Mbatia alipoleta hoja ya mitaala ya elimu ya tz wabunge wa ccm wakiongozwa na spika walimuona ni adui.
Serikali ya ccm imedhamiria kuzalisha mbumbumbu ili wawe mtaji wa ccm.
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Necta wametangaza matokeo..jamani watu wamefeli sana, hiki kizazi sijui kinaelekea wapi..hali ni tete!
Hongera kwa waliofaulu, waliofeli ni wao kujipanga sana.
Jamani hii kali gamba huyu kurusha lawama zote kwa walimu eti wamesahihisha vibaya mmmmh! nachangia uzi huu nikiwa na uchungu na utendaji wa Waziri Shukuru Kawambwa jamaa ni dhaifu ( lege lege) lakini ndugu yake Mtukufu JK anamhamisha wizara moja kwenda nyingine anapobadili baraza.Jamaa kiti kimekuwa cha moto, leo badala ya kumwachia Katibu wa NECTA Mama Joyce Ndalichako afanye kama anavyofanya miaka iliyopita kaibuka eti anatangaza matokeo daaah!Waziri mbovu amefunikwa utendaji hata na Naibu wake aliyesema Tanzania is made up of the islands of Pemba and Zimbabwe MULUGO kwani naibu anafanya kazi zinaonekana pamoja na kutuhumiwa na Mh.Joseph Mbilinyi kuwa alifeli na akaamua kununua jina la mtu mwingine.Ni aibu kwa yeye kutakiwa kujiuzulu kwa kudanganya bunge kuwa nchi ina mitaala kumbe hakuna na Spika na Naibu wake kukandamiza wapinzani kwani hawawajali Watanzania wanaangalia kutetea Serikali ya Chama chao kwa manufaa yao wachache leo matokeo yanatoka zaidi ya nusu ya watahiniwa wamepata sifuri!Kweli mficha maradhi kifo humuumbua! Kwa aibu anaibuka eti yeye leo mtangaza matokeo kwanini asimwachie Mama Ndalichako. KAWAMBWA unamulikwa na watetezi wa wanyongekama Mbatia na Lissu wewe hujali unadai mitaala ipo eti unaamka leo kutoka katika usingizi wako ulikuwa wapi kuchakarika na kufanya kazi kama Waziri wa Elimu!Mpaka watoto wafeli vibaya ndo uwe mbele mbele hatari sana. Cargo wewe ni mwana propaganda husemi ukweli eti waalimu wamesahihisha vibaya sio sawa kwani elimu imeshuka mtihani wa kidato cha pili ulifutwa,shule za kata hazina maabara,maktaba,vifaa kama vitabu,walimu wachache n.k..CARGO HUANGALII VYANZO VYA TATIZO UNAANGALIA MATOKEO yaani huangalii ulipojikwaa unaangalia ulipoangukia gamba kweli kweli wewe unataka kupotosha ukweli kwa wana JF na wageni wanaotembelea humu .Au umetumwa kuhamishia lawama kwa walimu kwani humu JF kuna mamluki wengi sana wanapindisha ukweli uwe uongo na uongo uonekane ukweli.JAMANI MUWE NA UCHUNGU WATOTO WETU MNAWALISHA SUMU KIELIMU WANAKUWA MBU MBU MBU. Nisiongee matatizo tu SULUHISHO NI HILI (MAWAZO YANGU NAKARIBISHA WENGINE ZAIDI) 1.SERIKALI IANGALIE UPYA NA KUREKEBISHA SEKTA YA ELIMU AMBAYO NDIO UTI WA MGONGO WA TAIFA LETU IFANYE HIVI HUU NI USHAURI WA BURE (a)Irekebishe maslahi ya waalimu ili ivutie vijana wenye uwezo mzuri kama Daraja la kwanza na la Pili kujiunga na mafunzo ya ualimu.Haiyumkiniki waliopata daraja la nne mwishoni na sifuri na wanaoghushi vyeti kusomea ualimu kufundisha vijana wetu kuanzia chekechea mpaka juu.Cream inatakiwa iwaelekeze watanzania wengine sio ubovu kwani unazalisha ubovu mbaya zaidi. (b)Wale waalimu wliopo na wanaopangiwa vijijini waongezewe maslahi na malipo zaidi ya wa mijini ili kuvutia waalimu waende katika mazingira hayo magumu kufanya kazi na kusaidia elimu kuboreka katika shule za kata. (c)Shule za kata zilijengwa kisiasa kuonesha watoto wengi wanaenda Sekondari bila ubora wa Elimu yenyewe, Siasa ziachwe katika jambo muhimu kama hili ni aheri shule chache bora kuliko shule nyingi mbovu. (d) Wananchi tuamke kudai serikali itutimizie huduma kama elimu kwani Watanzania tuna udhaifu wa kudai kutimiziwa haki zetu wakati kodi tunalipa hata kwa njia isiyo ya moja kwa moja bei zipo juu sana na mifumuko ya bei za bidhaa kila siku,pia tunakatwa sana mishahara.Wafanye kazi wasiwabane mbavu watetezi wetu bungeni wanapojaribu kutumia nafasi ya bunge kuibana serikali.Hatupendi Bunge muhuri na linalotetea serikali.Serikali(executive), mahakama (judiciary) na bunge (parliament) zote zinajitegemea bila kumwingilia mwenzake na tulowachagua watutetee sio kulinda serikali isiyodeliver. LEO NAISHIA HAPA ELIMU NDIO UFUNGUO WA MAISHANdugu zanguni hatutafika???!!!! Baada ya matokeo kutangazwa nilikuwa karibu na baadhi ya walimu wakishangalia kwa vifijo na ndelemo huku wakisema "our mission was perfect implemented" Aaahahaha kumbe ni mpango uliopangwa toka kwa wakuu wa chama cha walimu that wanafunzi wafelishwe ili madai yao yasikilizwe na serikali.... Ukwel wa tetesi nilizozipata na zina uhakika waalimu waliosahihisha karatasi walifanya hvyo kimakusudi na walikuwa wanatia mikasi tu ..... Mbaya zaidi hata hzo karatasi alizozionyesha waziri walimu waliziweka kimakusudi ili wanafunzi waonekane walishindwa kujibu paper!!! Chondo chonde ndugu zangun waalimu hyo si njia sahihi ya kudai haki zenu!!!!! Kuwen waungwana mlichowafanyia wadogo zetu siyo kabisaaaaaa!!!! Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Inashangaza, hiyo si shule ya wajinga aka Waislaam?