haitasaidia mkuu hii mimi naona kunauwezekano watoto wengi wanaenda sekondari wengi wao walofail mitihani na hii inafanyika ili serikali ionekane iansomesha kumbe ndio inaongeza wajinga ndani ya nchi yetuSasa hivi wamekuja na mpya. Wanalazimisha watoto wote wa darasa la saba mwaka huu wenye uwezo mdogo kurudia darasa la sita. Maafisaelimu wilaya wanawakoromea walimu wakuu kuwakaririsha watoto. Kwa ufupi hali ni mbaya kwani watoto wanakataa wenzao wanawazomea, wao wenyewe hawakujiandaa kisaikologia. My take: hivi sheria ya kutokaririsha watoto ilitenguliwa lini? Je kwa watoto kurudia itawabadilisha kwa muda wa mwaka mmoja bila serikali kuangalia changamoto gani zinasababisha?
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa na QT.
Jumla ya watahiniwa waliofaulu kwa Mujibu wa Matokeo hayo ni 23520 kuanzia daraja la I hadi la IV huku katika mchakato huo wasichana waliofaulu katika mchakato huo ni 7178 na wavulana ni 16342.Aidha Waziri Kawambwa amesema kuwa waliofaulu kwa daraja la kwanza ni 1641, daraja la pili ni 6495 na daraja la tatu ni 15426 na walio feli ni 24903.
Shule bora ni pamoja na St. Francis Girl ya Mbeya, Marian Boys ya Bagamoyo, Feza Boys Dar es Salaam, Marian Girls Bagamoyo na Simini,hizo ndizo zilizopo kwenye tano bora huku shule nyingine ni Kanosa, Jude, St. Mary.
Source ni michuzi
bwana elimu ya bongo sio hao walio fail waende wakachukue certificate, diploma then jiwe si ndo shortcut siku hizi. Pale TIA kusoma certificate mtu awe na D moja tu anaanza cheti. Unadhan degree kujazana mjini zinatoka wapi? Tena hao walio fail ndo uwa wanakunjuka na GPA za 3.8 na kuendelea kwaiyo wasiuzunike sana.