Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
Nawasalimia wote JF.
Nimeamua kuandika jumbe mbalimbali kwa lengo la kufundisha na kuwafumbua macho waliotayari.
Leo hii nitaongelea suala la huyu anayeitwa shetani. Imetokea kuogopwa sana na kuonekana ni kiumbe hatari sana (Kiumbe wa kusadikika).
Kwa kuwa nililelewa katika dini ya kikristo nimekuwa nikikaa na kuyatafakari maandiko matakatifu.
Nikiri kwamba biblia imejaa uvuvio wa roho. Ndani ya hiyo biblia kuna mambo ukiyafanya na kuyachukulia serious unafanikiwa sana.
Katika kuyasoma maandiko nimekuja kugundua kwamba:-
1. Aliye laaniwa katika bustani ya edeni siyo shetani bali ni nyoka.
Mwanzo 3 inaeleza yote kwa Nyoka alikuwa "mwelevu" kuliko wanyama wote wa mwituni. Maana yake Nyoka alikuwa na akili. Alikuwa anajua mambo mengi. Na ikumbukwe wanyama waliumbwa kabla ya watu.
Na kwa jinsi ninavyotafakari kwa kina. Mungu alipowaumba wanyama, ilipita muda, kwamba hao wanyama walipewa mafundisho mbalimbali na Mungu. Ikatokea Nyoka akawa na akili kuliko wengine. Lakini Mungu akaona aumbe mtu kwa mfano wao.
Hapa tunaona kabisa aliyeenda kuongea na Hawa ni Nyoka. Na hapa ukisoma issue Hawa ndiye aliyeongea uongo. Yeye nyoka alimuuliza Swali linaloanzia na "eti" Mungu kawakataza kula matunda ya miti yote!?
Hawa aliongezea umbea kwa mti wa kati wamekatazwa hata kuugusa.
Sehemu ya pili ni pale Mungu anatoa laana. Utakuta yule aliyelaaniwa ni Nyoka na siyo Shetani.
Mfundisho:- Yule atakayeweza kuwasiliana na Nyoka huenda akajuwa mambo mengi sana, kwa sababu yeye ni mwelevu.
2. Ayubu alikuwa akimtumikia YAHWEH kwa uelekevu. Ukisoma Ayubu Sura ya 2. Utaona wana wa Mungu walipoenda kujihudhurisha Mbele ya Yahweh Shetani naye alikuwepo.
Hapa tunaona kabisa kuwa Shetani na wana wa Yahweh hawana ugomvi wowote. Maana yake na yeye ni sehemu ya hao. Ukiendelea kusoma Yahweh alimuuliza Shetani kuwa ametoka wapi!? Na akamuuliza kuwa amemuona Ayubu, maana shetani alikuwa akipeleka taarifa kwa Mungu kuhusu Ayubu.
Kwa kukatisha Maelezo Shetani alikuwa akiripoti mara kwa mara kwa Yahweh.
Fundisho:- Shetani ni kati ya watumishi wa Yahweh.
3. Yesu alipokuwa akiwafundisha wanafunzi wake namna ya kusali. Alisema salini hivi:-
Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako kitukuzwe, ufalme wako uje, mapenzi yako tatimizwa hapa duniani kama huko mbinguni, usitutie majaribuni (Katika vishawishi)......
Sasa hapa tunaona wazi kabisa kumbe Baba aliye mbinguni ndiye anayetutia sisi katika vishawishi. Wala siyo shetani. Na ukiangalia sehemu nyingi katika Maandiko utaona namna Mungu alivyokuwa akiwatia kwenye vishawishi. Wengine alikuwa akiwatia moyo mgumu.
Mfano Farao alitiwa moyo mgumu na Mungu mwenyewe. Sauli alitiwa roho mbaya. Daudi alijazwa ushawishi na Mungu ili awahesabu wana wa Israeli.
Fundisho:- Hapa tunaona anayewaweka kwenye vishawishi huwa ni Mungu mwenyewe.
SHETANI NI NANI!?
Ukifuatilia kwa makini sana kwenye biblia utagundua, Shetani ni kati ya watumishi waaminifu wa Mungu. Kwamba shetani kazi yake ni kupeleka taarifa negative za mtu kwa Mungu. Yaani shetani ni mtumishi wa Mungu kwa kazi maalum. Yaani ni watu wasiojulikana wa Mungu.
Nawasilisha.