Uhalisia wa mbinguni au peponi

Uhalisia wa mbinguni au peponi

Jokajeusi

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2018
Posts
6,323
Reaction score
10,813
Wasalamu wakuu!

Moja kwa moja kwenye mada.
Watu wamekuwa wakifundishwa mafundisho mbalimbali kuhusu mbinguni na kuzimu. Mafundisho mengi kama si yote ni uongo na uzushi mtupu. Dunia imehadaiwa na watu wajanja kwa manufaa ya wachache.

Mbinguni ni nini?
Mbinguni ni wapi?
Nani anaishi huko?
Nani mtawala wa mbinguni?
Ni umbali gani kutoka hapa duniani kufika huko?
Njia ipi ni rahisi kufika huko?
Je kuna uhusiano wa karibu kati ya dunia na mbinguni?
Je ipo haja ya kuamini uwepo wa mbinguni?
Je ni kweli watu wataenda mbinguni?
Je wakifika huko watafanya nini?

Mbinguni ni nini?
Mbinguni ni mkusanyiko wa jumuiya ya viumbe wenye fikara njema ambao huishi bila mwili. Kumbuka ni mawazo au fikara zilizonjema

Mbinguni ni wapi?
Mbinguni ni sehemu njema kimawazo ambapo fikara za wanadamu wenye mawazo mema huishi huko. Hapa fikara ichukuliwe kama akili au roho yenye utambuzi.

Nani anaishi huko?
Yeyote mwenye mawazo mema huishi huko kimawazo, atakapokufa mwili hufa lakini fikara zake huishi kwenye jumuiya hiyo. Mwanadamu akiwaza mema huanza maisha ya pepo safi tokea akiwa mwilini. Fikara njema huishi milele tofauti na kinyume chake.

Nani mtawala wa mbinguni?
Hakuna mtawala wa mbinguni isipokuwa mwenye fikara njema. Hakuna mkubwa wala mdogo, hakuna rangi katika fikara njema wala jinsia hivyo hakuna kuoa wala kuolewa huko mbinguni. Mtu mmoja anaweza kuuliza inamaana hakuna Mungu. Jibu ni kuwa kama ilivyofikara isivyoonekana ndivyo Mungu asivyoonekana. Vifikara vyema viwapo kwa binadamu huwafanya wanadamu kuwa miungu lakini mwanadamu ajapokufa fikara yake huishi kwenye fikara kubwa kulingana na aina ya fikara yake.

Ni umbali gani kutoka hapa duniani mpaka mbinguni?
Hakuna umbali wowote, ni sawa na kilomita sifuri yaani ni sawa na kusema hakuna umbali. Mbingu ipo fikarani mwa mtu. Kama mtu akifikiri mabaya basi hana mbingu fikarani halikadhalika na mwenye kufikiri mema hana kuzimu. Msamiati hii yaan Mbinguni na Kuzimu ni dhahania kama ilivyo mawazo ya mtu. Nikisema mawazo namaanisha kuzimu kupo na mbinguni pia kupo. Fikara ya mtu ndio mbingu au kuzimu ya mtu.

Njia ipi rahisi kufika huko?
Kwa kufikiri tuu. Ukitaka kwenda mbinguni ni kuwaza mema. Ukitaka kwenda kuzimu fanya hivyo hivyo. Kila kitu kipo fikarani mwa mtu.

Je kuna uhusiano wa karibu wa mbinguni na duniani?
Ndio, uhusiano ni mkubwa. kama nilivyosema fikara ndio mbingu na hiyo hiyo huweza kuwa kuzimu. Ni sawa na kusema, je kuna uhusiano wa karibu baina ya akili ya mwanadamu na gari, au nguo, au ndege n.k? Tafsiri ni kuwa bila mbingu na kuzimu yaani fikara hizi dunia isingeumbwa.

Je ipo haja ya kuamini uwepo wa mbinguni?
Haja ipo kutokana na kuwa mbingu ipo fikarani mwako. Ili fikara yako iishi dawamu basi sharti iwaze mambo mema. Kama ukitaka uishi kwa muda sharti uwaze mabaya.

Je ni kweli watu wataenda mbinguni?
Hapana, Watu hawawezi kwenda mbinguni kwani wao ni udongo na mbinguni ni jumuiya wa fikara njema. Ila fikara zao ndio huishi huko ikiwa ni njema na si zitaenda kwani mwanadamu tokea anazaliwa fikara yake huishi peponi au kuzimu kulingana na jinsi anavyowaza.

Je wakifika huko watafanya nini?
Hawawezi kufika, fikara njema ndizo zitaishi huko tangu sasa.

Mbinguni si sehemu physikali ili mtu aende kwa miguu au kwa chombo chochote. Hakuna umbali ndio maana nikasema huwezi enda kiumbo. Kuna watu wanawalghai watu wakisema mbinguni ni mbali sijui kilometa ngapi, sijui itakuchukua miaka 73 kufika huko. Huo ni uongo peupe. Sehemu yoyote isiyo ya kiumbo haina umbali. unaweza ukajigawanya hata mara mia ukawepo kote kote. ndio maana watu huweza kujiuliza hivi ni shetani anawezaje kudanganya watu mamilioni maeneo tofauti tofauti kwa sekunde moja. Hii ni kutokana na fikara tuu. Anachodili nacho nifikara Ovu. hivyo huweza kudanganya hata ulimwengu mzima kwa sekunde ikiwa ulimwengu mzima unafikara mbaya

Porojo za kwenda mbinguni ni ishu za kilaghai zaidi na zaidi. Mwanadamu hawezi kwenda mbinguni kama vile samaki asivyoweza ishi nchi kavu. Na kama itatokea akafanyiwa modification ili aweze ku-survive mbinguni ambapo ni sehemu iliyopo kifikara basi atakuwa si mwanadamu tena bali kiumbe kingine. Na huko kutakuwa si mbinguni.
 
