Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,255
- 1,565
Hakuna shaka kuwa janga la uharibifu wa mazingira ni tatizo la Dunia nzima, athari za janga hili ni kubwa sana, Tanzania kama sehemu ya Dunia tumeanza/tunaendelea kupitia maafa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mvua, kupungua kwa vyanzo vya maji, mafuriko, kukauka kwa mabwawa etc ambavyo vyote hivi vina athari kubwa kwenye uchumi wa Nchi na Mtanzania mmoja.
Kama Taifa, moja ya njia za kupambana na janga hili ni kupanda miti, natambua kampeni zinazofanywa na Taasisi mbali mbali za Serikali pamoja na Wadau wa Mazingira, lakini uhalibifu bado ni mkubwa.
Tunaweza kutumia Shule za Msingi , Shule za Sekondari pamoja na vyuo kuhakikisha tunapambana kwa nguvu zote katika upandaji wa miti. Mh Waziri (anayeshughulikia Mazingira), Mh Waziri -OR TAMISEMI- MMK, tukiazisha mashindano ya upandaji miti kwa Shule zote na vyuo , kisha shule 10 (mfano) zitakazoshinda zipewe hata milioni 200, amabazo mgao wake unaweza kuwa nusu ya fedha hizo ziende kuboresha mazingira na nusu iende kwa Walimu na Wanafunzi, kwa Idadi ya Shule na vyuo vilivyopo, baada ya miaka kumi, Tanzania itakuwa GREEN TENA.
Tunaweza kujifunza kwa Shule ya Sekondari Longido- ukifika hapo, hakika utaiona Tanzania ile yenye miti na uoto wa asili.
MWENYEZI MUNGU IBARIKI TANZANIA
MWENYEZI MUNGU MBARIKI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN