Mlatino Zeshalo
JF-Expert Member
- Sep 10, 2014
- 2,130
- 3,599
Ukitaka passport unapata kirahisi. Andaa documents zako zote, cheti cha kuzaliwa, academic certificates, affidavit/ cheti cha kuzaliwa cha mzazi (mmoja wapo), barua yako ya maombi ya passport na barua ya mzazi wako kukuruhusu kwenda nchi husika, barua ya utambulisho kutoka kwa WEO/VEO, copy ya kitambulisho au namba ya NIDA, Passport za ukubwa wanaohitaji wao ( nimeshasahau) lakini zinabackground nyeupe. Studio wanajua.Ku apply online kupo lakini lazima upeleke hard copy wakakague hapo ndo kuna ishu mara uwe na mwenyeji nchi unayokwenda mara mdhamini anayefanya kazi serikalini.
Wakati kukata passport sio kusafiri,jaman badilikeni mnakwamisha watu
Ukiwa na hivyo vyote, ingia kwenye web yao jaza form, lipia 20k ili uweze kuprint.
Tafuta link ya scholarship china, jaza form fresh, sehem ya kujaza passport number weka namba ya NIDA ili ikuruhusu kuendelea mbele. Ukimaliza utapewa pre admission letter, print. Ukikamilisha vyote hivyo nenda navyo uhamiaji wambie deadline ni baada ya week. Watakufanyia chap.
Hakikisha hakuna sehem umekosea herufi, umri wako au wa mzazi kwenye system ulivyojaza na physical documents zako kama affidavit, kitambulusho, nk.
Hivyo tu.