Uhasama wa Tanzania bara na Zanzibar unazidi kukua na utaleta madhara makubwa kama yanayosemwa hayatashughulikiwa

Kikemikali, muungano wetu ni compound na sio mixture!. Kikemikali, Ukichanganya vitu viwili na kuwa mixture, vitu hivyo vinakuwa havijaungana kikemikali, mfano kuchanhanya pombe na maji, kwa kutumia fractional distillation inawezekana kuitenganisha pombe na.maji. Vitu kama maji, H2Ounaweza kutenganisha hydrogen na oxygen, chumvi, unaweza hydrogen na.chlorine etc.
Duh!
Leo nimekuwa jasiri wa kukusoma hadi kwenye hiyo aya niliyonyanyua na kuibandika hapa.
Umeeleza vyema huko juu, lakini ukaja kujichanganya kwenye hizi kemikali, ambazo ni dhahiri huna ujuzi nazo.
Ukizungumzia hydrogen na chlorine kutengeneza compound, ambayo ni HCl, au maji, ukanyambua hydrogen na Oksijen, tayari unazungumzia kompound, huwezi tena kuzifanannisha na pombe na maji, ambzo ni compound mbili zilizochanganywa tu kwa pamja na zinaweza kutenganishwa kirahisi, kwa distillation kama ulivyoeleza hapo na kubaki na pyuwa compond ya maji, na ya pili ikiwa compound ya pombe.

Maelezo yako ya aina ya muungano wetu inashawishi kukubalika, lakini elewa kwamba hata hizi 'elements ulizozitaja kwenye mifano yako kiuhalisia zinaweza kunyambuliwa. Hydrogen atoms zake mbili zinatenganishwa na kuwa mbalimbali, na teknologia hiyo ndiyo inayofanya mambo mengi siku hizi. Kwa hiyo hakuna kinacho shindikana. hata huu muungano imebaki swala la muda tu. kama hakutatokea kiongozi mwenye ushawishi wa kutosha kuujenga upya na kuwashirikisha wananchi wake katika kazi hiyo, hatuna muda mwingi sana nao huu muungano.

Tanganyika inaweza kulazimisha muungano uendelee kwa nguvu au kwa kutoa rushwa kwa waZanzibari kama inavyofanyika sasa? Muungano wa kutumia nguvu ni shida tupu. Kuna mifano duniani ya miungano ya kutumia mabavu iliyodumu? Sina mfano usiokuwa na mashaka. Labda Marekani, zile Cnfederate states na hizi nyingine walizokuwa wakipambana nazo. Huu mfano tunaweza kuutumia hapa? Sina jibu ya hilo, ingawa naelekea kulikubali. Wakati mwingine manufaa ya muungano yasiyoonekana sasa, huko baadae ukishaleta neema watu wanasahau magumu waliyoyapitia. Confederate leo ukiwaambia wajitenge sidhani kuwa utawapata wengi.

Leo nimekusoma mkuu P, na nimeona mantiki ndani ya andiko lako refu kiasi.
 
Huu Muungano wetu adimu na adhimu, ume undergo chemical reaction kwa mataifa mawili Tanganyika na Zanzibar kuungana, kupoteza utaifa wake.na kuunda taifa jipya la Tanzania ambalo ni compound, halivunjiki tena!.

Muungano tutaulinda kwa gharama yoyote.
Hii sehemu ya mwisho ni kama unachekesha watu tu, au unakejeli tu ukiwa na maana ya kinyume cha unachozungumzia. Umeona wapi kiongozi anayejishughulisha na swala kama hilo la kulinda muungano; au hata "kujenga huo utaifa"? Wewe ni ujenzi gani unaouona ukifanyika hivi sasa, kama sio kinyume chake kabisa!
 
Sie wengine zanziber ni sawa na kisiwa cha mafia ukerewe au kome, hizi kelele zinachagizwa na wanasiasa wa hovyo kama lissu na jussa,

Nyerere aliuliza mpemba na mdigo na mjaluo yupi ndugu zaidi? Wapo wapemba wananunua mchele na hatuna shida nao, wapo dadapoa kutoka shinyanga wako unguja, kuna wamasai wapo fukwe za tumbatu wakisaka vibabu vya kiitaliano.
 
