Uhamiaji kukagua akaunti za kijamii za watalii, wasafiri wanaoomba visa au kupitia vituo vya mpakani

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
32,522
Reaction score
37,398
Mamlaka za Uhamiaji yaanza kutekeleza sheria ya kuoneshwa akaunti za Mitandao ya Kijamii ya ya wanaoingia nchini kama watembezi au kazi, wanafunzi n.k :

Ili kutii Agizo tamko la Januari 2025 14161 (Kulinda Marekani dhidi ya Magaidi wa Kigeni na Vitisho Vingine vya Usalama wa Kitaifa na Usalama wa Umma), CBP inaongeza mitandao ya kijamii kama kipengele cha lazima cha data kwa ombi la ESTA

Mandatory Social Media: CBP is adding social media as a mandatory data element for an ESTA application. The data element will require ESTA applicants to provide their social media from the last 5 years.

3. Mitandao ya Kijamii ya Lazima: Ili kutii Agizo Kuu la Januari 2025 14161 , CBP inaongeza mitandao ya kijamii kama kipengele cha lazima cha data kwa ajili ya ombi la ESTA. Kipengele cha data kitahitaji waombaji wa ESTA kutoa mitandao yao ya kijamii kutoka miaka 5 iliyopita.

4. Vipengee vya Data nyeti : Ili kutii EO (Agizo) la Januari 2025 (14161), na Aprili 4, 2025, Mkataba wa Kusasisha (up dating) Fomu Zote za Kukusanya Data ya Msingi ya Wasifu, CBP itaongeza "sehemu za data za thamani ya juu yaani taarifa siri nyeti binafsi" kwenye programu ya ESTA, inapowezekana. Hii ni pamoja na maelezo ambayo tayari yamekusanywa katika programu ya ESTA.

Aina za data za unyeti wa hali ya juu uhamiaji watakazo omba ni pamoja na:

a. Nambari za simu zilizotumika katika miaka mitano iliyopita;

b. Anwani za barua pepe zilizotumiwa katika miaka kumi iliyopita;

c. Anwani za IP na metadata kutoka kwa picha zilizowasilishwa kwa njia ya kielektroniki;

d. Majina ya wanachama wa familia (wazazi, mke, ndugu, watoto);

e. Nambari za simu za familia zilizotumiwa katika miaka mitano iliyopita;

f. Tarehe za kuzaliwa za mwanachama wa familia;

g. mahali pa kuzaliwa kwa washiriki wa familia;

h. Makaazi ya wanafamilia;

i. Biometriska - uso, alama za vidole, DNA, na iris;

j. Nambari za simu za biashara zilizotumika katika miaka mitano iliyopita;

k. Anwani za barua pepe za biashara zilizotumiwa katika miaka kumi iliyopita.

Hii ni kuangalia comments, uzi / thread, emojis, mirengo, misimamo inayotishia usalama wa nchi.

Mamlaka za Uhamiaji zinasema kupitia mitandao na majukwaa mbalimbali maofisa wa uhamiaji wanaweza kujua haiba, ndoto na matukio yanayoweza kufanywa na wageni kabla ya kuingia ndani ya nchi ktk border post za viwaja vya ndege, border ya mipakani ardhini na bandari mbalimbali.

SOMA KWA KINA : Source : Federal Register :: Request Access

.NB

Je mataifa mengine mengi yataiga utaratibu huo wa lazima ya wageni kuonesha akaunti zao za kijamii, simu zao n.k
 
Kichwa Cha habari mbona kimekaa kishari Shari ..ungemalizia uhamiaji marekani ..

Uhamiaji Tanzania, Wataigiza kwa diaspora, wenyeji na wageni watakaoingia nchini kwetu. Hili lina uhakika, lakini litalenga watanzania wa nasaba zote wanaorudi nyumbani kusalimia au shughuli zingine za kijamii kwao Tanzania.
 
