Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

mada nyingine bwana sasa labda nikuulize hivi wawezaje kujua kwamba karatasi ninayotia mkasi si ya mwanangu, mtu wangu wa karibu etc??

na je kwenye panel nzima muwe kazi ni kutia mkasi na inapohakikiwa kwa kufuata marking scheme bado ihakikiwe uongo kisa tu tunataka mission iwe accomplished??

kipi kigekuwa rahisi ama nafuu kwa mwl?? kutokumfundisha mwananfunzi ili afeli kwa kutokujua alichoulizwa ama kumfundisha kisha ukamwekee mkasi as unavyosema kwa jibu sahihi??
 
ulijuaje kwamba ao uliokaa naowakasema hayo ni waalimu?? je uliona vtambulisho vyao??ama uliwakuta shuleni??

je wafikiri kwamba hata katika matokeo haya mabovu hakuna ndugu wa waalimu ama watoto wetu?? na je waliofeli ni shule za serikali tu ama na za binafsi pia?? na katika chahce zilizofaulisha zipo za serikali??
 
Mbatia alipoleta hoja ya mitaala ya elimu ya tz wabunge wa ccm wakiongozwa na spika walimuona ni adui.
Serikali ya ccm imedhamiria kuzalisha mbumbumbu ili wawe mtaji wa ccm.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Miaka ijayo itakuwa rahisi sana kuwa sweep hawa mbumbumbu kwa kuwa hawatahitaji mtu wa kuwafundisha maisha magumu yapoje!
 
Acheni kuwasingizia walimu wetu. "Mission"ya kufelisha wanafunzi sio ya walimu bali ya serikali sema tu hii wengi hawajui. "Unategemea maziwa kwa ng'ombe asielisha akashiba"?
 
wewe na Ilunga hamna tofauti! kama hujui mitihani inavosahihishwa kaa kimya dogo!
 
kweli matokeo ya f4 yanazidi zorota kwakasi kubwa mno tatizo nini jamani.
 
matokeo haya kuwa mabaya ni sababu ya kufuta mtihani wa kidato cha pili. tutaendelea kuambulia sifuri za kutosha mpaka pale serikali hii itakapo ondolewa madarakani. upuuzi tunaoufanya watanzania kwa kupuuzia kuweka viongozi imara, matokeo yake ndio haya:wala tusilalamike sana.
 
Hyo n jitegemee,na makongo je umeiona? div. one 1,two 7,three 23 waliobak n 4 na 0,yan MAJANGA ma2pu ktk elimu,cjui na hzi shule za private nao walimu wao waligoma?
 
Siku ya leo ni kati ya siku yangu ya majonzi makubwa sana.Kwani wadogo zangu wawili, zao la shule za kata wameangukia pua.Nachelea kuamini kwamba majonzi haya yamenifika peke yangu ,yumkin hata wewe unayesoma hapa muda huu upo kwenye majonzi hata zadi ya haya niliyonayo.
Ni matokeo yaliyoniachia maswali mengi kuliko majibu.Na maadam SIRIKALI yetu isiyokuwa na huruma nasi iliamua kuitia kapuni hoja yenye mashiko ya mheshimiwa mbatia na kudai mitaala yetu ipo sawa, Nimeona heri nipate maliwazo na mawazo yenu ninyi THE GREAT THINKERS.
Matokeo mabovu ya hawa wadogo zetu nini chanzo hasa?
je ni ubutu wa walimu wetu waliopewa jukumu la kupevusha fikra za vijana wetu?
je ni uzembe wa wadogo zetu kutokupenda kujisomea bila kushurutishwa, na kuendekeza starehe,movie,video game na stori za vijiweni[camp]?
au ni ongezeko la hz shule za kisiasa wanazojitapa nazo majukwaani bila ya kutoa mifano ni kiongozi gani mwanae kapitia huku kata.Kwani dvs 4 na fld nyingi zimetokea kata.
Je ni matokeo ya ukosefu wa vitabu na maabara.Matokeo yake madogo wamekimbilia madesa ya nyambari nyangwine? madesa ambayo pindi nikisoma walimu waliyapiga vita sana.Na si ajabu mwanafunzi wa kizazi hichi ukimuuliza kama anafahamu Bunetti aKakujibu hafahamu
Mwisho wa siku nilijipa moyo kwa kusema "niliwatahadharisha kwamba necta si sawa na test ya darasani wawe makini"
Na kama ni walimu,nikawaza mbona mi kaka yao nimesoma shule za serikali (o level kibasila na a level mara sec) ambazo walimu ni tatizo daima,ni kwa nini wanafunzi wa siku hz hawana morali ya kujituma kusoma?
NAJUA MNA MENGI YA KUSEMA. ILA MI NAOMBA MAWAZO YENU ILI WALAU TUWEZE PATA MWAROBAINI WA HILI TATIZO.NA NATOA POLE ZANGU ZA DHATI KWA WOTE WALIOPATWA NA MASWAHIBU YALIYONIPATA
 
