Uhasama wa Mbowe na Ndugai ulianzia Kibaha Secondary

Uhasama wa Mbowe na Ndugai ulianzia Kibaha Secondary

Nadharia yako sio sahihi. Enzi hizo (enzi zetu) mtu aksoma shule ya serikali ilikuwa heshma kubwa. Wenye uwezo wa pesa/ madaraka walitumia msuli wao kuhakikjsha watoto wao wanasoma Goernment school. Ikitokea .toto kafeli la saba akaenda private form two au three alihamishiwa shule ya serikali taratibu za enzo hizo ziliruhusu kitu hicho.
Watoto wa dotcom hawawezi kukuelewa, tuliosoma enzi hizo ilikuwa ni fedheha kusoma private schools. Labda IST lakini si hizi Shaaban Robert au Mzizima. Shule tumesoma na watoto wa cream yote ya viongozi wa nchi.
 
  • Thanks
Reactions: RMC
Nakumbuka tukiwa kidato cha tano pale Ihungo sekondari Mh. Mbowe alikuwa kidato cha sita, wote tukiwa tunakaa Bweni la Mt. Meru kama sikosei.

Shule nzima nakumbula Mh. Mbowe ndo alikua mwanafunzi anapanda ndege kurudi kutoka likizo.

Mambo yalikuwa moto sana, sasa sijui kama Mh. hakuacha kweli mfuasi kule BK make mambo yetu wananfunzi tulijichanganya sana.

Hii ya Mbowe kusoma na Ndugai ndo haileti picha sahihii, Mh. Ndugai ni mdogo sana ki umri kwa Mbowe.
Kiumri Ndugai amemzidi Mbowe nadhani kwa mwaka mmoja au miwili kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, yaani kama wangekulia mtaa mmoja ingekuwa wamecheza pamoja.
 
Kama ofisi ya CAG ina watu wenye akili ndogo kama zako basi twafa, tutakuwa na bahati mbaya sana kama taifa
Kama unatumia akili faster hivi Kwa kutumia social media comments za avatars basi kazi ipo

Wewe ni zaidi ya ramli
 
Acha uongo shule ya sekondari Kibaha miaka ya tangu 1963 ilipoanzishwa mpaka miaka ya 1990 haikuwahi kuruhusu mwanafunzi kuwa na kitabu chake binafsi maana ilikuwa imejitosheleza kwa kila idara maana ilikuwa inadhaminiwa na nchi Skandinavia. Shule hiyo ilianzishwa na shirika la elimu Kibaha (Kibaha Education Center-KEC) ina maktaba yake yenye hadhi ya juu ndio wakati fulani chuo kikuu huria kabla hawajapata eneo la kujenga walikuwa wanatumia maktaba hiyo ambamokila aina ya vitabu vilikuwemo mpaka tafiti za chuo kikuu cha Dar Es Salaam na SUA.
Kwa hiyo wadanganye wasioelewa.

Shule hiyo ilikuwa inaitwa Co-education kwa upande wa O level na A level ni wavulana tupu.

Kidato cha tano-sita tahasusi zilikuwa mbili tu yaani
1. PCM-Physics, Chemistry and Advanced Mathematics Wanafunzi 72 kwa mikondo mitatu yaani X, Y and Z kila mmoja wanafunzi 24 walikuwa wanachaguliwa kuchukua tahasusi hiyo ni wale waliokuwa daraja la kwanza pointi 7 kushuka hadi daraja la pili pointi 18 tu
2. CBA-Chemistry, Biology and Agriculture (Wanafunzi 24) tu Tanzania nzima (mkondo mmoja) waliochaguliwa kwenda hapa wale walikuwa na daraja la kwanza pointi 7-9
Kila mwisho wa wiki mnafanya mtihani na matokeo yanabandikwa ubaoni kwa uwazi jumatatu yake halafu ukipata alama chini ya 25 unapigiwa mstari mwekundu halafu unasutwa kwenye baraza hadi kutandikwa viboko mbele ya wanafunzi wa jinsia zote.
Waliosoma hapo kwenye mtihani wa mwisho wote walikuwa wanafaulu kwenda ama chuo cha UDSM, SUA au nje ya nchi hasa Urusi, Yugoslavia, Ujerumani nk

Hawana mbwembwe, ni wa kimya wana akili sana

Ila kama alisoma O level inawezekana lakini sio A level maana enzi hizo shule ya Kibaha ambayo iko chini ya shirika la elimu Kibaha ilikuwa haitoi daraja '0', na '4' wengi waliku daraja la kwanza na la pili wawili au watatu wanaweza kuwa daraja la tatu ambao hata hivyo na wenyewe walikuwa wanachaguliwa kujiunga chuo kikuu.

Kuna baadhi wa walimu walikuwa wanatoka chuo kikuu cha UDSM waliokuwa wanapangwa kwenda kufundisha hapo walikuwa wakumbana na vichwa vilivyo mbele ya silabasi
Wewe umekurupuka.
Ndugai, nyalandu na hao kina kikwete wamepita kibaha wakiwa O level na 1 wapo NI class mate wangu na hata kwenye group la mwaka wetu yupo
 
Hawa miamba walijuana Kibaha Secondary.

Enzi hizo baba yake Freeman akiwa tycoon mkubwa sana nchini, alikuwa na mahotel Dar, Moshi na Arusha na alikuwa na ukaribu sana na baba wa Taifa mwalimu JK Nyerere.

Job Ndugai alitokea familia fukara kama watanzania wengi ila kichwani zilikwemo.

Kuna siku Job aliomba kitabu kwa Freeman akanyimwa ndio uhasama ukaanzia hapo,hicho kitabu alikuwa nacho Freeman peke yake shule nzima.
Chai
 
Hili nalo ni jipya😎
Mpaka December tunakamilisha kitabu
 
Hao wote walikuwa Maskini tu

Mbowe Hotel au Billicanas ilikuwa Nyumba ya NHC kama yalivyo Makao makuu ya Chadema

Sasa Ndio Tajiri huyo?
Mkuu usibishe. Baba yake Mbowe, Mzee Aikaeli alikuwa tajiri kabla hata ya uhuru. Aishi Hotel ni mojawapo ya hoteli kongwe ya kitalii kanda ya kaskazini. Ilimilikiwa na huyo mzee.
 
Hawa miamba walijuana Kibaha Secondary.

Enzi hizo baba yake Freeman akiwa tycoon mkubwa sana nchini, alikuwa na mahotel Dar, Moshi na Arusha na alikuwa na ukaribu sana na baba wa Taifa mwalimu JK Nyerere.

Job Ndugai alitokea familia fukara kama watanzania wengi ila kichwani zilikwemo.

Kuna siku Job aliomba kitabu kwa Freeman akanyimwa ndio uhasama ukaanzia hapo,hicho kitabu alikuwa nacho Freeman peke yake shule nzima.
Punguza mauongo we nae, huoni hata aibu kuandika kitu usichokua nacho na ushahidi.
 
Wewe umekurupuka.
Ndugai, nyalandu na hao kina kikwete wamepita kibaha wakiwa O level na 1 wapo NI class mate wangu na hata kwenye group la mwaka wetu yupo
Wewe ndio mkurupukaji ijapokuwa ni kweli huyo JK wako alisoma O level hapo Kibaha kwa masomo ya biashara ambapo alimaliza mwaka 1969 kisha akaenda Tanga technical school kwa taasusi ya HGE (masomo ya wavivu wa ubongo).
 
Introduction umepatia,

hiyo ya kitabu ndo umefunga kamba
 
Back
Top Bottom