Uhamiaji Tanzania badilikeni

Uhamiaji Tanzania badilikeni

SN.BARRY

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2012
Posts
4,038
Reaction score
8,929
1. Kazi yenu ni kutoa passport sio kujua mtu anaenda wapi. Passport ni haki ya kila mtu. Jifunzeni kutoka nchi nyingine.

2. Sasa hivi Tanzania ajira hamna. Mnanyima watu passport maana yake wafe na njaa wakiwa Tanzania. Jifunzeni kwa nchi jirani. Kenya, Uganda hata Rwanda raia wao wanafanya kazi nchi mbalimbali kama Dubai, Qatar, Canada, South Africa, Botswana, Namibia, Ubelgiji, Norway n.k Nyie mmekuwa mwiba kwa watanzania.

3. Sio kila recruitment agency inayopeleka watu kufanya kazi Ulaya, America na Asia ni matapeli. Acheni kukariri. Dunia ya leo huwezi kupata kazi nje ya nchi bila kutumia agent. Badilikeni. Kila kampuni mnaita matapeli hivi hamuwezi kutrace kujua uhalali wa kampuni? Jiongezeni.

4. Mnapenda sana makamera kudhalilisha watu wanaoenda nje kupambana na maisha. Nyie mpo ofisini mnakula mishahara muwaache vijana wakapambane nje. Tanzania kazi hamna hata hizo za saidia fundi hamna.

5. Mnasema mtu akienda kufanya kazi nje ananyanyaswa. Mnajua manyanyaso yapo kila mahali ni bora mtu akanyanyaswe nje alipwe milioni kwa mwezi kuliko unyanyaswe na makampuni ya Tanzania halafu ulipwe laki na nusu. Hivi mnajua mishshara wanayolipwa wafanyakazi wa Bakhresa, Mohamed Enterprises, viwanda vya pale mikocheni kama Frostan n.k, mnajua hata hapo Ubungo EPZ watu wanaingia saa 1 asubuhi kutoka saa 11 na mshahara ni laki na nusu? Huo sio unyanyasaji?

6.Kampuni ya G4S Security imeajiri watu kutoka Uganda wanafanya kazi ya Ulinzi Asia na Ulaya na wanalipwa mamilioni. Na hizo kazi lazima agent atumike. Fatilieni makampuni ya ajira kisha mtoe orodha ili vijana wajue kampuni ipi ni genuine sio kuzuia tu vijana wasitoke nje ya nchi.

ACHENI WATU WAKAFANYE KAZI NJE YA NCHI.
 
Mimi vile ni mdada walinambia eti naenda kufanya umalaya, in short uhamiaji hawana ufahamu na wanadhalilisha mara uraia mbona uko vile in short uhamiaji ni jipu
Pole sana, too embarrassing
ndio maana wanaogopa dualism maana wanaaminisha wadogo zetu hii nchi ni dona kantre ukitoka nje unakuta ulikoenda ndo dona kantre kwenyewe.
kibaya zaidi uhamiaji ni alfa na omega “i wish i could be IGP”
 
Kupata Passport ilitakiwa iwe ni haki ya kila mtanzania.

Unaweza ukapata deal la ghafla na unahitaji kusafiri.

Kama huna passport umeshakosa.

Haya mambo mtu anayeendeshwa na VX na kulipiwa kila kitu na serikali hawezi kufahamu.
 
Kupata Passport ilitakiwa iwe ni haki ya kila mtanzania.

Unaweza ukapata deal la ghafla na unahitaji kusafiri.

Kama huna passport umeshakosa.

Haya mambo mtu anayeendeshwa na VX na kulipiwa kila kitu na serikali hawezi kufahamu.
Kweli mkuu
 
Back
Top Bottom