Umejitahidi kueleza kwa kirefu lakini umeacha maswali mengi kuliko majibu uliyojaribu kujibu kwenye Akili za walio wengi.
Nijibu maswali yangu machache nikijibiwa nitarudi tena,
(1) wayahudi wa kweli mpaka sasa wako wapi?na nchi gani?
(2) Ni ushahidi gani unauotoa kudhihirisha kwamba wale wajakazi wa wake wa yakobo ambao Yakobo alizaa nao ni weusi kutoka kushi?
(3)biblia inaonyesha baada ya Yesu kupaa wanafunzi wake walikimbia uyahudi kuogopa kuuwawa na kukimbilia maeneo mbalimbali kama korintho,efeso, filipi,na maeneo mengi.
Na siku ya sabato walikuwa wakiingia kwenye masinagogi ya wayahudi kuhubiri habari za Yesu.
Je huko waliokuwa wayahudi ktk maeneo niliyotaja ndiyo huko ethiopia?
Yaani Filipi,korintho efeso ,Rumi na kwingineko ndio huko Ethiopia na misiri kwa waafirica wenzao?[/QUOTE/punainen/sokoro waito]
Nakujibu kama ifuatavyo
(1) wayahudi wa kweli mpaka sasa wako wapi?na nchi gani?
Wayahudi wa kweli % chache sana haizidi hata 1 ya hao waliopo hapo israel wapo israel sasahivi to the point unaweza sema hawapo kabisa,hiyo 1% ndio wale wayahudi wa ethiophia ambao ni weusi kabisa kama mimi na wewe HIYO 99% ya wayahudi halisi iliyobakia imetawanywa duniani kote kama neno la Mungu lilivyosema katika luka 21:20-24 Yesu alikuwa anawatabiria wayahudi kuhusu yatakayowapata baada ya kukataa neno lake mwishoni mstari wa 24 unasema "watachukuliwa mateka(utumwani) na mataifa yoote na mataifa (hawa wayahudi fake sasa wakipindi hiki) wataukalia Yerusalemu,hata majira ya mataifa yatakapo timia (mpaka Yesu atakapo rudi mara ya pili)"na sababu ya hiyo 1% ya wayahudi wa ethiophia kutangulia pale israel leo nikuwa wao hawakutawanywa kwenda utumwani kama hilo andiko la Luka linavyosemwa sababu hawakuwepo kipindi Yesu amekuja so ile laana ya kumkataa wao haipo juu yao ndiomaana leo wametangulizwa pale,
Sasa kama kifungu cha Luka 21 hakitakata kiu yako,naanza tangia mwanzo taifa la israel linatoka Misri kwenda Kaanani,
Musa na Haroon hawakuingia kaanan sababu hawakumwamini Mungu,walikuwa na mashaka-mashaka Hesabu 20:12! ndiomaana iliwachukua miaka 40 safari ya siku 3 tu Mungu alisubiri hadi watoto wao ambao walikuja kumwamini waingie kaanani ndiomaana waliotoka Misri na kuingia kaanan ni joshua na caleb tu kati ya wanaume laki 6 walioianza safari kutokea misri! Hesabu 32:11-13.
>Mara ya kwanza wana wa israeli kumkosea Mungu wakiwa Kaanani (Uasi wa Kwanza) baada ya kifo cha Joshua na Kaleb "Waamuzi 2:11-14,walimuacha Bwana wakamtumikia Baali(wakavunja lile agano Mungu alilomuapia Abraham na Yakobo) Mungu akawatia mikononi mwa maadui zao kila mahali! waamuzi 2:18 baada ya kumrudia Mungu,akawainulia waamuzi,mwamuzi huyo akawaokoa kwenye mikono ya maadui zao, ukiendelea kusoma mstari wa 19 hadi mwisho wa hicho kitabu choote cha Waamuzi then ukaendelea vitabu vyoote vya agano la kale kuanzia kitabu cha kutoka hadi Malaki (sina haja yakukupa vifungu vyoote) kila mara wana wa Israel walipokuwa wakifanya uasi,wakivunja yale maagano ambayo Mungu aliwaapia Baba zao Mungu alikuwa anawapatiliza(anawalipiza,anawaadhibu) kwa kuwaweka kwenye mikono ya maadui zao huko watateswa nakufanywa watumwa mpaka wanamkumbuka Mungu wao na kutubu dhambi zao Mungu ni Mungu wa Rehema anakumbuka yale Maagano aliyowaahidi baba zao na kisha anawasamehe then kitu cha kwanza (KUWA MAKINI HAPA) Mungu anawainulia Mwamuzi au Nabii kati yao ambaye roho wa bwana atakaa ndani yake ili awatoe huko waliko kuwarudisha kwenye nchi yao kaanani,Ukisoma biblia yoote hakuna mahala wana wa Israeli walijirudisha wenyewe! miongoni mwa hao waamuzi,na manabii ukiwatoa Mussa,Haruni,Joshua na Kalebu wanaopatikana kitabu cha waamuzi ni Shamgani (Waamuzi 3:31),Tola (waamuzi 10:1),Jair (10:3-5),Ibzan (12:8-10) Abdoni (12:13-15) na listi inaendelea hadiwatakuja akina Samsoni hapo na wengine weengi sana Mungu aliowainua.