Necta wametangaza matokeo..jamani watu wamefeli sana, hiki kizazi sijui kinaelekea wapi..hali ni tete!

Hongera kwa waliofaulu, waliofeli ni wao kujipanga sana.

Mtoa mada rekebisha kiswahili chako siyo UHALISIA WA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 NINI KIMEPELEKEA KUFELI
BALI NI MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 NINI KIMESABABISHA KUFELI ?
 
uzembeeeeeeeee wa wanafunziiiiiiii wenyewe tatizoooo wamekalia mapenziii na facebook kwa sana mpaka wanasahau kilichowapeleka shuleeee !! hapo hakna kulaumu serikaliiii wala walimuuuu matoto ya siku hiziiiiii hayana spiritya kusoma enziiiiiiiiiiii zetutulikuwa tunamezaaaaaaaaa hadi nukta ila kwa sasa mwanafunziiiiii wa kidato cha nne tena wa sayansiukimuuliza what iz matter hajui kwa haliiiiiiii hiyo unategemea kitu gani rather than expecting more zerooooooooooo.... shame on you all form 4 leavers 2012
 
Haya ndo matokeo ya kufanyia siasa chafu mambo ya msingi kama elimu! CCM wanaiua hii nchi.
 
mpaka shule za private.....nyie baraza maswali mliyatoa wapi?
 
