Uhamiaji acheni siasa, mnafeli wapi?

Uhamiaji acheni siasa, mnafeli wapi?

Wadau, nimelileta hili maana limenivuruga akili haswa.

Ipo hivi: Niliingia tovuti ya Uhamiaji kwa ajili ya maombi ya passport ila mambo niliyokutana nayo huko yameniacha hoi na kunifanya niamini siasa siyo mchezo mzuri. Kero nilizoziona ni kama ifuatavyo:

1. Katika kujaza form kuna kipengele kimeniuliza dhumuni la safari na ninasafiri kwenda nchi gani. hapa najiuliza kila anayeomba passport ni lazima awe anasafiri au passport unatakiwa uwe nayo ili ikitokea unasafiri ndio unaomba Visa ya nchi husika.

2. Hiki ndo kituko zaidi, imagine kuna kipengele kinanielekeza uwezekano wa kuombwa uthibitisho wa tiketi ya kurudi, cheti cha kuzaliwa cha bibi.

Hivi mtu nina miaka 30 unaniambia kweli nilete cheti cha kuzaliwa cha bibi, nyie bibi zenu wana hivyo vyeti? Au ndiyo mwenye nguvu mpishe? Acheni kuweka siasa kwenye mambo yenye maslahi na maisha ya watu.

3. Ajabu ni kuwa utaratibu wa kuomba passport umewekwa uonekane ni lazima uwe unasafiri ndiyo uombe passport, lakini je, inapotokea mtu anatakiwa asafiri haraka iwezekanavyo kuna utaratibu wa uhamiaji kutoa passport haraka iwezekanavyo au ndo mtafuata taratibu zenu na kuharibu dili za watu?

4. Kwa sasa tuna vitambulisho vya taifa ambavyo kuvipata kuna mchakato mtu anapitia kama kuhakikiwa na uhamiaji wenyewe, amabapo wasio na vyeti vya kuzaliwa wamepeleka viapo na walipokidhi vigezo wakapatiwa NATIONAL ID, anapokuja mtu anataka passport jaribuni kurahisisha kwa huyu mwenye kitambulisho cha NIDA maana taratibu mnazotaka apitie tayari alizipitia wakati mnamthibitisha kuwa ni Mtanzania na mkampa go ahead kwenda NIDA kupata ID. Kiukweli uhamiaji nilijaribu kuona labda hata kun amahali inasema kwa Muombaji mwenywe kitambulisho cha taifa afuate hatua hizi, sikuona zaidi ya mahali tu mmeomba utambulisho wa taifa. Badilikeni muende na kasi ya technolojia sio kila siku mtu anarudia kufanya vitu vilevile, mbona tra, brela nk, hawana longolongo wanaomba tu namba ya NIDA basi mchezo umeisha.

There is no such a thing as a little freedom, either you are completely free or a total slave.

Ndio umejua leo mkuu? Tukisema hapa nyie sio ndio mnao tokwa na povu?
 
Malalamiko dhidi ya uhamiaji ni mengi sana, ajabu ni kwamba mamlaka zinazohusika zinaweka pamba masikioni.

Passport yangu kubwa ya zamani inakwisha muda wake mwishoni mwa mwezi huu, ila kila nikiwaza urasimu wao wa kupata passport mpya najikuta nakata tamaa kabla hata sijauanza.

Ni kwanini wenye passport kubwa za zamani asingetakiwa kuleta kitambulisho cha NIDA tu kupata passport mpya?

Taarifa za wateja wenu za mwanzo hamnazo kwenye kanzidata?

Sent using Jamii Forums mobile app

Halafu mkuu hizi passport wanazishusha hadhi kabisa, yaani sasa hivi unapokwenda unaambiwa nida lete

Hata ukiwa na passport ya kidigital hawaitaki, kwa maana hizi passport ni bogas au vipi?

Nchi za wenzetu passport ina nguvu pamoja na driving licences, ukiwa na driving licence inajitosheleza peke yake ikiwa bank au popote pale kwenye huduma
 
Inasikitisha,ilitakiwa uwe na ID tu ili kuomba passport mpya,sio takataka zingine(elewa huwezi pata ID kama huna viambatanishi vilivyopo kwenye passport)kabla ya nchi kuwekeza zaidi kwenye ID ambazo zimo ndani ya central data systems ya nchi sisi tunafanya siasa na mihemko.na kichekesho zaidi hizi ID zina ukomo!!ilitakiwa hii ID inakoma pale unapokuwa umekufa ndio maana wenzetu wanaziita ni Life book(card),unazaliwa nayo,unakua nayo,unasoma nayo,unafanya kazi nayo,unaishi nayo na unakufa nayo!!!.
 
Halafu mkuu hizi passport wanazishusha hadhi kabisa, yaani sasa hivi unapokwenda unaambiwa nida lete

Hata ukiwa na passport ya kidigital hawaitaki, kwa maana hizi passport ni bogas au vipi?

Nchi za wenzetu passport ina nguvu pamoja na driving licences, ukiwa na driving licence inajitosheleza peke yake ikiwa bank au popote pale kwenye huduma
Elewa hiyo driving licence ina ID number yako that why inajitosheleza,unapokwenda hospitalini na kutoa driving licence kama ndio utambulisho wako,wakiingiza ile ID number informations zako zote zinajitokeza,hapa kwetu bado sana.
 
Mkuu Affidavit oath ya mzazi sasa hivi wana national ID ambayo walitakiwa kuwa na hiyo Affidavit ili wakamilishe mchakato kupata ID, simple maths A=B, A=C, automatically B=C, kwa nini mtu arudie mchakato kupata Affidavit ya mzazi wakati mzazi aliapa kupata NIDA ID, why wasiweke kipengere kama mzazi ana NIDA ID basi ijazwe tu namba maana wao na NIDA sin watoto wa nyumba moja.
Well said mkuu. Umenena vema kabisa
 
Back
Top Bottom