KERO Uholela wa NGONO, POMBE NA MUZIKI: Ndilo janga kubwa zaidi la kizazi chetu"

KERO Uholela wa NGONO, POMBE NA MUZIKI: Ndilo janga kubwa zaidi la kizazi chetu"

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Kwa wakubwa wetu waliozaliwa miaka ya 1960-1970, maarufu kama baby boomers, watakuwa na kumbukumbu nzuri ya usemi maarufu wa enzi hizo, "Sex, drugs, rock and roll" ambao kimsingi ulikuwa ni wimbo wa Ian Durry wa mwaka 1977.

"Sex, drugs, rock and roll" haukuwa wimbo au usemi tu wa wakati huo. Ulikuwa ni kielelezo cha juu cha mapinduzi ya utamaduni. Uliakisi maisha ya watu maarufu wa wakati huo kama Freddie Mercury mwanamuziki maarufu wa band ya muziki wa rock&Roll iliyoitwa Queens kutoka Uingereza. Freddie alifariki kwa ugonjwa wa UKIMWI tarehe 24 November 1991.

Zama hizi mpya zilishuhududia kukua kwa utamaduni mpya uliohalalisha na kuhimiza ngono kabla na nje ya ndoa, biashara ya ngono na ushoga, ufahari katika matumizi ya vilevi na madawa ya kulevya na kukua kwa madisko na matamasha ya muziki.

Kwa kifupi huu ulikuwa ni mwanzo wa utamaduni mpya uliorithiwa sasa na vizazi vya millenials na Gen Z. Kwa hali ilipofika sasa, "ngono pombe na muziki" ndio maana halisi ya maisha ya kisasa. Ukiingia katika mitandao ya kijamii, vyombo vyetu vya habari, majukwaa ya sanaa na vijiwe vya maongezi yetu, INJILI inayohubiriwa ni hiyo, "ngono, pombe na muziki"

Tunu za maadili ya asili sasa hivi zinadharauliwa na kuchukuliwa ni ushamba. Ndoa na ubikira ni kitu inachukuliwa kuwa kitu cha kizamani, sasa hivi mijadala ni idadi ya ma "X" na kufikishana kileleni. Kulewa na kuvuta shisha ndio aina mpya ya ustaarabu huku nyimbo zilizojaa matusi na zinaa zikiwa ndio burudani ya wakati wa sasa.

Jambo la kushangaza sana, pamoja na kwamba tumeshudia athari kubwa za utamaduni huu mpya ni kama tumekosa utashi wa kisiasa wa kuutambua utamaduni huu kama ni janga la kijamii lenye madhara makubwa ya sasa na ya muda mrefu. Hatuambiani ukweli juu ya utatu huu wa maovu jinsi unavyoimaliza jamii yetu.

Kama kweli tumechoka kupoteza nguvu kazi ya taifa kwa UKIMWI na uraibu wa vilevi, ongezeko la watoto wa mitaani, na watoto wa nje ya ndoa, matumizi mabaya ya rasilimali fedha, umasikini; ni muhimu tukafanya hatua ya makusudi ya kuutambua utamaduni wa uholela wa NGONO, POMBE na MUZIKI kama janga la Dunia na kizazi chetu.
 
Ngono, pombe na mziki ni vitu vipo maelfu ya miaka, hivyo wenye tatizo ni hicho kizazi na sio vitu hivyo.

Note: umeandika mashudu🚮🚮🚮🚮
We jamaa unapenda kujibu hoja kwa kukurupuka sana, mleta mada kachambua vizuri sana.

Hebu jiulize tu miaka 20 au 30 nyuma uapatikanaji wa ngono ulikuwa rahisi kama sasa ambao ndiyo umezalisha single mothers wengi kuliko wakati wowote?

Zamani pombe ilikuwa ya watu wenye umri mkubwa na wazee, leo hii vijana wa kuanzia miaka 17+ wanakunywa pombe kupindukia mpaka wengine wamedhoofika kiafya.

Muziki umetapakaa na ndiyo kiburudisho muhimu wakati wakilewa.

Epuka kuwaona wengine hawana akili, fikiria kwa kina kabla ya kujibu hoja za watu.
 
Sasa hapo tatizo ni ngono na pombe au ni akili za wanaojipendekeza kwenye hivyo vitu?

Note: usinipangie namna ya kujibu , au kutoa maoni.
 
Single mothers wana tatizo gani ?
Unajua kiwango cha maambukizi ya magonjwa ya ngono ya Ukimwi, kisonono na kaswende miaka 30 nyuma ambapo ngono haikuwa inapatikana kirahisi kwa mujibu wenu kilikuaje kulinganisha na sasa??
 
Single mothers wana tatizo gani ?
Unajua kiwango cha maambukizi ya magonjwa ya ngono ya Ukimwi, kisonono na kaswende miaka 30 nyuma kilikuaje kulinganisha na sasa??
Kilichopo sasa ni ongezeko la watu, ndio maana tatizo likaonekana kubwa, ila hao wazamani nao walikua wachafu tu.
 
Kilichopo sasa ni ongezeko la watu, ndio maana tatizo likaonekana kubwa, ila hao wazamani nao walikua wachafu tu.
Na maendeleo ya mitandao ya kijamii na TV kila nyumba.
 
Juzi nipo mitaa ya mbagala nasikia singeli anaimba mwanaume wa dar anavaa uhusika wa mwanamke moja ya verse zake inasema hivi....

"Shoga wangu kama wewe malaya basi mimi malaya sugu"

Nasikitika kuwepo kwenye hiki kizazi I wish nisingekuwepo hiki kizazi.
 
Sasa hapo tatizo ni ngono na pombe au ni akili za wanaojipendekeza kwenye hivyo vitu?

Note: usinipangie namna ya kujibu , au kutoa maoni.
Kama ambavyo hutaki kupangiwa namna ya kujibu au kutoa maoni, basi na wewe tumia hiyo hiyo kanuni kutowapangia watu cha kuandika .

Usidharau wengine
 
Kweli kabisa pia vile vile matumizi mabaya ya mitandao,uangaliaji wa video chafu unaangamiza sana jamii zetu
 
Ni jangq tena sio kidogo miziki mingi siku hizi haijabeba ujumbe mzuri bali ni kusifia pombe,kuipamba ngono na kudhalilishq wanawake tofauti na miziki kama ya kina Ferooz ya ugonjwa wa ukimwi ulikua na ujumbe mzuri sana
 
Back
Top Bottom