Ndugu zanguni hatutafika???!!!! Baada ya matokeo kutangazwa nilikuwa karibu na baadhi ya walimu wakishangalia kwa vifijo na ndelemo huku wakisema "our mission was perfect implemented" Aaahahaha kumbe ni mpango uliopangwa toka kwa wakuu wa chama cha walimu that wanafunzi wafelishwe ili madai yao yasikilizwe na serikali.... Ukwel wa tetesi nilizozipata na zina uhakika waalimu waliosahihisha karatasi walifanya hvyo kimakusudi na walikuwa wanatia mikasi tu ..... Mbaya zaidi hata hzo karatasi alizozionyesha waziri walimu waliziweka kimakusudi ili wanafunzi waonekane walishindwa kujibu paper!!! Chondo chonde ndugu zangun waalimu hyo si njia sahihi ya kudai haki zenu!!!!! Kuwen waungwana mlichowafanyia wadogo zetu siyo kabisaaaaaa!!!! Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Jamani hii kali gamba huyu kurusha lawama zote kwa walimu eti wamesahihisha vibaya mmmmh! nachangia uzi huu nikiwa na uchungu na utendaji wa Waziri Shukuru Kawambwa jamaa ni dhaifu ( lege lege) lakini ndugu yake Mtukufu JK anamhamisha wizara moja kwenda nyingine anapobadili baraza.Jamaa kiti kimekuwa cha moto, leo badala ya kumwachia Katibu wa NECTA Mama Joyce Ndalichako afanye kama anavyofanya miaka iliyopita kaibuka eti anatangaza matokeo daaah!Waziri mbovu amefunikwa utendaji hata na Naibu wake aliyesema Tanzania is made up of the islands of Pemba and Zimbabwe MULUGO kwani naibu anafanya kazi zinaonekana pamoja na kutuhumiwa na Mh.Joseph Mbilinyi kuwa alifeli na akaamua kununua jina la mtu mwingine.Ni aibu kwa yeye kutakiwa kujiuzulu kwa kudanganya bunge kuwa nchi ina mitaala kumbe hakuna na Spika na Naibu wake kukandamiza wapinzani kwani hawawajali Watanzania wanaangalia kutetea Serikali ya Chama chao kwa manufaa yao wachache leo matokeo yanatoka zaidi ya nusu ya watahiniwa wamepata sifuri!Kweli mficha maradhi kifo humuumbua! Kwa aibu anaibuka eti yeye leo mtangaza matokeo kwanini asimwachie Mama Ndalichako. KAWAMBWA unamulikwa na watetezi wa wanyongekama Mbatia na Lissu wewe hujali unadai mitaala ipo eti unaamka leo kutoka katika usingizi wako ulikuwa wapi kuchakarika na kufanya kazi kama Waziri wa Elimu!Mpaka watoto wafeli vibaya ndo uwe mbele mbele hatari sana. Cargo wewe ni mwana propaganda husemi ukweli eti waalimu wamesahihisha vibaya sio sawa kwani elimu imeshuka mtihani wa kidato cha pili ulifutwa,shule za kata hazina maabara,maktaba,vifaa kama vitabu,walimu wachache n.k..CARGO HUANGALII VYANZO VYA TATIZO UNAANGALIA MATOKEO yaani huangalii ulipojikwaa unaangalia ulipoangukia gamba kweli kweli wewe unataka kupotosha ukweli kwa wana JF na wageni wanaotembelea humu .Au umetumwa kuhamishia lawama kwa walimu kwani humu JF kuna mamluki wengi sana wanapindisha ukweli uwe uongo na uongo uonekane ukweli.JAMANI MUWE NA UCHUNGU WATOTO WETU MNAWALISHA SUMU KIELIMU WANAKUWA MBU MBU MBU. Nisiongee matatizo tu SULUHISHO NI HILI (MAWAZO YANGU NAKARIBISHA WENGINE ZAIDI) 1.SERIKALI IANGALIE UPYA NA KUREKEBISHA SEKTA YA ELIMU AMBAYO NDIO UTI WA MGONGO WA TAIFA LETU IFANYE HIVI HUU NI USHAURI WA BURE (a)Irekebishe maslahi ya waalimu ili ivutie vijana wenye uwezo mzuri kama Daraja la kwanza na la Pili kujiunga na mafunzo ya ualimu.Haiyumkiniki waliopata daraja la nne mwishoni na sifuri na wanaoghushi vyeti kusomea ualimu kufundisha vijana wetu kuanzia chekechea mpaka juu.Cream inatakiwa iwaelekeze watanzania wengine sio ubovu kwani unazalisha ubovu mbaya zaidi. (b)Wale waalimu wliopo na wanaopangiwa vijijini waongezewe maslahi na malipo zaidi ya wa mijini ili kuvutia waalimu waende katika mazingira hayo magumu kufanya kazi na kusaidia elimu kuboreka katika shule za kata. (c)Shule za kata zilijengwa kisiasa kuonesha watoto wengi wanaenda Sekondari bila ubora wa Elimu yenyewe, Siasa ziachwe katika jambo muhimu kama hili ni aheri shule chache bora kuliko shule nyingi mbovu. (d) Wananchi tuamke kudai serikali itutimizie huduma kama elimu kwani Watanzania tuna udhaifu wa kudai kutimiziwa haki zetu wakati kodi tunalipa hata kwa njia isiyo ya moja kwa moja bei zipo juu sana na mifumuko ya bei za bidhaa kila siku,pia tunakatwa sana mishahara.Wafanye kazi wasiwabane mbavu watetezi wetu bungeni wanapojaribu kutumia nafasi ya bunge kuibana serikali.Hatupendi Bunge muhuri na linalotetea serikali.Serikali(executive), mahakama (judiciary) na bunge (parliament) zote zinajitegemea bila kumwingilia mwenzake na tulowachagua watutetee sio kulinda serikali isiyodeliver. LEO NAISHIA HAPA ELIMU NDIO UFUNGUO WA MAISHA
 
Last edited by a moderator:
Mimi nimefurahishwa na mavuno ya serikali ya ccm na shule zao za kata, ona sasa, mwaka jana Wanafunzi wakaandika BONGO Fleva na kuchora maua, Leo Mitusi,... next wataishia kuwapiga then kuwala 0713 then DEATH. Chama Chetu cha Mapinduziiii chajengaaa nchiiiiiiiiii..........:rockon:
 
elimu inawekwa rehani! ukombozi ni muhimu kwa sasa.
 
Back
Top Bottom