Hapana mkuu njia halali ya kwenda Marekani bado ipo na itakuwa wazi.
Wakati wa utawala wa Trump (2016-2020) nilikwenda States mara kadhaa na ni kweli wale maofisa uhamiaji walikuwa "hostile" kwa wageni khasa weusi.
Lakini ukiwa uko sawa hakuna shida kwani hata sasa waweza kuingia na GC yako bila shida ukumbuke tu kuirekebisha kama yakaribia kuisha muda wake (hutakiwi kuwa nje ya Marekani kwa zaidi ya mwaka mmoja).
Trump shida yake amesema wazi ni wahamiaji waso na vibali halali vya ukaazi.
Na amesema atamalizia ule ukuta mrefu kuzuia uingiaji haau nchini humo.