Muungano tutaulinda kwa gharama yoyote.
Ni waziu kabisa, leo umevuta hisia zangu, kwani siondoki kwenye bandiko lako hili.
Ukitaka mstari wako huo uwe na maana halisi, fanya kama Kagame alivyofanya na 'genocide' yake.
Kule kuzungumzia tu jambo lolote linalohusiana au kuamsha hisia za watu juu ya 'genocide', piga marufuku. Mtu akisikika anazungumzia mambo ya mfarakano wa muungano adhimu, jela inamsubiri. Bila ya hivyo, uchokonozi utaendelea na taratibu muungano utaendelea kulegea.
Nimekumbuka jambo jingine katika mfano wa 'compound' zako uliotoa hapo juu.
Ungetaka muungano uwe compound ya kweli, na siyo mchanganyiko ty wa compound mbalimbali zinazoweza kuchambuliwa kirahisi, jambo la kwanza ni kuzipika hizo elements katika tanuru la moto mkali - ondoa vitu vinavyozuia utengenezwaji wa compound imara. Unda serikali moja, acha kucheza na nyani karibu ya shamba lako la mahindi. Unaacha vichaka jirani na shamba wanakoweza kujificha nyani na mara kwa mara wanaibuka kushambulia shamba, kwa nini? Serikali moja, basi, na achana kabisa kucheka na nyani wakati wowote. Hapa umetumia mabavu, ambayo hatimaye yanaweza kuifanya compound yako kuwa imara zaidi.

Nadhani sasa nimemalizana nawe.
 
Sheria iliyounda Senagambia, had provisions za kuuvunja. Ule ulikuwa ni mkataba, the same to UK kujitoa EU.

Huu Muungano wetu adimu na adhimu ni Muungano wa dhima ya Muungano wa milele, zile Articles of the Union, sio mkataba, ni makubaliano ya milele, hakuna provision ya kuuvunja Muungano, tumeunganisha nchi mbili kwa kuchanganya udongo, na kuumwaga bara na Zanzibar, ili kuuvunja, lazima tuutafute ule udogo, tuupembue, punje za udongo wa Tanganyika, zirejeshwe Tanganyika na punje za Zanzibar zirejeshwe Zanzibar.

Kikemikali, muungano wetu ni compound na sio mixture!. Kikemikali, Ukichanganya vitu viwili na kuwa mixture, vitu hivyo vinakuwa havijaungana kikemikali, mfano kuchanhanya pombe na maji, kwa kutumia fractional distillation inawezekana kuitenganisha pombe na.maji. Vitu kama maji, H2Ounaweza kutenganisha hydrogen na oxygen, chumvi, unaweza hydrogen na.chlorine etc.

Lakini vitu viwili vinapoungana kwa chemical reaction, vitu viwili vile hufa na kuzaliwa kitu kipya kinachoitwa compound, huwezi tena kuvirejesha kwenye hali ya awali kama kuyeyusha sabuni ya unga kwenye maji, kunatokea chemical reaction, huwezi kutenganisha.

Huu Muungano wetu adimu na adhimu, ume undergo chemical reaction kwa mataifa mawili Tanganyika na Zanzibar kuungana, kupoteza utaifa wake.na kuunda taifa jipya la Tanzania ambalo ni compound, halivunjiki tena!.

Muungano tutaulinda kwa gharama yoyote.
P
Hayo yote unayoyang'ang'ania umeyajaza kwenye mawazo yako tu.Ila kiuhalisia ukiamua kuyakataa inawezekana.Nyerere alisema hakuwa malaika kwamba hakukosea.Mmeng'ang'ania makosa yake tu badala ya kuachana nayo.
 
Jinsi masuala ya muungano yanavyoshughulikiwa na kwa sasa, ni mtu kipofu wa akili tu ndio hataona kwamba kadiri siku zinavyopita mbegu za uhasama kati ya Tanzania bara na Zanzibar inazidi kuota mizizi, majani ya chuki yakizidi kuchanua. Ni kiongozi mjinga tu asieweza kuona kwamba jinsi haya mambo ya muungano yanakoenda, yanaweza kusababisha mgongano (confrontation) mkubwa sana kati ya wakazi wa Zanzibar walioko bara na wakazi wa bara walioko Zanzibar.

Badala ya kujibu hoja zinazowekwa mezani, viongozi wameamua kwa makusudi kuwashambulia wale wanaozitoa, bila kuona kuwa kwa kufanya hivyo wanazidi kuchochea uhasama kati ya Tanzania bara na Zanzibar. Kwa kumfurahisha nani?

Kama Tanzania bara wanaona kwamba kwao kero kubwa ya muungano ni kutokuwa na serikali ya Tanganyika, kwa nini hawasikilizwi? Wakati wa Nyerere huenda kulikuwa na sababu za msingi kuwa na serikali mbili, lakini ni wazi hilo halikubaliki kwa sasa, na huwezi kulilazimisha likaendelea kuwapo bila kuleta madhara.

