Ukisikia roho mbaya za kichawi ndo hizi, ndo maana wabongo wengi hata passport hawana sababu ya kuogopa safari. Mbongo yeyote aliyesafiri akavuka mipaka ya Tanzania hawezi kuja kuchoma watu wanaopambana kutafuta maisha.
Hivi mu Ethiopia akilala Mbagala wiki moja huku akichangia kipato gesti na vyakula mchana usiku, baadae akapanda basi au ndege kuelekea South Africa wewe na umaskini wako unapungukiwa nini?,au nini kinaongezeka kwenye maisha yako!?
Wakikamatwa wakatozwa hela wakaruhusiwa kwenda mbele kwenye akaunti yako zinaongezeka shilingi ngapi!? Mambo mengine jifunzeni kuwa mnayaona na kukausha, hao wa Ethiopia hawajachagua kukimbia nchi yao, ni hali ngumu ya maisha.
Nyie ndo kipindi cha utumwa mlikuwa mnawaonesha waarabu, Babu zetu walipojificha kwa malipo ya slice za mikate. Mpumbavu kabisa mleta mada huna akili, na nahisi unakula na kulala kwa shemeji.