Uhamisho wa Watumishi kwa njia ya mfumo mpya wa Kieletroniki itabaki story!

Uhamisho wa Watumishi kwa njia ya mfumo mpya wa Kieletroniki itabaki story!

D___________Loy

Senior Member
Joined
Jan 21, 2020
Posts
168
Reaction score
146
Nawasilisha hii hoja nikiwa na nia njema. Kama kuna mwenye update atoe ushirikiano ili tufahamu ni lini huu mfumo utaanza kutoa huduma hasa katika kipengele cha Uhamisho.
 
Hao jamaa miyeyusho sana,mara ya mwisho walisema wanamalizia walioomba kwa barua kwanza ndo waanze wa mfumo...sijui hadi lini sasa?!!..au hadi wajisikie..
 
Nami nasubilia uanze kazi, nataka nitole huku Harmashauri ya Mpimbwe nihamie kwa Mama Kizommkazi Magogoni...
 
Huu mfumo ni hasa upande wa Uhamisho ni uongo hakuna atakae hama Kupitia huo mfumo kwa kuwa ubabaishaji ni mwingi ukiwapigia simu majibu yao ni haya:
#Subiri maombi yenu yanafanyiwa kazi utaona mabadiliko.
#Sasa hivi maombi ya kwenye mfumo hayafanyiwi kazi subiri mpaka katibu Mkuu atakapoamua mwenyewe kwani yeye ndio mwenye access ya kuingia kwenye mfumo. Kwa majibu hayo tu itoshe kusema Uhamisho haupo tena ila tunachezeana akili tu.
 
Back
Top Bottom