POTOSHI Uhalisia wa picha hii ya Rais Samia akidaiwa kuwa na Mnaijeria David?

POTOSHI Uhalisia wa picha hii ya Rais Samia akidaiwa kuwa na Mnaijeria David?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu kupitia mitandao mbalimbali ikiwemo X kuekuwa na picha hii inayosambaa kwa kasi, uhalisia ni upi?
1779733595216.png
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo X kuanzia Mei 25, 2026, kumekuwa na picha inayosambaa ikimuonesha Rais Saia Suluhu Hassan na kudaiwa amesimama na mwandishi wa habari za uchunguzi, mwandishi na mtasharishaji wa Filamu kutokea nchini Nigerja David Hundeyin.

Uhalisia wa Picha hyo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kwa kutuia nyenzo za kidigitali umebaini kuwa picha hiyo si halisi bali imehaririwa kwa kutumia nyenzo za kidigitali.

Kwa kutumia google reverse image search imebainika kuwa picha halisi inamuonesha aliyekuwa waziri wa fedha, ambaye kwa sasa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba akiwa na Rais Samia. Picha hiyo ilichapishwa na Mwigulu mwenyewe Januri 27, 2025 kupitia ukurasa wake wa X.
1779734273696-png.3595005

Mwigulu alichapisha picha hiyo na ujumbe uliosomeka:

"Hongera na baraka tele katika siku yako ya kuzaliwa, Mheshimiwa Rais Dkt. @SuluhuSamia. Mungu akujalie afya na siha njema, hekima na mafanikio katika uongozi wako. Happy Birthday MAMA."

Hivyo basi picha innayosambaa kuanzia Mei 25, 2026 kupitia mitandao ya kijamii si hali bali iehaririwa kwa kutumia nyenzo za kdigitali.
Back
Top Bottom