UHANITHI baada ya Kitovu cha Mtoto kukatika na kudondokea Sehemu zake za Siri

UHANITHI baada ya Kitovu cha Mtoto kukatika na kudondokea Sehemu zake za Siri

Nimepata kusikia huko uswahilini kuwa, eti mtoto wa kiume akidondokewa na kitovu chake ndo basi tena. Yaani jogoo halitapanda mlima. Mimi sioni uhusiano wa kisayansi hapo. Je kuna ye yote ajuaye anisaidie/atusaidie kupata ukweli wa jambo hili?

hakuna lolote mkuu, ni sawa tu na zile simulizi za 'Vimbwenelehi' na vibwengo!
 
Naweza kukubaliana na wewe,yaani wana-draw attention ya wazazi juu ya kidonda. Kitovu kinapodondoka hakina tena communication na sehemu nyingine ya mwili,kwanza huwa kimekufa,sasa taarifa toka kwenye kitovu mfu kwenda kwenye mwili hai ni ngumu kidogo. Kateni nondo tuendelee kufaidi.
Unajuwa mambo mengi ya mila, inatakiwa utulivu sana kuelewa, na pia wakati unatafakali kumbuka mambo hayo kipindi ambacho yakitokea ni enzi hizo, tunazo ziita za mababu yaani zaidi ya miaka 1000 nyuma.

Sasa nambie kwa mfano, tunaambiwa kuwa kufagia usiku kunapoteza bahati.
Je unaweza kuichambua vipi statement kama hii.
 
imani hizo kule kwetu hatuna kabisa ila huku pwani zimeshamiri sana sijui zimetokea wapi
 
hakika hata mimi nilisikia hivyo, lakin nilijitahidi kuuliza kwa matabibu nao walibainisha kama ifuatavyo. kuwa kitovu ni sehemu sensitive sana kwani mtoto akiwa tumboni kilitumika kupitisha chakula, hewa na mahitaji yote ya bin'Adam.

sasa kwa kuwa ni sehemu sensitive sana inatakiwa kutunzwa isipate na infection za aina yoyote kwani zinaweza sababisha madhara makubwa na hata kifo cha mtoto.

sasa matabibu wakaamua kuonyesha umuhimu wa hilo basi waliamua kuwaeleza wazazi wote wawe makini kwa hilo.

hayo ndio niliyobainishiwa na wataalamu wa afya.
 
Very true mkuu.
 
Hii ni mila ya siku nyingi sana, na imerithishwa kizazi hadi kizazi.

Madhumuni haswa ya kina mama kuambiwa hivyo, ni kuwataka wawe makini sana na kidonda kilichopo hapo (Kitovuni), kwani wakifanya mchezo na kidonda kikipata athali yoyote (Bacteria na Vijidudu vya Pepo punda), Mama anaweza kumkosa mtoto wake.

Ili wazazi (wakina mama) wawe makini na kumuangalia mtoto, ndio ikaja dhana hiyo ya Kitovu cha mtoto kiangaliwe sana ili kisije kumuangukia mtoto na kuwa na matatizo hayo yaliyo tajwa, na hii ni kuwa tunazingatia sana urijali na kuendeleza familia zetu.
ni ili kuhakikisha mtoto wa kiume anakua salama...?
 
Naweza kukubaliana na wewe,yaani wana-draw attention ya wazazi juu ya kidonda. Kitovu kinapodondoka hakina tena communication na sehemu nyingine ya mwili,kwanza huwa kimekufa,sasa taarifa toka kwenye kitovu mfu kwenda kwenye mwili hai ni ngumu kidogo. Kateni nondo tuendelee kufaidi.
Kitovu ni sumu mbaya, ila nami natafakari relation kati ya hayo maswali, there must some thing associated with dissolution which can be adsorbed if fall on that part and might result into serious effect to babies.
 
hizi ni imani tu sina uhakika lakini may be hata mimi nilshasikia hilo kwa bibi lakini sijui undani wake na kipindi hicho nilikuwa mtoto china ya miaka 14
 
Hizi ni myth mkuu ni kama vile kusema mtoto akibeba mzigo au kufagia watakuja wageni!
 
Hii nilipata kuisikia siku nyingi kidogo ya kwamba kama mtoto mdogo ataangukiwa na kitovu(Kile kijipande cha nyama kinachodondoka baada ya kitovu kukauka na kupona siku kadhaa baada ya mtoto kuzaliwa),sasa hicho kijipande kikimuangukia sehemu zake za siri,basi kama mtoto huyo ni wa kiume hatoweza kuattain erection maisha yake yote.

Huyu aliyeniambia akazidi kusema,ndo mana wakina mama uwa makini sana vitovu hivi,vinadondokea wapi?Mnaoshinda mawodini na mahospitalini tuambieni,jee hii ni kweli na kama ni kweli what is the mechanism behind.

