Uhamiaji Arusha kuambiwa na Makonda watoe pasipoti kwa siku saba: Tuna tatizo la siasa nchi hii…

Uhamiaji Arusha kuambiwa na Makonda watoe pasipoti kwa siku saba: Tuna tatizo la siasa nchi hii…

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Kweli tunaweza kuwa na wakuu wa mikoa wasiojua pasipoti zinaprintiwa wapi?

Au tunajua lakini tunafanya kick za kisiasa? Kwamba leo Mnataka kutuaminisha kwamba Ofisi ya Uhamiaji Arusha inatoa pasipoti? Toka lini?

Hii kick tumeikataa kweupe kabisa tutafute kick nyingine.
Lakini pia tujiulize uhusiano kati ya pasipoti ya watanzania na utalii je kuna Sehemu hivi vitu vinaingiliana?

Wageni wanakuja na pasipoti zao kutoka nje mkuu wa mkoa anataka kuunganisha utoaji wa pasipoti na kuongezeka kwa watalii...

Mwisho, unapojadili pasipoti tumeona Kagera wakiambiwa ni mkoa wa mpakani na sisi wenyeji wa huko tunafuatiliwa sana kufahamu asili yetu jambo ambalo nakubaliana na uhamiaji.

Je, Arusha ambapo kila siku wanakamatwa wasomali na waethiopia tunataka kufanya pasiwe siyo mkoa wa mpakani? Kama mkipunguza ukaguzi huko ondoeni na ukaguzi kwetu Kagera na huko Kigoma.

Uhamiaji mkiendelea kukimbizwa na siasa kesho hao hao wanasiasa watakuja kuwatuhumu mmetoa pasipoti kwa masai wa Kenya, kwa Wasomali na waethiopia. Tuache usalama ubaki kuwa suala la ndani ya nchi kama waasisi wa taifa letu walipoamua kuliweka.

Pasipoti ya Uhamiaji imewekwa siku kumi na nne kwa sababu unaomba mkoani, maombi yanatumwa DAR wa salaam then wanakurudishia pasipoti yako kwa posta.

Na tukumbuke huko DAR awashughulikii maombi ya Arusha wanashughulikia maombi ya nchi nzima. Leo kila mkuu wa mkoa akitaka pasipoti za watu wake zitoke anavyojisikia sisi tuliopo Mwanza ambapo Mzee Mtanda ajatusemea tutapata pasipoti?

Taasisi za umma lazima ziwe na service charter ambayo imefanyiwa utafiti siyo kila mtu anajiwekea muda wake.............Makonda anaweza akawa na nia njema lakini namsihi mambo ya security ajaribu kwanza kushauriana na hao wahusika kabla ya kwenda viral.

Huko Ulaya kwenyewe hakunaga siasa kwenye pasipoti. Afrika yetu fundisheni viongozi.
 
Kweli tunaweza kuwa na wakuu wa mikoa wasiojua pasipoti zinaprintiwa wapi?

Au tunajua lakini tunafanya kick za kisiasa? Kwamba leo Mnataka kutuaminisha kwamba Ofisi ya Uhamiaji Arusha inatoa pasipoti? Toka lini?
Hiyo ndiyo Afrika, Tanzania, CCM na Samia, na siasa za kihalifu za Makonda. Mtu kama huyu eti anapewe ukuu wa mkoa baada ya kuvurunda kwingineko, hivi huwa ni nani anashinikiza watu kama akina Makonda wenye sifa mbovu za uongozi na kukataliwa na jumuiya ya kimataifa wawe viongozi tena mahali kama Arusha penye Jumuiya ya Africa Mashariki na Jumuiya nyingi nyingine za Africa? Wananchi tuikatae CCM kwa nguvu zetu hii ni dharau kubwa kwa watanzania.
 
Huyu kijana anapaswa ajipange haswa, maana huo mkoa alio pangiwa nikama raia walikua wanataka RC wanae mtaka wao, ama wanataka RC wanae mzidi kwa power....😜
 
Hiyo ndiyo Afrika, Tanzania, CCM na Samia, na siasa za kihalifu za Makonda. Mtu kama huyu eti anapewe ukuu wa mkoa baada ya kuvurunda kwingineko, hivi huwa ni nani anashinikiza...
Sema hiyo ni dharau kubwa kwa wana Arusha, usitujumlishe waTanzania...😜
 
