Jokajeusi
JF-Expert Member
- Jun 1, 2018
- 6,323
- 10,813
Wasalamu wakuu!
Moja kwa moja kwenye mada.
Watu wamekuwa wakifundishwa mafundisho mbalimbali kuhusu mbinguni na kuzimu. Mafundisho mengi kama si yote ni uongo na uzushi mtupu. Dunia imehadaiwa na watu wajanja kwa manufaa ya wachache.
Mbinguni ni nini?
Mbinguni ni wapi?
Nani anaishi huko?
Nani mtawala wa mbinguni?
Ni umbali gani kutoka hapa duniani kufika huko?
Njia ipi ni rahisi kufika huko?
Je kuna uhusiano wa karibu kati ya dunia na mbinguni?
Je ipo haja ya kuamini uwepo wa mbinguni?
Je ni kweli watu wataenda mbinguni?
Je wakifika huko watafanya nini?
Mbinguni ni nini?
Mbinguni ni mkusanyiko wa jumuiya ya viumbe wenye fikara njema ambao huishi bila mwili. Kumbuka ni mawazo au fikara zilizonjema
Mbinguni ni wapi?
Mbinguni ni sehemu njema kimawazo ambapo fikara za wanadamu wenye mawazo mema huishi huko. Hapa fikara ichukuliwe kama akili au roho yenye utambuzi.
Nani anaishi huko?
Yeyote mwenye mawazo mema huishi huko kimawazo, atakapokufa mwili hufa lakini fikara zake huishi kwenye jumuiya hiyo. Mwanadamu akiwaza mema huanza maisha ya pepo safi tokea akiwa mwilini. Fikara njema huishi milele tofauti na kinyume chake.
Nani mtawala wa mbinguni?
Hakuna mtawala wa mbinguni isipokuwa mwenye fikara njema. Hakuna mkubwa wala mdogo, hakuna rangi katika fikara njema wala jinsia hivyo hakuna kuoa wala kuolewa huko mbinguni. Mtu mmoja anaweza kuuliza inamaana hakuna Mungu. Jibu ni kuwa kama ilivyofikara isivyoonekana ndivyo Mungu asivyoonekana. Vifikara vyema viwapo kwa binadamu huwafanya wanadamu kuwa miungu lakini mwanadamu ajapokufa fikara yake huishi kwenye fikara kubwa kulingana na aina ya fikara yake.
Ni umbali gani kutoka hapa duniani mpaka mbinguni?
Hakuna umbali wowote, ni sawa na kilomita sifuri yaani ni sawa na kusema hakuna umbali. Mbingu ipo fikarani mwa mtu. Kama mtu akifikiri mabaya basi hana mbingu fikarani halikadhalika na mwenye kufikiri mema hana kuzimu. Msamiati hii yaan Mbinguni na Kuzimu ni dhahania kama ilivyo mawazo ya mtu. Nikisema mawazo namaanisha kuzimu kupo na mbinguni pia kupo. Fikara ya mtu ndio mbingu au kuzimu ya mtu.
Njia ipi rahisi kufika huko?
Kwa kufikiri tuu. Ukitaka kwenda mbinguni ni kuwaza mema. Ukitaka kwenda kuzimu fanya hivyo hivyo. Kila kitu kipo fikarani mwa mtu.
Je kuna uhusiano wa karibu wa mbinguni na duniani?
Ndio, uhusiano ni mkubwa. kama nilivyosema fikara ndio mbingu na hiyo hiyo huweza kuwa kuzimu. Ni sawa na kusema, je kuna uhusiano wa karibu baina ya akili ya mwanadamu na gari, au nguo, au ndege n.k? Tafsiri ni kuwa bila mbingu na kuzimu yaani fikara hizi dunia isingeumbwa.

Haja ipo kutokana na kuwa mbingu ipo fikarani mwako. Ili fikara yako iishi dawamu basi sharti iwaze mambo mema. Kama ukitaka uishi kwa muda sharti uwaze mabaya.
Je ni kweli watu wataenda mbinguni?
Hapana, Watu hawawezi kwenda mbinguni kwani wao ni udongo na mbinguni ni jumuiya wa fikara njema. Ila fikara zao ndio huishi huko ikiwa ni njema na si zitaenda kwani mwanadamu tokea anazaliwa fikara yake huishi peponi au kuzimu kulingana na jinsi anavyowaza.
Je wakifika huko watafanya nini?
Hawawezi kufika, fikara njema ndizo zitaishi huko tangu sasa.
Mbinguni si sehemu physikali ili mtu aende kwa miguu au kwa chombo chochote. Hakuna umbali ndio maana nikasema huwezi enda kiumbo. Kuna watu wanawalghai watu wakisema mbinguni ni mbali sijui kilometa ngapi, sijui itakuchukua miaka 73 kufika huko. Huo ni uongo peupe. Sehemu yoyote isiyo ya kiumbo haina umbali. unaweza ukajigawanya hata mara mia ukawepo kote kote. ndio maana watu huweza kujiuliza hivi ni shetani anawezaje kudanganya watu mamilioni maeneo tofauti tofauti kwa sekunde moja. Hii ni kutokana na fikara tuu. Anachodili nacho nifikara Ovu. hivyo huweza kudanganya hata ulimwengu mzima kwa sekunde ikiwa ulimwengu mzima unafikara mbaya
Porojo za kwenda mbinguni ni ishu za kilaghai zaidi na zaidi. Mwanadamu hawezi kwenda mbinguni kama vile samaki asivyoweza ishi nchi kavu. Na kama itatokea akafanyiwa modification ili aweze ku-survive mbinguni ambapo ni sehemu iliyopo kifikara basi atakuwa si mwanadamu tena bali kiumbe kingine. Na huko kutakuwa si mbinguni.