Si kweli...kitovu hicho kikiangukia kwenye sehemu za siri za mtoto wa kiume (uume) si kweli kwamba mtoto huyo hatasimamisha uume wake katu. Hii ni moja ya mila tu na stori za tangu zamani ambazo zimesaidia sana wamama wengi kuwa waangalifu kwenye kutunza kitovu cha mtoto, na hii imesaidia sana kupunguza maambukizi ya kitovu ambayo ni sababu kuubwa ya kusababisha cord sepsis na septicaemia, magonjwa ambayo yanaongoza kwa kuua vichanga.

Nashkuru sana kwa uvumi au imani hii kwani maisha ya watoto wengi sana yanalindwa simply kwa akina mama kuwa waangalifu kwa vitovu vya watoto. Nimeona hata kina mama wasomi kabisa na Masters na PhD zao japo hawaamini lakini they don't take any chances kitovu kuangukia uumeni mwa watoto wao, na hapo ndio matunzo mazuri ya kitovu yanapoanzia!

Bravo aliyeanzisha imani hii..

NB: Sikufanya research rasmi, lakini kwa observation tu wakati nipo Idara ya vitoto vichanga Muhimbili (Neonatal Unit), vitoto vingi vilivyokuwa na cord sepsis vilikuwa vya kike...inawezekana sababu ni kina mama wako makini na vitovu vya watoto wa kiume zaidi ya watoto wa kike (not published).
 
Hakuna lolote hapo coz me mwanangu aliangukiwa kukawa na bonge la discusion kuhusiana na hiyo iman ikanibidi nitafute msaada wa kidaktari ila wote walisema hakuna uhusiano wowote kati ya kipisi cha kitovu na udindaji wa dogo, rite this moment mtoto wng hana shida hapo kabisa.

Hizi mila zipo nyingi sana zinapata nguvu kwa kuunganisha matukio tuu. Yaan mfano ukimuona simba mkodolee macho na usimuoneshe kisogo coz ukifanya hivyo Simba atakukimbia ni dhahili kabisa huyo aliyeileta maada labda alikutana na simba aliyeshiba na hivyo watu kuamini kutokana Vigumu kwa tukio kama lile kutokea tena kutokana watu kumuogopa simba.
 
Madokta na wataalam wa haya mambo ya kijamii naomba mnipe mawazo yenu kuhusu hili swala ambalo binafsi haliniingii akilini. Nimepita mikoa mingi hapa Tz na nimekutana na hii dhana ya kuwa kitovu cha mtoto kinapokatika na kudondokea sehem yake ya siri basi automatically huyu mtoto wa kiume anakuwa ******* na Kama ni wa kike basi hatakuwa na hisia za mapenzi na hatazaa. Je wataalam wa JF mnalizungumziaje hili na kitaalam kitovu kinauhusiano gani na sehemu za Siri za mtoto?

ONE LOVE
 
Kwanza ningependa kujua Kama ni kweli au ni Imani tu.
 
Halijathibitishwa kisayansi na hakuna matarajio ya kuweza kuthibitishwa ever.

Ni imani tu ambazo kwangu naona zimekosa muelekeo
 
Madokta na wataalam wa haya mambo ya kijamii naomba mnipe mawazo yenu kuhusu hili swala ambalo binafsi haliniingii akilini. Nimepita mikoa mingi hapa Tz na nimekutana na hii dhana ya kuwa kitovu cha mtoto kinapokatika na kudondokea sehem yake ya siri basi automatically huyu mtoto wa kiume anakuwa ******* na Kama ni wa kike basi hatakuwa na hisia za mapenzi na hatazaa. Je wataalam wa JF mnalizungumziaje hili na kitaalam kitovu kinauhusiano gani na sehemu za Siri za mtoto?

ONE LOVE

Kwa kuanzia....Imani hii si ya kweli, japo nachelea kuiita potofu (Kiswahili kigumu sometimes). Siiti potofu kwa sababu haina hasara kwa mtoto, bali ina faida!

Dhana hii ilianza zamani za mabibi zetu walipogundua kuwa kama hutunzi vyema kitovu cha mtoto mchanga basi mtoto huyo ataugua na kufariki. Na hilo ni kweli, kwani mtoto atapata 'umbilical infection/sepsis' na kama hatapata matibabu ya haraka na stahiki atafariki kwa 'septicaemia'.

Kwa hiyo imani hiyo ilitungwa ili wamama wawe makini kuchunga kitovu kisiangukie uume mtoto akawa h*nithi, wakati huo huo mama atachunga kitovu kisipate maambukizi. Hivyo japo si kweli kwamba mtoto akiangukiwa kitovu anakuwa h*nithi, lakini uongo huo una faida kwa mtoto kuangaliwa vyema kitovu chake.
 
Mkuu Riwa asante sana kwa maelezo yako
yametoa ufafanuzi mzuri sana sana
Asante sana
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom