Uhamiaji wafafanua kampeni ya 'mjue jirani yako' kujengea wananchi uzalendo kutoa taarifa za uhalifu na wahamiaji haramu

Uhamiaji wafafanua kampeni ya 'mjue jirani yako' kujengea wananchi uzalendo kutoa taarifa za uhalifu na wahamiaji haramu

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Paul John Mselle ametoa ufafanuzi kuhusu kampeni mpya ya “Mjue Jirani Yako”, akisema inalenga kuongeza usalama wa kijamii na taifa kwa ujumla.

Akizungumza na Morning Jam ya Capital Radio, Mselle amesema kampeni hiyo ni mkakati mahsusi wa kuhakikisha kila raia anawajibika kwa kumtambua mtu anayeishi jirani naye, ikiwa ni hatua ya kuzuia uhalifu, ukaazi haramu, na kuongeza ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya dola.

Ameeleza kuwa kampeni hiyo pia inaleta faida za kijamii kama kuimarisha mshikamano, kusaidiana katika shida na kuhakikisha maendeleo ya pamoja katika jamii


 
Go1AooyWkAAXLJB.jpeg
 
Nendeni mkawakamate wale waliouwa na kuzika binadamu kama mifugo kwanza wapumbavu nyinyi
 
Vyombo vya ulinzi na usalama wao wameisha tengeneza uadui na wananchi, watavuna walichopanda
 
Back
Top Bottom