Muungano tunaweza kulazimishwa uendelee kuwapo kwa kutumia nguvu ya dola, lakini haitazuia watu kuanza violence (kupigana) uhasama unaojitokea ukizidi kukua. Amini nawaambieni, huu muungano mnaodai uko imara unaweza kuvunjwa kwa nguvu na kuleta hali ya machafuko bara na visiwani. Watanzania bara walioko visiwani wataondolewa kule kwa nguvu, na wa-Zanzibar walikoko bara wataondolewa huku kwa nguvu, na hata kupoteza mali au uhai wao. Ndilo tunalosubiri? Au tunadhani haliwezi kutokea Tanzania, vitu kama hivyo vinatokea Rwanda tu?

Muungano ulifanyika zaidi ili Zanzibar kusiwe na counter-revolution ya Waarabu (wajomba) walipopinduliwa na kuchinjwa, na kwa Tanganyika kulinda usalama wake katika kuwa kitovu cha kupigania uhuru wa Afrika. Sasa hizi sababu sio hoja tena. Kama imefikia mahali Watanzania hawautaki muungano, basi ni bora uvunjwe kwa utaratibu na kuelewana, watu waulizwe je ungependa kubaki bara au kurudi visiwani, au ungependa kubaki visiwani au kurudi bara nk. Labda tuanze na "Referendum", wananchi ndio tuamue kidemokrasia kama tunataka au hatutaki muungano, sio serikali ituamulie kwa maslahi yake, au maslahi ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar, au maslahi ya CCM.

Tusione aibu kukaa chini na kutafakari kuuvunja muungano, kama kuwa na serikali moja au tatu haiwezekani, kwa sababu mfumo wa muungano uliopo sasa hivi unazidi kukuza uhasama kati ya Tanzania bara na Zanzibar. Mwaka 1982 Senegal na Gambia waliungana na kuwa nchi moja ya Senegambia. Iliposhindikana, waliuvunja muungano, mwaka 1989. Juzi hapa Uingereza imejitoa kwenye muungano wa Ulaya. Kwa hiyo Tanzania haitakuwa ya kwanza kuvunja muungano.
Mkuu mbona solution ipo tu tuungane kama nchi huru kwenye east Africa community itatoasha hiyo
 
Ingekuwa muungano tuliutaka sisi ndiyo ungesema yote hayo. Huu muungano ni wa Uingereza na Mmarekani. Kama wao hawautaki utavunjika siku moja tu.

Tumewachiwa dudu la "divide and rule" sisi kwa ujinga wetu tunaona tuna muungano.
 
Sheria iliyounda Senagambia, had provisions za kuuvunja. Ule ulikuwa ni mkataba, the same to UK kujitoa EU.

Huu Muungano wetu adimu na adhimu ni Muungano wa dhima ya Muungano wa milele, zile Articles of the Union, sio mkataba, ni makubaliano ya milele, hakuna provision ya kuuvunja Muungano, tumeunganisha nchi mbili kwa kuchanganya udongo, na kuumwaga bara na Zanzibar, ili kuuvunja, lazima tuutafute ule udogo, tuupembue, punje za udongo wa Tanganyika, zirejeshwe Tanganyika na punje za Zanzibar zirejeshwe Zanzibar.

Kikemikali, muungano wetu ni compound na sio mixture!. Kikemikali, Ukichanganya vitu viwili na kuwa mixture, vitu hivyo vinakuwa havijaungana kikemikali, mfano kuchanhanya pombe na maji, kwa kutumia fractional distillation inawezekana kuitenganisha pombe na.maji. Vitu kama maji, H2Ounaweza kutenganisha hydrogen na oxygen, chumvi, unaweza hydrogen na.chlorine etc.

Lakini vitu viwili vinapoungana kwa chemical reaction, vitu viwili vile hufa na kuzaliwa kitu kipya kinachoitwa compound, huwezi tena kuvirejesha kwenye hali ya awali kama kuyeyusha sabuni ya unga kwenye maji, kunatokea chemical reaction, huwezi kutenganisha.

Huu Muungano wetu adimu na adhimu, ume undergo chemical reaction kwa mataifa mawili Tanganyika na Zanzibar kuungana, kupoteza utaifa wake.na kuunda taifa jipya la Tanzania ambalo ni compound, halivunjiki tena!.

Muungano tutaulinda kwa gharama yoyote.
P
Unachanganya mambo sana, Unasema muungano imepoteza Tanganyika na Zanzibar lakini bado tunaona Zanzibar ikiwepo, ndiyo maana tunasema lengo la muunganiko haikutimia..watu warudi Lab kufanya tena titration.