Mamlaka za Uhamiaji yaanza kutekeleza sheria ya kuoneshwa akaunti za Mitandao ya Kijamii ya ya wanaoingia nchini kama watembezi au kazi, wanafunzi n.k :

Ili kutii Agizo tamko la Januari 2025 14161 (Kulinda Marekani dhidi ya Magaidi wa Kigeni na Vitisho Vingine vya Usalama wa Kitaifa na Usalama wa Umma), CBP inaongeza mitandao ya kijamii kama kipengele cha lazima cha data kwa ombi la ESTA

Source : Federal Register :: Request Access

Mandatory Social Media: CBP is adding social media as a mandatory data element for an ESTA application. The data element will require ESTA applicants to provide their social media from the last 5 years.

Hii ni kuangalia comments, uzi / thread, emojis, mirengo, misimamo inayotishia usalama wa nchi.

Mamlaka za Uhamiaji zinasema kupitia mitandao na majukwaa mbalimbali maofisa wa uhamiaji wanaweza kujua haiba, ndoto na matukio yanayoweza kufanywa na wageni kabla ya kuingia ndani ya nchi ktk border post za viwaja vya ndege, border ya mipakani ardhini na bandari mbalimbali.

.NB

Je mataifa mengine mengi yataiga utaratibu huo wa lazima ya wageni kuonesha akaunti zao za kijamii, simu zao n.k
Hii ni kwa Marekani ila najua CCM na serikali zake watapita humo humo. Hata ukifika Mbezi pale kutokea kijijini kwenu watataka kukagua simu yako.
 
Hivi hawa watawala wakijua namba yako ya simu, wakawa na access ya kujua tovuti na mitandao unayoingia kupitia kwa ISP wako, wana uwezo wa kutambua post zako za JF au wataona tu nyuzi ulizoingia?

Siulizi hivi kwa kuwa naogopa ila nataka tu kujua.

Swali zuri sana la msingi.

Kwa sasa kabla hawajaigiza umahiri wa taifa hilo kuu, Tanzania na nchi zingine zenye udikteta uchwara wanatumia haya yafuatayo kugandamiza raia wake:

Pia kwa nyongeza kujiwezesha kiufahamu, Ili kusadiki baadhi ya masuala yaliyomo katika kitabu cha Eric Kabendera kuwa siyo riwaya ya kusadikika, kuna ukweli kwa vithibitisho, basi msikilize mwalimu huyu :

Jinsi mitandao ya simu inavyotumiwa na wasiojulikana kufuatilia nyendo za watu:

Jinsi ya Kuepuka Kutekwa nyara na watu wasiojulikana ambao pia hawajulikani na 'Serikali Nzima' - ​

View: https://m.youtube.com/watch?v=inj9f4BUxVw
Kifaa chako cha kieletroniki kinavyoweza kuwasaidia watu wasiojulikana kukufuatilia kwa njia zifuatazo :
  • Trailing and surveillance
  • Triangulation
  • SIM CARD
  • IMEI
  • LUKU malipo ya umeme kujua makazi
  • APPS za mikopo kuruhusu kufahamu contacts /picha / mikopo chechefu unayodaiwa kama ipo n.k
  • Hacking Software
  • Text msg
  • Dating sites
  • SIMU kuwa ya moto bila kuitumia
  • Microphone ya simu
  • Camera ya simu kuchukua mazingira uliyopo
  • Hata simu za kiswaswadu si salama
  • N.k
 
Kama jina lako la kwenye no. ya Simu ni tofauti na La JF hawawezi kujua.

Lkn Vile vile, Iwe hyo no. Yako ya simu hawajaitoa humu JF 🤣
 
Swali zuri sana la msingi.