Sasa nikirudi kwenye swali lako kuhusu waliko wayahudi halisi, jibu nikwamba Wametawanywa Duniani koote wapo katika kipindi cha Mapatilizo kama Yesu alivyowaambia kwenye kitabu cha Luka 21:20-25 baada ya kumkataa na kulikataa neno lake!,kama tu vipindi vyoote vile walivyokuwa wakiliasi neno la Mungu anawakabidhi kwenye mikono ya maadui zao! neno lake ni amini na kweli na halibadiriki ndugu yangu ni lile lile tangu enzi za Musa mpaka sasa,hawa waliopelekwa pale israeli kwa msaada wa Marekani na uingereza na wakaanzisha taifa lao 1948 wakajiita wao ni wayahudi,Mungu alilijua hili ndiomaana Yohana aliambiwa aseme hilo katika ufunuo 2:9 Kuwa hao wanaojiita yakuwa ni wayahudi na sio ni sinagogi la shetani! shetani kashawapeleka wale Fake pale kusudi wajiandae kumpokea Huyo masihi wao wanaemsubiri ambaye atakuwa ni mpinga kristo! wale original hawajarudi bado,ukisema hao waliopo hapo ndio wale wa zamani nabii nani kawarudisha pale?,lini walitubu ile dhambi yao ya Uasi wa kukataa neno la Mungu (Yesu)? okay kama Mungu ndio kawarudisha pale mbona hawakai kwa amani (vita kila siku) kama ilivyokuwa zamani akiwarudisha wanakaa kwa amani?
ukijiuliza hayo maswali utagundua nnachokimaanisha.
(2) Ni ushahidi gani unauotoa kudhihirisha kwamba wale wajakazi wa wake wa yakobo ambao Yakobo alizaa nao ni weusi kutoka kushi?
Ni simple assumption wayahudi hawakuwa wanachukuana vijakazi,i mean myahudi kuwa na kijakazi wa kiyahudi vijakazi wakipindi hicho walikuwa watu wa nje ya uyahudi wengi walikuwa wakush,Musa alioa mkushi hesabu 12:1,ukisoma hiyo thread yangu utagundua wayahudi wakipindikile walikuwa "people of colour" yaani watu wenye rangi nyeusi na Mungu aliweka ukoma juu yao namna ya kuutambua na namna ya kuutibu,hawakuwa wazungu,
(3) Biblia inaonyesha baada ya Yesu kupaa wanafunzi wake walikimbia uyahudi kuogopa kuuwawa na kukimbilia maeneo mbalimbali kama korintho,efeso, filipi,na maeneo mengi.
Na siku ya sabato walikuwa wakiingia kwenye masinagogi ya wayahudi kuhubiri habari za Yesu.
Je huko waliokuwa wayahudi ktk maeneo niliyotaja ndiyo huko ethiopia?
Ethiophia ni habari nyingine kabisa wale wayahudi wa ethiophia walikuwepo kule tangia enzi za Suleiman! kabla Yesu hajaja kufanya huduma duniani na hadi kaja wao walikuwepo kule kule ethiophia,yesu alivyopaa kwenda mbinguni wanafunzi wake walifanya huduma kwa muda wa miaka 40 hv sehemu mbalimbali za dunia ni mtume mmoja tu ndio alibaki kuhubiri Yerusalem wengine walitawanyika sehem mbali mbali za dunia,na baada ya yesu kuwajaza Roho mtakatifu wale mitume walipata sana ujasiri wa kulihubiri neno la Bwana kila kona wengi waliteswa na kuuawa kwaajiri ya jina lake kama Yesu alivyokuwa amewajulisha kabla.so walihubiri injili kila kona ya dunia sio tu hayo maeneo uliyoyataja hapo juu