Uhamiaji Musoma, huyu mama kutoka Burundi angefariki damu yake ingewalilia

Uhamiaji wakipanda kwenye gari kukagua utadhani wanalipwa mamilioni ya shilingi, shati zenyewe zimepauka kama nini.

Wengi lugha zao zq vijijini unaona kabisq huyu JKT ndio ilimleta mjini
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sasa hivi kwenye vizuizi vyao wanakuuliza vitambulisho tushazoea hayo mambo ugenini eti na nyumbani unakolomewa wakati wenzetu raia wao wanawajua wanawauliza wageni bongo shida sana kweli...
Ulishawahi kwenda nchi gani ambayo ni homogeneous kiasi watu wote wanafanana.
.
Ukisafiri kwenda Zambia huuliza raia wao reg kifupi inaitwa National registration card usipokuwa nayo kisanga.

Malawi pia ni vile vile ila ya Malawi inaitwa National card.

Rwanda na Uganda pia ni hivyo hivyo.

Zimbabwe ndio kabisa.

Je afrika kusini hawahoji?

Australia ya kwao inaitwa Australia border forces unajua wanafanyaje kwa raia wao kumbuka hili ni bara nchi lililozungukwa na maji pande zote.

Marekani Wana social security card ambayo inayo taarifa zote ili kuzuia wahamiaji Toka kusini mwa Amerika na mexico.

Tanzania nayo sio kisiwa inabidi iwe na some formulation, ili iweze kuregulate. Wageni wanaoingia na kuishi Tanzania.

Tanzania ni nchi yenye jamii za kibantu, kinilotiki, kikushi, watu pori ambao hao watu wapo pia katika Mataifa mengine waliyopakana nayo.

Embu bwana great thinker nambie unamtofautishaje mkimbu wa Tabora na Mfulero wa Kongo kwa kuwaaangalia tu.

Hivyo lazima wahoji.

Mimi dereva wa Lori kwa hiyo nishazoea kukutania nao na huwa natoa ushirikiano.
 
Nakazia

Mungu amlaani hicho kibarua chake kisimpe manufaa yoyote kutokana unyama aliofanya, vijana wa hovyo hivyo roho mbaya wengine mimba ziliingia wazazi wao wakiwa disco au vilabu vya pombe za kienyeji
 
hakuna uhamiaji wasumbufu kama wa tz ,nimegundua hilo wakuu sijui wanamatatizo gani .sasa huyo mama serious she is not a threat to the nation, kwanin umhangaishe .doesn't make any sense .

very inhumane and barbaric shame on them.
Ushawahi pita boda za Burundi??? Wajinga sana wale jamaa
 
Kama hakuwa na nyaraka na inapaswa uwe na Nyaraka kuingia Tanzania basi huyo ni mkosaji/mhalifu.
 
Nakazia

Mungu amlaani hicho kibarua chake kisimpe manufaa yoyote kutokana unyama aliofanya, vijana wa hovyo hivyo roho mbaya wengine mimba ziliingia wazazi wao wakiwa disco au vilabu vya pombe za kienyeji
Mungu amuongezee nguvu huko alipo
 
Unauliza vitu gani Mkuu Malawi hapo wageni ndio mtatoa vitambulisho wenyeji ndio wanatoa ID kama hana sio ishu ya kushushana kwenye gari hakuna Nchi Raia anashushwa na udereva wako wa Roli umeona wapi..?hapo Longido mwanafunzi alitaka kushushwa mpaka abiria wakapiga kelele
 
Sijakuelewa mwanafyale I'd na vitambulishio vina tofauti gani
 
Sijakuelewa mwanafyale I'd na vitambulishio vina tofauti gani
Nimeongea kitu kimoja haraka...Zambia,Malawi,Botswana,Zim kote huko mwenyeji akionyesha kitambulisho kwenye bus la local kapenda maana yapo maswali kujua huyu raia au mgeni labda hiyo fani sio ya kwako...
 
