 0: 240,903 (60.1%)

2011 Form 4 results

DIV 1: 3,671 (1.09%)
DIV 2: 8,112 (2.41%)
DIV 3: 21,794 (6.84%)
DIV 4: 146,639 (43.60%)
DIV 0: 156,085 (46.41%)

2010 Form 4 results

DIV 1: 5,363 (1.53%)
DIV 2: 9,944 (2.83%)
DIV 3: 25,107 (7.14%)
DIV 4: 136,777 (38.9%)
DIV 0: 174,407 (49.60%)

2009 Form 4 results

DIV 1: 4,419 (1.78%)
DIV 2: 10,493 (4.21%)
DIV 3: 27,310 (11.2%)
DIV 4: 130,651 (52.61%)
DIV 0: 65,708 (26.46%)





Je, wakulaumiwa ni nani?




Watu wangu wanaangamia kwa kukosa Maarifa.






 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…