Passport inachukua muda gani mpaka kuipata mimi sina uzoefu!
Mimi nimefuatilia pasipoti za wanangu kwa kipindi tofauti, moja nikiwa ubalozini na tatu nikiwa Mwanza
Kwa ubalozini lazima taarifa zako zitumwe Tanzania kwa ajili ya kuprintiwa paspoti na inachukua mwezi + hadi uipate huko nje

Mwanza kwa uzoefu nilionao nilitumia 15 hadi ishirini na moja japo watoto kwenye maombi baada ya kujaza online ilinichukua lisaa kimoja wakawa wamepigwa picha. Baada ya picha nakulipia 130,000 wanavyodai na nilivyoambiwa maombi lazima yatumwe huko DSM kwa posta ndipo pasipoti itolewe na ikikamilika irudishwe Mwanza uende ukachukue

Hasa hapa najiuliza Makonda atatumia mbinu gani kutekelezeka kwa agizo lake kama mikoa yote nchini pasipoti zinaprintiwa DAR ?

Na kama pasipoti za Arusha zikitumia siku saba je sisi wa mikoa mingine hatutaruhusiwa kuhudumiwa au watarpprint kwa sababu Makonda kasema?

Kama Kagera na Kigoma wanasema ni mkoa wa Mpakani kwanini Arusha na kwenyewe pasiwepo na taadhari ya kiusalama kama wanavyojiwa ndugu zetu huku?

Lakini pia taasisi zinazotoa huduma lazima ziwe na mkataba wa huduma kwa mteja; mkataba wa huduma kwa mteja wa uhamiaji unasemaje? Kama mkataba huo unasema siku kumi na nne ni utafiti gani umefanyika kushusha siku hadi 7? Je hizi saba zinaendana na hali halisi ilivyo ya usafirishaji wa pasipoti?

Najadili hii hoja kama great thinker kusaidia policy za nchi kubadilika siyo kwa kusukumwa na mtu mmoja bali kusukumwa na utafiti.
 
Makonda anakitu sema chuki uliyonayo kwa makonda hata akiongea kitu gani huwezi kumuelewa.
Mimi nataka nione nani atakae ibuka kidedea kati ya wafanya biashara, utalii, chugareee, wadudu, upinzani/ngome dhidi ya RC Makonda...🤣🤣
 
Hahaha mkolomije kaingia chuga
Vp bado hajafika kwa mromboo?
Makonda kama tunakumbuka alikwenda Tunduma akawatangazia Madereva wote kwamba mama ameelekeza wapewe pasipoti bure......tuwaulizeni Madereva kama wanapata pasipoti bure.

Hakuna Dreva anapewa pasipoti bure : tunafanya haya kufungua mijadala ya yale yanayotekelezeka na yasiyotejelezeka
 
Kweli tunaweza kuwa na wakuu wa mikoa wasiojua pasipoti zinaprintiwa wapi?

Au tunajua lakini tunafanya kick za kisiasa? Kwamba leo Mnataka kutuaminisha kwamba Ofisi ya Uhamiaji Arusha inatoa pasipoti? Toka lini?
Inashangaza mtu kateuliwa mkuu wa mkoa lakini hafahamu majukumu yake na mipaka ya maagizo. Nchi ngumu sana hii.
 
Mimi nimefuatilia pasipoti za wanangu kwa kipindi tofauti, moja nikiwa ubalozini na tatu nikiwa Mwanza
Kwa ubalozini lazima taarifa zako zitumwe Tanzania kwa ajili ya kuprintiwa paspoti na inachukua mwezi + hadi uipate huko nje

Mwanza kwa uzoefu nilionao nilitumia 15 hadi ishirini na moja japo watoto kwenye maombi baada ya kujaza online ilinichukua lisaa kimoja wakawa wamepigwa picha. Baada ya picha nakulipia 130,000 wanavyodai na nilivyoambiwa maombi lazima yatumwe huko DSM kwa posta ndipo pasipoti itolewe na ikikamilika irudishwe Mwanza uende ukachukue
Labda katumwa na mama usishangae kesho akiwa waziri wa mambo ya ndani uhamiaji zote zinakua chini yake na passport tunapata kwa siku mbili!
 
makonda hana shida ila kuna watu wanakinyongo nae sana ingekuwa vzuri zaidi hata paspot zitolewe hata baada ya siku mbili mambo yaende chapu chapu ila kwa kufata utaratibu...mtoa maada kwani dar ndo nn hicho kitu inatakiwa kinamalizika mkoani
 
Back
Top Bottom