Kuna siku Sasa tunavuka Mtera ...wale Uhamiaji ... Yaaani mi kimsingi ni Afisa Mkuu (Principal officer)..... Kilichafuka ... Nimeajiriwa kijana nikiwa na miaka22 2010... Sasa wengi hawaaminigi cheo changu ....
 
Ukweli ni kwamba waTz walio wengi wana roho mbaya sana, sasa hivi watu hawajali tena hata utu! Huwa inanisikitisha sana [emoji22]
 
Nimeongea kitu kimoja haraka...Zambia,Malawi,Botswana,Zim kote huko mwenyeji akionyesha kitambulisho kwenye bus la local kapenda maana yapo maswali kujua huyu raia au mgeni labda hiyo fani sio ya kwako...
Nimekutajia kwamba Zambia wanaita reg kwa kifupi, na raia wa Zambia hukitoa na kuonyesha maafisa wao wanapotaka kuvuka mageti Yao.

Abiria wote hushuka ndani ya basi, na mmoja mmoja hukaguriwa na asiye kuwa nacho ana kisanga
Kwa Zambia mpaka wakomfirm kwa local chief wako tayari basi lishakuacha na muda huo upo immigration detention zao.

Hayo maswali yanatumika sana Afrika ya Mashariki kwa sababu ya asili yetu na vitambulishio vimechelewa.

Malawi ni vivyo vivyo tofauti Malawi kidogo Wana afadhali kwenye ukali, ila baada ya maswali hutaona raia wao wametoa.

Sijui unapinga nini?
 
Kuna siku Sasa tunavuka Mtera ...wale Uhamiaji ... Yaaani mi kimsingi ni Afisa Mkuu (Principal officer)..... Kilichafuka ... Nimeajiriwa kijana nikiwa na miaka22 2010... Sasa wengi hawaaminigi cheo changu ....
Mh ndio cheo Gani hiki
 
Zambia ndio Nchi inayoongoza kwa sheria kali kwa wageni ila sio kuwashusha raia akiwa hana reg atashushwa mgeni kama hana kitambulisho wao wanauliza maswali tuu ili kuthibitisha kama raia kweli Wazambia wanathanini sana raia wao na wanawaamini raia wao wakiongea ni wakweli...nimeshinda sana kamwala market na sasa wameamia Comesa kwenye soko la wageni na tuna vijana bado wana maduka hapo na nyumba za kupangisha..SA si wanakamata sana wasio na passport ila raia hata asiwe na chochote akijitambulisha tuu na wao wanajua aguswi...hiyo ya geti kushushwa haipo afisa uhamiaji anaingia ndani ya bus kwa alie na mashaka nae ndie anashuka sio wote mshuke chini mpande kwa kitambulisho Wazambia ni watu wabishi hawawezi kufanyiwa hivyo hasa bara bara ya Nakonde mpaka Livingstone au Chirundu boarder...
 
Unapandaga gari za wapi kwenda Lusaka, maana wanakagua mpaka mizigo na hii ni tofauti na kwetu Tanzania mpaka wapate taarifa.
soko la Comesa hufanya ukaguzi mara kwa mara uwe na pasipoti usiwe nao wanakudaka, wamasai ndio wanakoma.
comesa hawajaanza leo na ukaguzi wa Zambia mnashuka wote ndio wanakagua mmoja mmoja mmoja , nina vijamna wengi hapo Zambia kuanzia Chisato, Isoka,chinsali,Mpika, mkushi , chilanga,kafue mpaka chilundu achilia mbali hapo Livingstone na Lusaka na Chilundu border.
hivyo najua ninachosema halafu Zambia haishindi sheria kali Australia immigration
Tuludi kwenye hoja ya msingi jamaa humu anasema immigration hawapaswi kumuhoji mtu eti kisa Watanzania wanafahamiaka ndio nikamjibu hii nchi sio homogeneous country hivyo wana haki ya kuhoji ili kuthibitisha akitlea mfano wa afisa Takukuru, unaonekana umesafiri sana je hii ni sawa, Zambia kama case study hapa ni nchi yenye sheria ngumu za immigration je wazambia wangemchukulia sheria gani pia kumbulka Zambia immigration wana detention zao.
Je wasipohoji watajuaje huyu ni raia na huyu sie,

Je mama mjamzito nana haki ya kuvunja sheria, kwa maelezo yao na sympath zilizopo humu, unafikiri afisa alitenda sasawa
anasema alitekelezwa je ana ushahidi?
Mhamiaji haramu lakini hatuna ushahidi wa status yake kwamba ni kweli au hapana , kisa ana matatizo haachwe
Nijibu Mwanafyale
 
Kuongezea tu Zambia reg yao wanaipata kwa kuanzia kwa chifu hivyo unapoulizwa chifu wako ni nani lazima uwe na jibu iwapo umepoteza pasipoti na muda mwingine wana confirm
 
Mkuu mbona unazunguka tupo Afrika kwenye Nchi za Sadc umehamia Australia tena zipo Nchi nyingi kwa sisi wasafiri tumekutana nazo hasa Singapore na Hong kong...Sidney hawanfanyii interview mmarekani ila Singapore walivyo watata hata mmarekani wasipomuelewa anadunda tuu kuingia kwao...Comesa na kamwala pana mgogoro ambao wazambia hawataki wageni wauze kwa sisi Wanyaki kuwa na wadogo ambao ni raia wa Zambia kwa kuwa wameishi sana kule ni kawaida tuu ndio maana naongea kitu nachokijua maana nimeishi kabwata na Matero mimi mwenyewe napopita na gari ni mwendo wa kinyanja tuu tena gari zinakua na namba GP wakitaka documents ni za gari wale ukiongea lugha yao hawana shida kabisa na wewe au uongee kiingereza kilichonyooka...
 
Labda ninyi mnaoongea Kinyanja au kichewa. ina maana umefoji pia reg maana ndio niliambiwa nifanye ili nibaki salama ila jamaa ni wasumbufu sijapata ona.
kuhusu comesa Tanzania tulishajitoa ila watanzania bado wanafaidika
kuhusu kuzunguka nilitoa mifano mbalimbali kutoka nchi tofauti tofauti.
hivyo sio jambo la ajabu kuulizwa na kuhojiwa kuhusu uraia wako kama jamaa wanavyoema as if ni kitu kisichotakiwa.
kama wewe ni mnyaki na unafanya biashara Zambia maana yake mzigo unachukua Dar hivyo inyala immigration check point unaifahamu, jamaa wanakagua kichwa kwa kichwa. je kuna watu huwa wanalalamika.
point yangu ni nini, sio jambo la ajbu duniani kukaguliwa na kuulizwa maswali
Mpaka sasa hapa ninapotumia Jf nipo Mbala nchini Zambia
 
Wewe Mkuu mbona mgumu kuelewa nifoji reg ili iweje nipo kama Mtanzania nafanya shughuli zangu Tanzania,SA na Zambia kidogo mambo ya kufoji documents ilikua miaka ya 2000 huko unachukua uraia wa SA kwa ajili ya kupata kazi na mambo mengine wengine walikua wanachukua ukimbizi wa Pemba ili wapate permit za kazi au Rwanda humu kwingine hakuna mambo hayo na mambo yanakwenda kwa sasa hivi hii passport mpya huwezi kufanya chochote ndio mwisho wa matatizo...mimi mambo ya safari siwazi nimeanza mapema mno...Nishawahi ingia Angola na passport ya Malawi nikitokea SA ili nikauze vitu enzi hizo kupata visa yao ilikua inasumbua mno kwetu ila Wamalawi walikua wanapeta leo hii kuniulizia cheki point unanishangaza...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…