Kweli tunaweza kuwa na wakuu wa mikoa wasiojua pasipoti zinaprintiwa wapi?
Au tunajua lakini tunafanya kick za kisiasa? Kwamba leo Mnataka kutuaminisha kwamba Ofisi ya Uhamiaji Arusha inatoa pasipoti? Toka lini?
Hii kick tumeikataa kweupe kabisa tutafute kick nyingine.
Lakini pia tujiulize uhusiano kati ya pasipoti ya watanzania na utalii je kuna Sehemu hivi vitu vinaingiliana?
Wageni wanakuja na pasipoti zao kutoka nje mkuu wa mkoa anataka kuunganisha utoaji wa pasipoti na kuongezeka kwa watalii...
Mwisho, unapojadili pasipoti tumeona Kagera wakiambiwa ni mkoa wa mpakani na sisi wenyeji wa huko tunafuatiliwa sana kufahamu asili yetu jambo ambalo nakubaliana na uhamiaji.
Je, Arusha ambapo kila siku wanakamatwa wasomali na waethiopia tunataka kufanya pasiwe siyo mkoa wa mpakani? Kama mkipunguza ukaguzi huko ondoeni na ukaguzi kwetu Kagera na huko Kigoma.
Uhamiaji mkiendelea kukimbizwa na siasa kesho hao hao wanasiasa watakuja kuwatuhumu mmetoa pasipoti kwa masai wa Kenya, kwa Wasomali na waethiopia. Tuache usalama ubaki kuwa suala la ndani ya nchi kama waasisi wa taifa letu walipoamua kuliweka.
Pasipoti ya Uhamiaji imewekwa siku kumi na nne kwa sababu unaomba mkoani, maombi yanatumwa DAR wa salaam then wanakurudishia pasipoti yako kwa posta.
Na tukumbuke huko DAR awashughulikii maombi ya Arusha wanashughulikia maombi ya nchi nzima. Leo kila mkuu wa mkoa akitaka pasipoti za watu wake zitoke anavyojisikia sisi tuliopo Mwanza ambapo Mzee Mtanda ajatusemea tutapata pasipoti?
Taasisi za umma lazima ziwe na service charter ambayo imefanyiwa utafiti siyo kila mtu anajiwekea muda wake.............Makonda anaweza akawa na nia njema lakini namsihi mambo ya security ajaribu kwanza kushauriana na hao wahusika kabla ya kwenda viral.
Huko Ulaya kwenyewe hakunaga siasa kwenye pasipoti. Afrika yetu fundisheni viongozi.