Rejea kauli ya Mzee Pinda akiwa Waziri Mkuu kuwa Zanzibar siyo nchi baada ya kubanwa sana Bungeni ajibu...Viongozi wako wa CCM ni sikio la kufa, hivi mnashauriana nini huko Chamani?
 
Jinsi masuala ya muungano yanavyoshughulikiwa na kwa sasa, ni mtu kipofu wa akili tu ndio hataona kwamba kadiri siku zinavyopita mbegu za uhasama kati ya Tanzania bara na Zanzibar inazidi kuota mizizi, majani ya chuki yakizidi kuchanua. Ni kiongozi mjinga tu asieweza kuona kwamba jinsi haya mambo ya muungano yanakoenda, yanaweza kusababisha mgongano (confrontation) mkubwa sana kati ya wakazi wa Zanzibar walioko bara na wakazi wa bara walioko Zanzibar.

Badala ya kujibu hoja zinazowekwa mezani, viongozi wameamua kwa makusudi kuwashambulia wale wanaozitoa, bila kuona kuwa kwa kufanya hivyo wanazidi kuchochea uhasama kati ya Tanzania bara na Zanzibar. Kwa kumfurahisha nani?

Kama Tanzania bara wanaona kwamba kwao kero kubwa ya muungano ni kutokuwa na serikali ya Tanganyika, kwa nini hawasikilizwi? Wakati wa Nyerere huenda kulikuwa na sababu za msingi kuwa na serikali mbili, lakini ni wazi hilo halikubaliki kwa sasa, na huwezi kulilazimisha likaendelea kuwapo bila kuleta madhara.

Muungano tunaweza kulazimishwa uendelee kuwapo kwa kutumia nguvu ya dola, lakini haitazuia watu kuanza violence (kupigana) uhasama unaojitokea ukizidi kukua. Amini nawaambieni, huu muungano mnaodai uko imara unaweza kuvunjwa kwa nguvu na kuleta hali ya machafuko bara na visiwani. Watanzania bara walioko visiwani wataondolewa kule kwa nguvu, na wa-Zanzibar walikoko bara wataondolewa huku kwa nguvu, na hata kupoteza mali au uhai wao. Ndilo tunalosubiri? Au tunadhani haliwezi kutokea Tanzania, vitu kama hivyo vinatokea Rwanda tu?

Muungano ulifanyika zaidi ili Zanzibar kusiwe na counter-revolution ya Waarabu (wajomba) walipopinduliwa na kuchinjwa, na kwa Tanganyika kulinda usalama wake katika kuwa kitovu cha kupigania uhuru wa Afrika. Sasa hizi sababu sio hoja tena. Kama imefikia mahali Watanzania hawautaki muungano, basi ni bora uvunjwe kwa utaratibu na kuelewana, watu waulizwe je ungependa kubaki bara au kurudi visiwani, au ungependa kubaki visiwani au kurudi bara nk. Labda tuanze na "Referendum", wananchi ndio tuamue kidemokrasia kama tunataka au hatutaki muungano, sio serikali ituamulie kwa maslahi yake, au maslahi ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar, au maslahi ya CCM.

Tusione aibu kukaa chini na kutafakari kuuvunja muungano, kama kuwa na serikali moja au tatu haiwezekani, kwa sababu mfumo wa muungano uliopo sasa hivi unazidi kukuza uhasama kati ya Tanzania bara na Zanzibar. Mwaka 1982 Senegal na Gambia waliungana na kuwa nchi moja ya Senegambia. Iliposhindikana, waliuvunja muungano, mwaka 1989. Juzi hapa Uingereza imejitoa kwenye muungano wa Ulaya. Kwa hiyo Tanzania haitakuwa ya kwanza kuvunja muungano.
Watakaoteseka ni akina Samia na wazanzibari wenzake.
 
Kama Tanzania bara wanaona kwamba kwao kero kubwa ya muungano ni kutokuwa na serikali ya Tanganyika

HATUTAKI SERIKALI ya Tanganyikana. Tunataka nchi ya Tanganyika.

Hatutaki serikali tatu. Serikali tatu zinakupa Marais watatu, mabunge watatu, wabunge mia tisa, Majaji Wakuu Watatu, Makamu wa Rais watatu, Waziri Wakuu watatu.

HAKUNA formulation ya Muungano wa watu milioni 62 na watu milioni moja unusu halafu ikawa fair. Mkubwa atanyonywa na vilio havitaisha.

Huwezi kuunganisha shamba lako na mashamba ya Muhammed Dewji halafu muanze kugawana mavuno na mamlaka ya uendeshaji na amana za mikopo na nafasi za wakulima. Wewe unamwongezea thamani gani ?

Tuuvunje Muungano, for the love of God!
 
Back
Top Bottom