KUHUSU MHE. JOHN WEGESA HECHE KUONDOKA NCHINI BILA KUFUATA TARATIBU
Idara ya Uhamiaji inapenda kuujulisha Umma kuwa leo tarehe 18 Oktoba, 2025 katika Kituo cha Uhamiaji cha Mpaka wa Sirari mkoani Mara,
Mhe. John Wegesa Heche ameondoka nchini kwa kuvuka mpaka na kuingia nchi jirani bila kufuata taratibu na Kanuni za Uhamiaji zilizoundwa chini ya Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54.
Soma Pia: John Heche amekamatwa na kuzuiliwa mpaka wa Sirari akiwa anaelekea Kenya kwenye mazishi ya Odinga
Hivyo, Idara ya Uhamiaji inatoa wito kwa raia wa Tanzania na wageni wote wanaotoka na kuingia nchini kufuata taratibu na kanuni zinazongoza uingiaji, ukaazi na utokaji wa watu nchini ili kuepuka kutenda kosa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
View attachment 3490526
======
Kilichotokea:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amefanikiwa kuvuka mpaka wa Tanzania na Kenya kupitia mpaka wa Sirari mkoani Mara jioni ya siku ya Jumamosi Oktoba 18, 2025, baada ya kuzuka mvutano kati ya maofisa wa uhamiaji wa Tanzania na wenzao wa Kenya.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na Heche aliyekuwa mpakani hapo, tukio hilo lilitokea wakati kiongozi huyo akijaribu kuvuka kuelekea nchini Kenya ambako anatarajiwa kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, yatakayofanyika Jumapili Oktoba 19, 2025, katika kijiji chake cha Bondo.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa Heche alikumbana na maofisa wa uhamiaji wa Tanzania ambao walidai kuwa anahusishwa na kesi nchini, na hivyo wakajaribu kumzuia kuendelea na safari yake, lakini upande wa Kenya ulitaka ushahidi wa kisheria wa kumzuia kuvuka.
“Hapa ni One Stop Center, ukiwa unapiga muhuri wa passport tayari unakuwa upande wa Kenya. Askari wa Tanzania walikuja na kudai Heche ana kesi, lakini wenzao wa Kenya waliuliza kama kuna zuio la mahakama. Waliposhindwa kuonesha nyaraka yoyote ya kumzuia, askari wa Kenya walikataa kumkabidhi. Baada ya giza kuanza kuingia, wananchi wa Kenya wakamchukua kutoka kwa Askari wa Kenya na kuondoka naye,” kimesema chanzo hicho.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Heche sasa yupo nchini Kenya baada ya kupokelewa na wananchi waliokuwa mpakani.
Awali, taarifa rasmi ya CHADEMA ilisema kuwa Heche alizuiwa na maofisa wa Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania wakati akijiandaa kuvuka mpaka, na kwamba hati yake ya kusafiria ilizuiwa bila maelezo ya wazi.
Mpaka sasa mamlaka za Tanzania hazijatoa kauli rasmi kuhusu tukio hilo.