Duh!Kikemikali, muungano wetu ni compound na sio mixture!. Kikemikali, Ukichanganya vitu viwili na kuwa mixture, vitu hivyo vinakuwa havijaungana kikemikali, mfano kuchanhanya pombe na maji, kwa kutumia fractional distillation inawezekana kuitenganisha pombe na.maji. Vitu kama maji, H2Ounaweza kutenganisha hydrogen na oxygen, chumvi, unaweza hydrogen na.chlorine etc.
Leo nimekuwa jasiri wa kukusoma hadi kwenye hiyo aya niliyonyanyua na kuibandika hapa.
Umeeleza vyema huko juu, lakini ukaja kujichanganya kwenye hizi kemikali, ambazo ni dhahiri huna ujuzi nazo.
Ukizungumzia hydrogen na chlorine kutengeneza compound, ambayo ni HCl, au maji, ukanyambua hydrogen na Oksijen, tayari unazungumzia kompound, huwezi tena kuzifanannisha na pombe na maji, ambzo ni compound mbili zilizochanganywa tu kwa pamja na zinaweza kutenganishwa kirahisi, kwa distillation kama ulivyoeleza hapo na kubaki na pyuwa compond ya maji, na ya pili ikiwa compound ya pombe.
Maelezo yako ya aina ya muungano wetu inashawishi kukubalika, lakini elewa kwamba hata hizi 'elements ulizozitaja kwenye mifano yako kiuhalisia zinaweza kunyambuliwa. Hydrogen atoms zake mbili zinatenganishwa na kuwa mbalimbali, na teknologia hiyo ndiyo inayofanya mambo mengi siku hizi. Kwa hiyo hakuna kinacho shindikana. hata huu muungano imebaki swala la muda tu. kama hakutatokea kiongozi mwenye ushawishi wa kutosha kuujenga upya na kuwashirikisha wananchi wake katika kazi hiyo, hatuna muda mwingi sana nao huu muungano.
Tanganyika inaweza kulazimisha muungano uendelee kwa nguvu au kwa kutoa rushwa kwa waZanzibari kama inavyofanyika sasa? Muungano wa kutumia nguvu ni shida tupu. Kuna mifano duniani ya miungano ya kutumia mabavu iliyodumu? Sina mfano usiokuwa na mashaka. Labda Marekani, zile Cnfederate states na hizi nyingine walizokuwa wakipambana nazo. Huu mfano tunaweza kuutumia hapa? Sina jibu ya hilo, ingawa naelekea kulikubali. Wakati mwingine manufaa ya muungano yasiyoonekana sasa, huko baadae ukishaleta neema watu wanasahau magumu waliyoyapitia. Confederate leo ukiwaambia wajitenge sidhani kuwa utawapata wengi.
Leo nimekusoma mkuu P, na nimeona mantiki ndani ya andiko lako refu kiasi.