Umejieleza vizuri ila nilijitahidi kuwaeleza walokole kuhusu mbingu wakawa wakali nikaingia mitini. Sasa mbona tuliambiwa Yesu alipaa mbinguni? Huenda ni hekaya za abunuwasi.
 
Umejieleza vizuri ila nilijitahidi kuwaeleza walokole kuhusu mbingu wakawa wakali nikaingia mitini. Sasa mbona tuliambiwa Yesu alipaa mbinguni? Huenda ni hekaya za abunuwasi.

embu fikiri pamoja nami
Walisema alipaa kuelekea huko juu ambapo wengi hupahusisha na mbinguni jambo ambalo ni tata na linamafungamano na uongo kwa kiasi kikubwa.
Huko juu yaani angani kuna milki nyingi za anga. huwezi ukaumbwa duniani ukafie mbinguni, au ukaishi mbinguni. Hata ukisoma kile kitabu cha chenye historia ya wayahudi ambapo kanisa katoliki limekiita Biblia. Kipo wazi kwa sehemu kubwa. Mwanadamu aliumbwa duniani akapewa bustani ambayo ndiyo ilikuwa kiunganishi cha mwili wake na fikara yake(hapa fikara ni mbingu ambapo fikara kuu ni Mungu) Kumbuka fikara haionekani wala kushikika.

Pia Adamu aliumbwa nje ya edeni baadaye ndio aliletwa edeni baada ya wazo kuu kufikiria ishu ya hii bustani. Sharti kubwa alilopewa adamu ni kuwa akiwa pale edeni asije kula tunda la kati lenye maujuzi ya mema na mabaya kwani atakapokula kifo kitakuwa mshahara wake. Kifo hapa ni kuzimu Mkuu. Na edeni ndio pepo au mbingu. kitendo cha yeye kula lile tunda alijikuta yupo uchi lakini hakufa kimwili lakini kifikara tayari alikuwa kuzimu. Hivyo Mungu aliamua kumtimua katika bustani ya edeni kwani kimwili hakuwa kiumbe wa pande hizo. Ili arudi mavumbini yaani katika dunia alipotokea
 
Mkuu umeweka ukweli fikirishi sana ngoja tuendelee kufikiri tu

Kila kitu ni fikara mkuu.
Ukifikiri utajiri,basi nafsi yako huishi kitajiri na kupata utajiri ni haki yako.
huwezi kufikiri kujenga nyumba nzuri alafu usiijenge. Wazo ndio kila kitu mkuu
 
Ila ukweli ni kuwa mbinguni ni hali si mahali,kuzimu ni hali si mahali ,toharani ni hali si mahali.Uungu ni sifa na si jina kamilifu bali huwakilisha sifa ya uwezo usioshindwa.Roho ni hali tupu isiyo na chochote ndani yake kwakuwa yenyewe si kitu bali ni hali.Kweli hizi chungu ni ngumu kuzielewa na kisha kuzikubali.Mfano kufa ni hali si kitu ni hali ya kutokuwa na uhai kumbe uhai nao ni hali.
 
Ila ukweli ni kuwa mbinguni ni hali si mahali,kuzimu ni hali si mahali ,toharani ni hali si mahali.Uungu ni sifa na si jina kamilifu bali huwakilisha sifa ya uwezo usioshindwa.Roho ni hali tupu isiyo na chochote ndani yake kwakuwa yenyewe si kitu bali ni hali.Kweli hizi chungu ni ngumu kuzielewa na kisha kuzikubali.Mfano kufa ni hali si kitu ni hali ya kutokuwa na uhai kumbe uhai nao ni hali.


Safi sana, wewe unaelewa sana mkuu
 
Bustani ya eden kwangu ni fix iliyokubuhu , hata gharika kuu ni vitu vya kufikirika tu . Kila mtu anajua imani yake usisubiri eti uambiwe Mungu anakupenda eti utoe sadaka, Mungu hali sadaka ila watu wanaokuzunguka wanahitaji msaada na toa mwenyewe kwa mkono wako. Handanganywi mtu hapa. Mkuu nakubaliana nawe kuhusu mbingu " keep it up"
 
Daaah kwihiyo MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI?


Malipo ya mwili ni hapa hapa duniani mkuu.
Adhabu ilishatolewa tangu mwanzo kuwa ukichagua kuishi daima basi kuwa na fikara njema lakini ukitaka kupotea kuwa na fikara mbaya.

Zaidi na zaidi ni kuwa, ukiona umetenda hujaadhibiwa jua watoto wako wapo kwenye orodha ya adhabu zako. Ikiwa mtoto anarithi sura, rangi, tabia n.k pia uwezekano wa kurithi adhabu zako upo.
 
Bustani ya eden kwangu ni fix iliyokubuhu , hata gharika kuu ni vitu vya kufikirika tu . Kila mtu anajua imani yake usisubiri eti uambiwe Mungu anakupenda eti utoe sadaka, Mungu hali sadaka ila watu wanaokuzunguka wanahitaji msaada na toa mwenyewe kwa mkono wako. Handanganywi mtu hapa. Mkuu nakubaliana nawe kuhusu mbingu " keep it up"


Edeni ni fix kwa kigezo cha yenyewe kuwa duniani eti pale sijui Iraq lakini ukweli ni kuwa Eden ni mbingu ambayo fikara njema ya adamu na hawa walikuwa wakiishi huko.
 
Alhamisi Imeamka kivyake, [emoji23][emoji23][emoji3] haina uhusino na siku ingine
 
Atutaki upuuzi wao tena.
tapatalk_1516361334135.jpeg
 
Back
Top Bottom