Kwa sasa kabla hawajaigiza umahiri wa taifa hilo kuu, Tanzania na nchi zingine zenye udikteta uchwara wanatumia haya yafuatayo kugandamiza raia wake:

Pia kwa nyongeza kujiwezesha kiufahamu, Ili kusadiki baadhi ya masuala yaliyomo katika kitabu cha Eric Kabendera kuwa siyo riwaya ya kusadikika, kuna ukweli kwa vithibitisho, basi msikilize mwalimu huyu :

Jinsi mitandao ya simu inavyotumiwa na wasiojulikana kufuatilia nyendo za watu:

Jinsi ya Kuepuka Kutekwa nyara na watu wasiojulikana ambao pia hawajulikani na 'Serikali Nzima' - ​

View: https://m.youtube.com/watch?v=inj9f4BUxVw
Kifaa chako cha kieletroniki kinavyoweza kuwasaidia watu wasiojulikana kukufuatilia kwa njia zifuatazo :
  • Trailing and surveillance
  • Triangulation
  • SIM CARD
  • IMEI
  • LUKU malipo ya umeme kujua makazi
  • APPS za mikopo kuruhusu kufahamu contacts /picha / mikopo chechefu unayodaiwa kama ipo n.k
  • Hacking Software
  • Text msg
  • Dating sites
  • SIMU kuwa ya moto bila kuitumia
  • Microphone ya simu
  • Camera ya simu kuchukua mazingira uliyopo
  • Hata simu za kiswaswadu si salama
  • N.k

Hiyo ya LUKU nimewahi kuiwaza na kuigusia humu. Ni njia rahisi sana ya kumdaka mtu.

Wengine tayari tunajua tunajulikana vizuri tu ila tumeamua tuishi maisha huru na tuseme chochote tunachowaza bila kumjali huyo "big brother".
 
Ila ISP wana uwezo wa kujua website zote unazoingia.

ISP ni internent Service Provider Mfano Mitandao ya Simu Tunayo tumia, Hawa wanauwezo wa kuina websites ulizo tembelea na data ulizo Tumia.

Mfano: Watajua umeingia JF, lkn hawawezi kujua umeandika wala kusoma nn, Sawa sawa na FB, Google and the like ni kama browsing history tu.

Swala la kuipa serikali hizo taarifa, Ni mpaka kuwe na legal request, Au kibongo bongo ni simu moja tu ya mkubwa wanapewa, lkn mpaka wanafika huko basi umeandika very sensitive issues kama kabendera, Azory gwanda and the like.
 
Nadhani ISP wanaona exact link uliyoingia siyo tu jina la website kwa maana hiyo wanaona uzi ulioingia. Labda wasichoweza kujua ni kama umesoma tu uzi, umeuanzisha au kuchangia ila wakifanya data analysis wanaweza kujua.

Kama ulivyosema, kwa Tanzania ambapo serikali ina unlimited powers, hakuna mtu au taasisi inayeweza kuwazuia kupata hizo data kutoka kwa ISP bila hata kuwa na warrant.

Huko FB na IG ni tofauti kidogo ingawa napo siyo pagumu kama wakiamua kutengeneza profile yako.
 
Hii ni kwa Marekani ila najua CCM na serikali zake watapita humo humo. Hata ukifika Mbezi pale kutokea kijijini kwenu watataka kukagua simu yako.
Hawana uhalali wa kukagua simu ya mtu. Hata USA kwenyewe wanakotaka uorodheshe account zako za social media, hawakagui simu bali unawapa username tu wanaona unachopost au ulichopost.
 
Hii ni sahihi.

Na nilazima watu wajue, Jumbe tunazopost kwenye mitandao ni public information sio Privacy info kama SMS tunazo chart na wake zetu.
 
Hawana uhalali wa kukagua simu ya mtu. Hata USA kwenyewe wanakotaka uorodheshe account zako za social media, hawakagui simu bali unawapa username tu wanaona unachopost au ulichopost.

Hii ni sahihi.

Na nilazima watu wajue, Jumbe tunazopost kwenye mitandao sio public information sio Privacy info kama SMS tunazo chart na wake zetu.
Lakini mkumbuke Marekani wanakagua kujua mitazamo yako kuhusiana na taifa lao.

Kwa hiyo tunaposema CCM na serikali zake zitapita humo humo tunamaanisha hata ukiwa "critical" kwa mauaji ya MO29 watakuwa na haki ya kukuchukulia hatua au kukunyima huduma fulani.
 
Na sisi tuweke vigezo kama umefollow au like post za Mange Kimambi, Larry Madowo hamna kuingia 😏
 
Back
Top Bottom