Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

Sasa hivi wamekuja na mpya. Wanalazimisha watoto wote wa darasa la saba mwaka huu wenye uwezo mdogo kurudia darasa la sita. Maafisaelimu wilaya wanawakoromea walimu wakuu kuwakaririsha watoto. Kwa ufupi hali ni mbaya kwani watoto wanakataa wenzao wanawazomea, wao wenyewe hawakujiandaa kisaikologia. My take: hivi sheria ya kutokaririsha watoto ilitenguliwa lini? Je kwa watoto kurudia itawabadilisha kwa muda wa mwaka mmoja bila serikali kuangalia changamoto gani zinasababisha?
 
haitasaidia mkuu hii mimi naona kunauwezekano watoto wengi wanaenda sekondari wengi wao walofail mitihani na hii inafanyika ili serikali ionekane iansomesha kumbe ndio inaongeza wajinga ndani ya nchi yetu
 
huku nikupotezeana maisha ni afadhari hawa watoto wangewaacha wakazalisha ndani ya miaka 4 waliofilsi familia na hata taifa kwa kukaa miaka 4 for nothing
 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa na QT.

Jumla ya watahiniwa waliofaulu kwa Mujibu wa Matokeo hayo ni 23520 kuanzia daraja la I hadi la IV huku katika mchakato huo wasichana waliofaulu katika mchakato huo ni 7178 na wavulana ni 16342.Aidha Waziri Kawambwa amesema kuwa waliofaulu kwa daraja la kwanza ni 1641, daraja la pili ni 6495 na daraja la tatu ni 15426 na walio feli ni 24903.

Shule bora ni pamoja na St. Francis Girl ya Mbeya, Marian Boys ya Bagamoyo, Feza Boys Dar es Salaam, Marian Girls Bagamoyo na Simini,hizo ndizo zilizopo kwenye tano bora huku shule nyingine ni Kanosa, Jude, St. Mary.
Source ni michuzi

Rekebisha hapo kwenye red isomeke Rosmini SS- Tanga
 
bwana elimu ya bongo sio hao walio fail waende wakachukue certificate, diploma then jiwe si ndo shortcut siku hizi. Pale TIA kusoma certificate mtu awe na D moja tu anaanza cheti. Unadhan degree kujazana mjini zinatoka wapi? Tena hao walio fail ndo uwa wanakunjuka na GPA za 3.8 na kuendelea kwaiyo wasiuzunike sana.

D moja unadanganya mkuu, then mwanafunzi aliyesoma shule ya kata ataziweza hizo gharama kweli? Au umeongea tu kujifurahisha?
 
Wadau matokea ya kidato cha nne kwa mwaka 2012 yametoka tembeleeni website ya 'NECTA' nimejaribu saana naona web ipo bzy ila matokea ya jitegemee ni mabovu sana....
Maana...
Div 1 - 1
Div 2 - 2
Div 3 - 26
Div 4 - 210
Failed - 443
 
Jumla div 1,2,3,4 na zero ngapi?mwenye link atuwekee hapa hizi data
 
Matokeo ya Form Four hayana majina bali ni namba za watahiniwa tu! Issue ya matokeo ya kitaifa kuifanya kuwa ya kifamilia sio fresh!
 
huku nikupotezeana maisha ni afadhari hawa watoto wangewaacha wakazalisha ndani ya miaka 4 waliofilsi familia na hata taifa kwa kukaa miaka 4 for nothing

Mungu alinusuru taifa letu na vijana wetu waliopo mashuleni.
 
nusu ya watahiniwa wamepata division sifuri, kama serikali haioni mambo haya itajuta kwa vijana kuiondoa madarakani kwa mawe na marungu
 
Heri yetu tuliosomea chini ya miembe miaka ilee
 
Kwenye uongo ukweli ujitenga hatimae mzizi wa fitina umekatwa,wapo wapi waliokuwa wanawakejeli walimu. Watanzania tunaendelea kunyanyaswa kielimu wakati watoto wa wakubwa wanasoma shule bora kisha wanakuja kututawala . Kazi ipo
 
ha ha ha yaani hata mimi nilikuwa nawaza kitu kama hicho ila sijathibitisha kama ni kweli ndio maana wameamua kubadilisha kuwa na namba tu, hilo nalo linawezekana ila wanafanya sio vyema maana sasa wadogo zetu watakuwa wanatudanganya matoeko maana sasa lazima umuulize namba yako ngapi ilingali zamani tulikuwa tunaangalia majina tunajua, ni ujing mtupu kuendesha kazi kifamilia zaidi kama hilo kweli limehusika
 
hapa walioshindwa kupata alama za juu, walie na serikali yao na wajitahidi sana katika harakati za kujikomboa! nchi yetu ipo kwenye harakati za ukombozi..
 
Tusibaki kuilaumu serikali na kuwatupia lawama Waalimu, tutizame hata vijana wetu. Wanatumia muda mwingi kwenye mitandao, kuvaa milegezo na kulala kwenye madisco, ngoja waje mtaani wayaone maisha yalivyo! Sorry kwa kusema ukweli.
 
Back
Top Bottom